Rais Samia akiingia katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar

Ndugu zangu Watanzania,

Ukimuangalia Rais Samia Unagundua ya kuwa Muda wote amejaa ari,nguvu na hamasa kubwa sana ya kufanya kazi. Unaona muda wote akiwa na morali na utayari wa kuwatumikia watanzania.unaona muda wote mawazo,akili,fikira na kiu yake ni kuwatumikia na kuwawazia watanzania.

Unaona Mungu akiendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.yupo imara kila muda na mwenye nguvu Utafikiri kijana wa miaka 30.Huyu Mama na Rais ni Bahati sana kuwa naye na kuongozwa naye.yupo imara kiakili na kimwili.

Embu angalia Alivyoingia na kuelekea katika kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri ikulu ndogo ya Tunguu visiwani Zanzibar hii leo.Hatua zake na mwendo wake na hata muonekano wake ni wakuleta matumaini kwa watanzania.Ni wakuleta tabasamu katika maisha ya watanzania.unaona wazi kwa jicho la tatu kuwa Huyu ni kiongozi tuliyemhitaji watanzania kutuongozaView attachment 3135089

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Nimependezewa na utembeajivwao.!
Wote wametanguliza mguu wa kulia mbele na mguu wa kushoto nyuma.
Mkono wa kushoto mbele na mkono wa kulia nyuma.
 
Hahaha hivyo ni vikao vya ndani vya ccm , na mambo yao ccm na mikakati yao ya kupika takwimu, lazima wakajifiche huko nchi za nje.
 
Mwaka kesho atakuwa na kampeni kuzunguka nchi nzima kuomba kura kwa watanzania wamchague kuwaongoza, tunamtakia afya njema na nguvu tele kuweza kufanya kampeni vema

..tumuombee apone kikohozi chake.

..ana laana ya kumcheka Jiwe kwamba alikufa kwa Korona.

Cc Etwege
 
Unaona Mungu akiendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.y
1729950716221.jpeg

Janabi ana wasiwasi na uzito unaozidi kila siku wa raisi wetu wewe unasema anaendelea kujaliwa afya njema, uko sawa wewe? Hebu mtafute Janabi akueleweshe.
 
Akiingia nayo ni story 😄 🤣 😂 😆 😄 Lucas Mwashambwa kwanini umekuwa chawa promax?
Kama alianza kuwa Chawa wangu Mimi Mwalimu wake nikiwa namfundisha Chuoni Ilala ili nimpe Marks za bure unategemea nini jipya labda kutoka Kwake Mkuu? Tena najilaumu kweli kweli kwanini alivyokuwa akijipendekeza vile Kwangu 'sikumpididi' kabisa ili aniheshimu hadi sasa.
 
Wewe hunaga akili kichwani mwako, ndio maana huwa nakupuuza tu na sioni sababu ya kubishana na mtu mjinga jinga.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ukimuangalia Rais Samia Unagundua ya kuwa Muda wote amejaa ari,nguvu na hamasa kubwa sana ya kufanya kazi. Unaona muda wote akiwa na morali na utayari wa kuwatumikia watanzania.unaona muda wote mawazo,akili,fikira na kiu yake ni kuwatumikia na kuwawazia watanzania.

Unaona Mungu akiendelea kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kututumikia watanzania.yupo imara kila muda na mwenye nguvu Utafikiri kijana wa miaka 30.Huyu Mama na Rais ni Bahati sana kuwa naye na kuongozwa naye.yupo imara kiakili na kimwili.

Embu angalia Alivyoingia na kuelekea katika kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri ikulu ndogo ya Tunguu visiwani Zanzibar hii leo.Hatua zake na mwendo wake na hata muonekano wake ni wakuleta matumaini kwa watanzania.Ni wakuleta tabasamu katika maisha ya watanzania.unaona wazi kwa jicho la tatu kuwa Huyu ni kiongozi tuliyemhitaji watanzania kutuongozaView attachment 3135089

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Anawatumikia watanzania au anafanya kazi ya urais ili alipwe mshahara wake? Kuwatumikia kwani anafanya kwa kujitolea?
 
Anawatumikia watanzania kwa moyo wa upendo, unyenyekevu, uzalendo na ukarimu wa hali ya juu sana
 
Back
Top Bottom