Kumbuka madaraka uliyo nayo sasa kwa mujibu wa katiba kuna watu hawakupendezwa uwe nayo.
Kama ujuavyo, watu hao wala si wa upinzani bali wa kijani wenzako.
Walisema waswahili kikulacho ki nguoni mwako.
Au unadhani walishakuridhia sasa na kila kitu wewe na wao ni shwari?
Hadi sasa kuna mengi umefanya. Hata hivyo tambua wanaokupongeza na kukukosoa kwa dhati ni watu kutokea upinzani peke yao. Kuwa macho na wanao kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
"Akili za kuambiwa Changanya na za kwako." -- JK.
Tulipo sasa tunaelekea kwenye kimbembe cha katiba mpya. Wapinzani wanakwambia ukweli kuhusu hili. Heri kwako ungewasikiliza.
Kujaribu kuzuia au kuuchelewesha ujio wa katiba mpya kutakugharimu wewe binafsi kisiasa, kinyume na wanavyo kushauri. Bado kuizuia haitakuwa rahisi.
Mivutano na ujanja ujanja vya nini? Kama watu wanataka katiba mpya si uwasikilize?
Utawalazimisha kinyume na matakwa yao kwa gharama ipi?