Rais Samia, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Rais Samia, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Naomba niambie tatizo la katiba iliyopo?
Katiba iliyopo imejivua nguo pale iliporuhusu Rais wa JMT asishtakiwe kwa lolote atakalofanya akiwa madarakani.

Hapa ni sawa na kusema Katiba iliyopo iliyojazwa viraka imejishusha na kumpandisha Rais awe juu yake.

Kwasababu Rais anaweza kuvunja sheria zote zilizopo ndani ya Katiba ya sasa apendavyo na asishtakiwe popote.

Hii maana kwa maana nyingine ni sawa na kusema Rais wa nchi ndie Katiba yetu ya sasa, yeye ndie anatuongoza kwa sheria zake apendazo, na bahati mbaya kwetu hadi vyombo vya dola vinamtii hivyo tunageuzwa watumwa ndani ya taifa letu.
 
Nitajie faida na hasara za viongozi wa mihimili kushitakiwa..
Dogo una maswali ya kukariri ya form two, big up!.

Ok, faida ya viongozi kushtakiwa;

- Wataogopa kuvunja sheria za nchi hovyo.

- Itaondoa kulindana.

- Uwajibikaji utaongezeka na hili kwa kiasi kikubwa litachochea kasi ya maendeleo ya nchi.

- Haki itakuwepo kwa wote bila kujali itikadi za vyama vyao, kwani sasa Katiba iliyopo inatoa haki hizo kwa kikundi fulani cha watu ili kulinda interest zao [ Kipilimba, Kingai etc].

-

Hasara.

Hakuna.
 
Kumbuka madaraka uliyo nayo sasa kwa mujibu wa katiba kuna watu hawakupendezwa uwe nayo.

Kama ujuavyo, watu hao wala si wa upinzani bali wa kijani wenzako.

Walisema waswahili kikulacho ki ngumu mwako.

Au unadhani walishakuridhia sasa na kila kitu wewe na wao ni shwari?

Hadi sasa kuna mengi umefanya. Hata hivyo tambua wanaokupongeza na kukukosoa kwa dhati ni watu kutokea upinzani peke yao. Kuwa macho na wanao kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

"Akili za kuambiwa Changanya na za kwako." -- JK.

Tulipo sasa tunaelekea kwenye kimbembe cha katiba mpya. Wapinzani wanakwambia ukweli kuhusu hili. Heri kwako ungewasikiliza.

Kujaribu kuzuia au kuuchelewesha ujio wa katiba mpya kutakugharimu wewe binafsi kisiasa, kinyume na wanavyo kushauri. Bado kuizuia haitakuwa rahisi.

Mivutano na ujanja vya nini? Kama watu wanataka katiba mpya si uwasikilize?

Utawalazimisha kinyume na matakwa yao kwa gharama ipi?
Usimtishe Rais wetu. Hakuna hao unadhani wanaweza kuandamana.

Katiba mpya Mimi naiona mwaka 2042. Sio sasa
 
Mambo haya 8 ndio yanahitaji katiba mpya? Maana hapa ndio wametaja(huko ulipoitoa hiyo screenshot) mambo Muhimu kuliko mambo yote..

Kingine uache Copy and Paste, badala yake toa mawazo yako kulingana na uelewa wako..

Hata kuhesabu pia hujui?

Point #8 inasoma nk, nk. Point hiyo ina points zingine ngapi ndani yake?

Screenshot hiyo ilikuwa ni katika kukukaribisha duniani. Ndiyo maana sentensi ya kwanza tu ilikuwa - "yameongelewa sana humu."

Ukiyataka zaidi yako kwenye uzi huu pia:

Katiba Mpya: Heri Rais Samia akaruhusu mchakato, asisubiri mashinikizo

Screenshot iliyokukera ni comment #31.

Huo uzi na comment hiyo umezielewa mwandishi wake?

Hata kama zisingekuwa zangu jifunze kuthamini mawazo yaliyopo tayari.

"Kutengeneza gari si lazima kuanza upya na magurudumu mstatili wakati duara yameshafahamika kuwa yanafaa!"

Ustaarabu ni kujenga kutokea katika vilivyopo.

Umri gani duniani mjomba?
 
Msituchonganishe wananchi na serikali yetu pendwa hayo makelele yenu ya mavitu yasiyo na tija kwa mwananchi wa kawaida anayeihitaji maji,elimu,umeme na barabara na anaona vinatekelezwa kwa kasi sana huku miradi ikizunduliwa kila kukicha.

Nendeni mkatafute katiba mpya za vyama vyenu kwanza, haiwezekani wenye viti wa vyama vya upinzani ni kama wafalme kikiwemo cdm tungu wengine tupo vijana wadogo tumekuwa watu wazima mwenye kiti ni huyo huyo tu

Na huyo katibu mkuu utafikiri amechimbiwa chini yaani hang'atuki pia ubinafsi na uonevu ni mwingi au mnajisikia ni sawa kuona wale akina mama wa viti maalumu wanao nyanyaswa wakiwa bungeni sasa katibu mkuu alipeleka majina NEC baada ya kupitishwa na chama chao kwaajili ya tamaa za watu wachache wanawageuka hapo kuna haki kweki.

Acheni mambo yenu.
 
Usimtishe Rais wetu. Hakuna hao unadhani wanaweza kuandamana. Katiba mpya Mimi naiona mwaka 2042. Sio sasa

Unasoma wapi vitisho? Kuchanganya akili zake kwenye porojo zenu ndiyo vitisho?

IMG_20220305_151655_415.jpg
 
Nitajie faida na hasara za viongozi wa mihimili kushitakiwa..
Wewe unapotezea muda wa watu. Hata wangekueleza nini, sidhani kama una akili ya kuelrwa chochote.

Maadam watanzania wenye uelewa walikwishatamka kuwa wanataka katiba mpya, hakuna wakubadili.

Ni mjinga tu ndiye anayeweza kufikiria kuwa maamuzi hayo ya wananchi anaweza kuyabadilisha.
 
Msituchonganishe wananchi na serikali yetu pendwa hayo makelele yenu ya mavitu yasiyo na tija kwa mwananchi wa kawaida anayeihitaji maji,elimu,umeme na barabara na anaona vinatekelezwa kwa kasi sana huku miradi ikizunduliwa kila kukicha.Nendeni mkatafute katiba mpya za vyama vyenu kwanza haiwezekani wenye viti wa vyama vya upinzani ni kama wafalme kikiwemo cdm tungu wengine tupo vijana wadogo tumekuwa watu wazima mwenye kiti ni huyo huyo tu na huyo katibu mkuu utafikiri amechimbiwa chini yaani hang'atuki pia ubinafsi na uonevu ni mwingi au mnajisikia ni sawa kuona wale akina mama wa viti maalumu wanao nyanyaswa wakiwa bungeni sasa katibu mkuu alipeleka majina NEC baada ya kupitishwa na chama chao kwaajili ya tamaa za watu wachache wanawageuka hapo kuna haki kweki.Acheni mambo yenu.
Acha wajadili watu wenye akili timamu.
 
Mbona kutaka kutuamuru oa kuanzia? Sisi tunataka kuanzia kwenye katiba yetu - katiba ya nchi.

Miaka 61 leo chama kile kile madarakani kikijipatia uhalali kupitia katiba ya nchi kinayoishinikiza kiujanja ujanja.

Tunataka Katiba Mpya itakayo waoa watu wote haki sawa.

Katika mpya ni sasa wala msijisumbue kujaribu kutuelekeza kwingineko.
 
HUYU mama ajihadhari sana na watu kama zitto kabwe kwenye uendeshaji wa nchi nadhani watanzania halisi wanajuwa unafiki wa HUYU dogo ,leo dunia ya Sasa huwezi endesha nchi kwa mawazo ya kina zitto kabwe,Steve Nyerere,masanja mkandamizaji,kigogo2014,suphian juma,kangi lugola,Polepole,msukuma,KiBAJAJI,gwajiboy,na pascal Mayalla,nk.
 
Kumbuka madaraka uliyo nayo sasa kwa mujibu wa katiba kuna watu hawakupendezwa uwe nayo.

Kama ujuavyo, watu hao wala si wa upinzani bali wa kijani wenzako.

Walisema waswahili kikulacho ki ngumu mwako.

Au unadhani walishakuridhia sasa na kila kitu wewe na wao ni shwari?

Hadi sasa kuna mengi umefanya. Hata hivyo tambua wanaokupongeza na kukukosoa kwa dhati ni watu kutokea upinzani peke yao. Kuwa macho na wanao kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

"Akili za kuambiwa Changanya na za kwako." -- JK.

Tulipo sasa tunaelekea kwenye kimbembe cha katiba mpya. Wapinzani wanakwambia ukweli kuhusu hili. Heri kwako ungewasikiliza.

Kujaribu kuzuia au kuuchelewesha ujio wa katiba mpya kutakugharimu wewe binafsi kisiasa, kinyume na wanavyo kushauri. Bado kuizuia haitakuwa rahisi.

Mivutano na ujanja vya nini? Kama watu wanataka katiba mpya si uwasikilize?

Utawalazimisha kinyume na matakwa yao kwa gharama ipi?
Nikajua umeandika cha maana kumbe ni ngonjera za Katiba mpya.

Kama wapinzani mna watu si komaeni vinginevyo Katiba itabakia kuwa hisani ya CCM na Rais in particular.
 
Nikajua umeandika cha maana kumbe ni ngonjera za Katiba mpya.

Kama wapinzani mna watu si komaeni vinginevyo Katiba itabakia kuwa hisani ya CCM na Rais in particular.

Kwani la maana ni lipi ndugu?

Au kwani la maana kwako ndiko la maana kwa dunia nzima?

Kwamba hudhani katika porojo zenu ni la msingi akaachanganya na akili zake?

Ama kweli kuna watu na makerubi.
 
Kwani la maana ni lipi ndugu?

Au kwani la maana kwako ndiko la maana kwa dunia nzima?

Kwamba hudhani katika porojo zenu ni la msingi akaachanganya na akili zake?

Ama kweli kuna watu na makerubi.
Katiba haiombwi inadaiwa,nyie sina watu? Tumieni hao kudai.

Watu wako busy na maisha wewe unaleta hadithi za kutoa ccm kuweka chadema.
 
Back
Top Bottom