Rais Samia, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Rais Samia, akili za kuambiwa changanya na za kwako

Kumbuka madaraka uliyo nayo sasa kwa mujibu wa katiba kuna watu hawakupendezwa uwe nayo.

Kama ujuavyo, watu hao wala si wa upinzani bali wa kijani wenzako.

Walisema waswahili kikulacho ki nguoni mwako.

Au unadhani walishakuridhia sasa na kila kitu wewe na wao ni shwari?

Hadi sasa kuna mengi umefanya. Hata hivyo tambua wanaokupongeza na kukukosoa kwa dhati ni watu kutokea upinzani peke yao. Kuwa macho na wanao kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

"Akili za kuambiwa Changanya na za kwako." -- JK.

Tulipo sasa tunaelekea kwenye kimbembe cha katiba mpya. Wapinzani wanakwambia ukweli kuhusu hili. Heri kwako ungewasikiliza.

Kujaribu kuzuia au kuuchelewesha ujio wa katiba mpya kutakugharimu wewe binafsi kisiasa, kinyume na wanavyo kushauri. Bado kuizuia haitakuwa rahisi.

Mivutano na ujanja ujanja vya nini? Kama watu wanataka katiba mpya si uwasikilize?

Utawalazimisha kinyume na matakwa yao kwa gharama ipi?
Wako pia wachama pinzani hawampendi huyu mama, hawa viumbe ni wadini na wakabila haswaa.

Kuhusu katiba mpya, navyoona zaidi ni chama pinzani/kaskazini ndiyo wanaodai katiba , na wachache kutoka chama tawala.
 
Huku kuona kwako ni kwa vigezo vipi mkuu, mbona wengine nasi tunaona kuona kwako hakuko sahihi?

Zingatia vigezo hivyo. Kote alipofanya vizuri kunatambuliwa na kupongezwa.

Vigezo vyako vya kuona kwako viko wapi?
 
Naomba niambie tatizo la katiba iliyopo?
Hata maiti haiwezi kuuliza swali hilo! Taifa limetumia mabilioni ya fedha kugharimia Tume ya Warioba kuandika katiba mpya halafu punguani fulani anajitokeza kutokuona tatizo!
 
Mimi nimemaliza mkuu.

Nahamia kwako,, je una uhakika gani ama kigezo gani umetumia kama wengi wao wanahitaji katiba?

Kwamba umemaliza? Bila shaka umeshindwa kuweka vigezo vyovyote.

Kwa hali hiyo ninakuribisha kwangu kwa mikono miwili, uhamie kabisa.

Matatizo ya katiba iliyopo ni kama yalivyo ainishwa kwenye post #11 na #27 kwenye uzi huu.

Nani asiyetaka katiba mpya kwenye hali ambapo:

IMG_20220324_225211_042.jpg

Nani asiyetaka kutendewa haki?

Yumkini hata wewe unataka katiba mpya ila hujijui tu.
 
Kwamba umemaliza? Bila shaka umeshindwa kuweka vigezo vyovyote.

Kwa hali hiyo ninakuribisha kwangu kwa mikono miwili, uhamie kabisa.

Matatizo ya katiba iliyopo ni kama yalivyo ainishwa kwenye post #11 na #27 kwenye uzi huu.

Nani asiyetaka katiba mpya kwenye hali ambapo:

View attachment 2163954

Nani asiyetaka kutendewa haki?

Yumkini hata wewe unataka katiba mpya ila hujijui tu.

Nimekupata chief, haki kwangu ndio kipaumbele
 
we huon ina mapungufu?hyo ilitungwa enzi ya chama kimoja katiba sio msahafu useme isibadilishwe
 
Back
Top Bottom