Rais Samia akiri kuwepo upungufu wa umeme, Makamba alisema ni 'scheduled maintainance'

IPTL muda wao huu...kuwasha mitambo...
Kazi iendelee
 
Mbona joto limezidi hivi Tanzania au mjambiani kajamba moto nini?
 
Njia ya muongo na mnafiki ni fupi. Wote tusiwaamini maana kwanza inaonesha ni jinsi gani rahisi hawasiliani na watendaji wake ndio maana wanapishana kwenye kutoa information.
 
Wanaturudisha enzi za Mkapa, Karamagi na Msabaha.
Aggreco, IPTL, Majenereta etc

Wakaja na Symbion na kutuahidi kukatika umeme is history. Wakaona haitoshi wakasema Sasa tunatumia gesi yetu kukatika umeme is history wakaongeza Songas bado Mambo yako pale pale, huku wakiendelea kuuza Majenereta na solar panels.

Wakaja na mradi wa JN Stiegler's gorge, nasikia huko Mambo si Mambo, maji yalitakiwa yaanze kujazwa juzi lkn Sasa hivi Ni until further notice.

SI WAACHIE NGAZI WAMPE HASHIM RUNGWE TUJILIE PILAU
 
Hiki hapa ndicho TANESCO wanasema. Swali: Kwa nini iwe ghafa namna hii? Kipi kilichotokea ambacho kwa miaka 5 mfululizo ya Jiwe hakikuweza kutokea? Eti hydropower plants zetu zote zimekaukiwa maji. Ndicho sasa Tanesco wanasema.
===
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema linachukua hatua za haraka kwa kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia.
Hatua hizo ni kutokana na mabadiliko ya hali hewa, kupungua kwa kiwango cha maji katika mito na mabwawa nchini.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 18, 2021 imesema hali ya upungufu huo imeathiri uzalishaji katika vituo vya kuzalishia umeme vinavyotumia maji.

“Athari kubwa imetokea katika vituo vyetu vya Kihansi, Kidatu na Pangani. Jumla ya upungufu wa uzalishaji ni nakribani megawati 345 ambayo ni asilimia 21 ya uzalishaji wote” imesema.

Hata hivyo shirika hilo limesema linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia kwa kuharakisha matengenezo ya baadhi ya mitambo yake ya Ubungo I inayozalisha megawati 25.

Vituo vingine ni Kinyerezi I megawati 185, Ubungo III megawati 112, pamojqa na kuwasha kituo cha Nyakato kinachozalisha megawati 36 hali itakayofanya kuwa na jumla ya megawati 358.

“Kwakuwa kutakuwa na upungufu kwa baadhi ya mikoa taarifa zitatolewa kwa wakati ili wateja waweze kupanga kazi zao”. Imeeleza.
 
Umeme utaletwa na ilani ya chama.
 
Kwa sisi tuliofanya kazi serikalini ninakubaliana na wewe. Uzembe, ulevi, uzinzi, wizi wa kudanganya, nepotisma na uvivu vimetawala sana kwenye ofisi za serikali na mashirika ya umma. Si unasikia siku hizi kwenye mitando wakisema kama mke wako ameajiriwa huko jiandae kisaikoloji maana watampitia tu. Hukijaribu kuwa muungwana either ufanyiwe majungu ufukuzwe kazi au upewe demotion. Hayo yalinikuta. Kuweka mtoto wa dada na wa shemeji bila kuangalia vigezo vinaua hii nchi sana. Hi nchi inatakiwa kuundwa upya na kugeuza mind set ya watanzania kuwa na uzalendo wa nchi yao.

Hii nchi inatakiwa kuwa na vingozi wa kusema kweli, kutowabagua watanzania, wenye kutenda haki na wenye kukubali katiba mpya na kuwa wakali sana kwa watu wazembe. Yaani tunatakiwa kufika sehemu ya kuweka system ya kumwajibisha hata raisi wa nchi pale anapoharibu. Hapo raisi atakuwa makini sana na watu anaowaweka madarakani ili wasimchafue.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…