Rais Samia akiri kuwepo upungufu wa umeme, Makamba alisema ni 'scheduled maintainance'

Rais Samia akiri kuwepo upungufu wa umeme, Makamba alisema ni 'scheduled maintainance'

Rais Samia akiwa mkoani Mwanza amesema anatambua uwepo wa upungufu wa umeme ikimaanisha vyanzo vilivyopo havikidhi mahitaji yaliyopo. Waziri wetu wa nishati aliliongelea suala la kukatikatika kwa umeme chanzo chake ni marekebisho ya mfumo wa zamani.

Tunaandaliwa kwa umeme wa dharura?
IPTL muda wao huu...kuwasha mitambo...
Kazi iendelee
 
Rais Samia akiwa mkoani Mwanza amesema anatambua uwepo wa upungufu wa umeme ikimaanisha vyanzo vilivyopo havikidhi mahitaji yaliyopo. Waziri wetu wa nishati aliliongelea suala la kukatikatika kwa umeme chanzo chake ni marekebisho ya mfumo wa zamani.

Tunaandaliwa kwa umeme wa dharura?
Mbona joto limezidi hivi Tanzania au mjambiani kajamba moto nini?
 
Makamba: Hakuna mgao wa umeme bali ni matengenezo ya kawaida.

Samia: Kuna upungufu mkubwa kwenye vyanzo vya maji hali inayopelekea mgao wa umeme na maji kutoepukika.

Tumwamini nani kati ya mkuu wa Nchi na Waziri wake?!

Juzi niliuliza humu hivi Makamba anatufanya sisi ni mapunguani na hadi muda huu anasubiri nini ofisini?!
Njia ya muongo na mnafiki ni fupi. Wote tusiwaamini maana kwanza inaonesha ni jinsi gani rahisi hawasiliani na watendaji wake ndio maana wanapishana kwenye kutoa information.
 
Wanaturudisha enzi za Mkapa, Karamagi na Msabaha.
Aggreco, IPTL, Majenereta etc

Wakaja na Symbion na kutuahidi kukatika umeme is history. Wakaona haitoshi wakasema Sasa tunatumia gesi yetu kukatika umeme is history wakaongeza Songas bado Mambo yako pale pale, huku wakiendelea kuuza Majenereta na solar panels.

Wakaja na mradi wa JN Stiegler's gorge, nasikia huko Mambo si Mambo, maji yalitakiwa yaanze kujazwa juzi lkn Sasa hivi Ni until further notice.

SI WAACHIE NGAZI WAMPE HASHIM RUNGWE TUJILIE PILAU
 
Rais Samia akiwa mkoani Mwanza amesema anatambua uwepo wa upungufu wa umeme ikimaanisha vyanzo vilivyopo havikidhi mahitaji yaliyopo. Waziri wetu wa nishati aliliongelea suala la kukatikatika kwa umeme chanzo chake ni marekebisho ya mfumo wa zamani.

Tunaandaliwa kwa umeme wa dharura?


View attachment 2015320
Hiki hapa ndicho TANESCO wanasema. Swali: Kwa nini iwe ghafa namna hii? Kipi kilichotokea ambacho kwa miaka 5 mfululizo ya Jiwe hakikuweza kutokea? Eti hydropower plants zetu zote zimekaukiwa maji. Ndicho sasa Tanesco wanasema.
===
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema linachukua hatua za haraka kwa kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia.
Hatua hizo ni kutokana na mabadiliko ya hali hewa, kupungua kwa kiwango cha maji katika mito na mabwawa nchini.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 18, 2021 imesema hali ya upungufu huo imeathiri uzalishaji katika vituo vya kuzalishia umeme vinavyotumia maji.

“Athari kubwa imetokea katika vituo vyetu vya Kihansi, Kidatu na Pangani. Jumla ya upungufu wa uzalishaji ni nakribani megawati 345 ambayo ni asilimia 21 ya uzalishaji wote” imesema.

Hata hivyo shirika hilo limesema linachukua hatua za haraka kuongeza uzalishaji kwa kutumia gesi asilia kwa kuharakisha matengenezo ya baadhi ya mitambo yake ya Ubungo I inayozalisha megawati 25.

Vituo vingine ni Kinyerezi I megawati 185, Ubungo III megawati 112, pamojqa na kuwasha kituo cha Nyakato kinachozalisha megawati 36 hali itakayofanya kuwa na jumla ya megawati 358.

“Kwakuwa kutakuwa na upungufu kwa baadhi ya mikoa taarifa zitatolewa kwa wakati ili wateja waweze kupanga kazi zao”. Imeeleza.
 
Tanzania sio nchi ya kuwa na mgao wa umeme...

Mazingira yana support tuwe na umeme wa kutosha kabisa... unless akili ndogo za viongozi...

Watu walitengeneza ardhi zenye rutuba na wanalima mboga na matunda jangwani, sisi tunashindwa nini??

Hakuna maendeleo yatakuja eti umejiandaa vyema kabisa, yaani upo perfect, hayo ni mawazo ya watu wenye uwezo duni wa kufikiri... start with what you have to get where you want to go...

Unaogopa miradi mikubwa kisa nini, tumefuta miaka 60 na hatujafanya cha maana kwa sababu ya huu ujinga...

Ngoja tuwaache waendelee kusubiri Tanzania iwe na pesa nyiiingiiiii, iwe na matrilioni ndipo wafanye miradi mikubwa....
Umeme utaletwa na ilani ya chama.
 
Huwa nasikitika Sana wanapolaumiwa wachezaji football wa Tanzania kuwa hawajui au hawapo serious pale timu yetu ya taifa inapofanya vibaya. Vijana hawa hulaumiwa sbb kazi yao hufanyikia hadharani ambapo na mashabiki hualikwa kushuhudia matokeo ya kazi yao.

Naamini kama na watendaji wa ofisi za umma wangekuwa wanafanyia kazi zao za kitaalam ktk majukwaa ya wazi na si ktk vi ofisi tena vyenye mafaili yaliyoandikwa SIRI wallah Watanzania tungeitisha mjadala wa kitaifa kutafuta suluhu ya matatizo ya uwajibikaji kati yetu. Serikalini kuna watendaji wabovu zaidi ya hawa wacheza football tunao watukana kila uchao.

Ni watendaji hawahawa wameshindwa kutengeneza miundombinu ya kuandaa wachezaji watetezi wa taifa wa kesho. Badala yake huishia kufanya mipango ya zimamoto kutaka matokeo ambayo wenzetu wamewekeza akili, maarifa, pesa na utaalam kuyapata.
Kwa sisi tuliofanya kazi serikalini ninakubaliana na wewe. Uzembe, ulevi, uzinzi, wizi wa kudanganya, nepotisma na uvivu vimetawala sana kwenye ofisi za serikali na mashirika ya umma. Si unasikia siku hizi kwenye mitando wakisema kama mke wako ameajiriwa huko jiandae kisaikoloji maana watampitia tu. Hukijaribu kuwa muungwana either ufanyiwe majungu ufukuzwe kazi au upewe demotion. Hayo yalinikuta. Kuweka mtoto wa dada na wa shemeji bila kuangalia vigezo vinaua hii nchi sana. Hi nchi inatakiwa kuundwa upya na kugeuza mind set ya watanzania kuwa na uzalendo wa nchi yao.

Hii nchi inatakiwa kuwa na vingozi wa kusema kweli, kutowabagua watanzania, wenye kutenda haki na wenye kukubali katiba mpya na kuwa wakali sana kwa watu wazembe. Yaani tunatakiwa kufika sehemu ya kuweka system ya kumwajibisha hata raisi wa nchi pale anapoharibu. Hapo raisi atakuwa makini sana na watu anaowaweka madarakani ili wasimchafue.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom