Rais Samia akiri miaka 45 ya CCM ndani ya 30 ya Upinzani haijawa rahisi

Rais Samia akiri miaka 45 ya CCM ndani ya 30 ya Upinzani haijawa rahisi

Mwanahabari wa Taifa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2020
Posts
1,588
Reaction score
956
===
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake Mkoani Mara yalikofanyika maazimisho ya miaka 45 ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) kitaifa,

Pamoja na mambo mengine Rais Samia Suluhu Hassan amekiri CCM kubakia imara ndani ya kipindi cha Vyama vingi haikuwa jambo rahisi,

Aidha, Ndg Samia Suluhu Hassan amejivunia imani kubwa waliyonayo Watanzania kwa Chama Chao cha Mapinduzi na ndio imekuwa siri ya mafanikio ya ccm-tanzania wakati wote wa Uhai wake,

Ndg Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania waendelee kuiamini na kuichagua CCM katika kila Uchaguzi kwani ndio Chama kinachojibu maswali ya maisha yao yote,

Zaidi,Soma hii taarifa ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka aliyeitoa kwa Watanzania muda mchache baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo ya 45,

photo_2022-02-05_05-04-36.jpg

photo_2022-02-05_05-04-02.jpg
 
Ni Lowassa tu ndio aliweza kuitingisha CCM,

Ila kwa Upinzania uliopo CCM itatawala zaidi ya miaka 100

Karibu CCM kama unataka kufanya Siasa za matokeo,
 
Uchaguzi wa 2020, ungekuwa halali na huru, Tundu Lissu angemuacha mbali sana Magufuli na ndio ingekuwa kifo cha ccm
Mama yangu huk9 kijijini alinisimulia alipita karibu na kituo cha kura alfajiri akaitwa akapige kura kabla ya wakati na alikuta masanduku yashajaa kura na ilikua kabla ya muda rasmi wa kufungua vituo.

Ile laana ya 2020 ndo ilibadili historia kwa rais kufia madarakani.
 
CCM kiuhalali uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 ilikuwa kicked to the touch,President Nyerere wakati alishastaafu siasa akaingilia kati uchaguzi ule kuanzia ccm hadi uchaguzi mkuu akauvuruga mno(kuna watanzania walitaka atangazwe mtakatifu!!);NCCR M ilishinda uchaguzi ule na ccm kwa makusudi mazima walivuruga uchaguzi wa Dar es Salaam bila soni ,makaratasi ya kupigia kura yamefika mapema huku Lingusenguse ila yamechelewa kufika pale kariakoo!!
 
Mkuu 1995 NCCR hawakushinda hata ukimuuliza mzee Mrema anamajibu,
 
Hata mfanyeje, ccm ya leo hsipo kwa ajili ya watanzania.
 
Ni Lowassa tu ndio aliweza kuitingisha CCM,

Ila kwa Upinzania uliopo CCM itatawala zaidi ya miaka 100

Karibu CCM kama unataka kufanya Siasa za matokeo,
Ni kwa aina ya vyombo vya ulinzi na usalama ndivyo ambavyo ni salama pekee kwa CCM kubakia madarakani. CCM ni dhoofu sana haina uwezo wa kupambana kihalali na vyama makini vya upinzani.

Toka mwaka 1995 kwa upande wa Zanzibar, na toka mwaka 2010 kwa upande wa Bara, CCM inashinda kwa figisu tu. Inabebwa na ZEC pamoja na NEC, hakujawahi kuwa "fair political space" katika majumuisho ya kupata kura halali zenye kuweza kuaminika na kumtangaza kuongozi halali atokanaye na CCM.

Hoja kuwa upinzani ni dhaifu haina mashiko na yenye kupaswa kupuuzwa. Kama la, basi CCM iridhie tume huru ya uchaguzi ama katiba mpya kabla ya mwaka 2024 ili wale wote wenye mashaka waone matokeo yake.
 
Chadema simmesema mnataka Katibu sio tume huru au sikuelewa,
 
===
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake leo Mkoani Mara yalikofanyika maazimisho ya miaka 45 ya CCM kitaifa,

Rais Samia Suluhu Hassan amekiri CCM kubakia imara ndani ya kipindi cha Vyama vingi haikuwa jambo rahisi,

Aidha, Ndg Samia Suluhu Hassan amejivunia imani kubwa waliyonayo Watanzania kwa Chama chao cha Mapinduzi na ndio imekuwa siri ya mafanikio ya ccm-tanzania wakati wote,

Zaidi,Soma taarifa ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka kwa Watanzania

View attachment 2109211

View attachment 2109217
Shaka Hamdu Shaka anakasi nzuri sana,
 
Back
Top Bottom