Rais Samia akishiriki Baraza la Eid El-Fitri kumbi wa JNICC Machi 31, 2025

Rais Samia akishiriki Baraza la Eid El-Fitri kumbi wa JNICC Machi 31, 2025

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais Samia akishiriki Baraza la Eid El-Fitri kumbi wa JNICC Dar es salaam, leo tarehe 31 Machi, 2025.


Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Alhaj Nuhu Jabiri, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Aidha, amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kufanyia kazi dosari zilizoripotiwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita na kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.

"Kupitia jukwaa hili, tunaziomba mamlaka za Serikali kuzifanyia kazi dosari zilizoripotiwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopita na kusisitiza suala la kutenda haki katika kila hatua ya mchakato wa uchaguzi, kwani haki ndiyo msingi mkuu wa amani. Tunatoa wito pia kwa vyama vya siasa pamoja na wagombea kuepuka vitendo vya rushwa, kwani rushwa ni adui wa haki"

Rais Samia: Serikali Haitovumilia Uchochezi wa Kidini

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania imeendelea kudumisha umoja na mshikamano kutokana na viongozi wa dini kuepuka mahubiri ya uchochezi na mafarakano.

Ameongeza kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua kali dhidi ya baadhi ya viongozi wa dini wenye mwelekeo wa kuhubiri chuki na uhasama dhidi ya Serikali.

"Tushikilie msimamo wa imani, udhibiti wa nafsi zetu na wajibu wetu katika kuikuza na kuitunza amani yetu nchini. Niwaombe katika madhehebu na makundi yenu mbalimbali muweze kuwadhibiti wale wachache miongoni mwenu walio na mwelekeo wa kuhubiri na kupandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya Serikali yao. Waache kufanya hivyo. Ni vyema sote tujue kuwa katika mifarakano na hasama hakuna atakayeibuka mshindi, bali kutatokea hasara na majanga,"

Uchaguzi Mkuu kufanyika kwa njia ya Haki, kwa kusimamia misingi yote ya Kanuni, Sheria na desturi zote za Uchaguzi, Falsafa ya 4R itaendelea kuwa moja ya nyezo kuu katika uchaguzi mkuu ujao
 
Viongozi wa Dini wamueleze ukweli kuwa kuiba kura ni dhambi, wamuambie ukweli.
 
Back
Top Bottom