Rais Samia akizindua mradi wa maji Kigamboni na kugawa mitambo ya Kuchimbia visima, Leo Novemba 11, 2022

TOKA MAKTABA :

Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda kata ya Serembala, Morogoro Kusini

MHE. PROSPER J. MBENA aliuliza:-
Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda lililopo katika kata ya Serembala, Morogoro Kusini umesababisha matatizo makubwa kwa wananchi wa kata ya Serembala, Magogoni na vijiji jirani kutokana na fidia kidogo kwa kupisha ujenzi wa mradi huo ikilinganishwa na mali walizoziachia yaani mashamba, nyumba zao na mali nyingine zilizo kwenye maeneo makubwa ya ardhi iliyochukuliwa kwa ajili ya mradi huo.

(a) Je, Serikali iko tayari kurudia zoezi la tathmini ya mali za wanavijiji wote walioathirika kwa kutoa nyumba na mashamba yao ili kupisha mradi wa bwawa la Kidunda na kuwalipa fidia wanayostahili?

(b) Je, Serikali iko tayari kwenye bajeti hii kumalizia malipo ya takribani shilingi bilioni 3.7 kuwafidia wananchi hao kulingana na tathmini iliyofanyika?

(c) Je, Serikali itakuwa tayari kuwawekea miundombinu ya uanzishwaji wa mashamba ya umwagiliaji na viwanda vidogo vidogo kwenye kata ya Serembala kwa ajili ya kutoa ajira kwa wananchi Serembala Magogoni, Mvuna na Kkata za jirani?

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Prosper Joseph Mbena, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-


Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaandaa malipo ya fidia kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 ambayo inaelekeza pia kuwa endapo malipo ya fidia yatachelewa kulipwa kwa zaidi ya miezi sita tangu kupitishwa, mlipaji anapaswa kufanya mapitio na kulipa nyongeza kutokana na muda uliozidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshalipa jumla ya shilingi bilioni 7.4 kwa familia 2,603 kama fidia ya kupisha ujenzi wa Bwawa la Kidunda.

Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa ajili ya fidia kulingana na tathmini iliyofanyika. Malipo yamekuwa yanafanyika kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bwawa la Kidunda linajengwa mahsusi kwa ajili ya kuhifadhi maji ya matumizi ya majumbani kwa wakazi wa Kibaha, Bagamoyo na Dar es Salaam. Bwawa hilo halitahusu kilimo kikubwa cha umwagiliaji. Serikali itaangalia uwezekano mwingine wa kuweka miundombinu wezeshi ya kilimo cha umwagiliaji kulingana na maeneo husika.(Makofi)
Source : Bunge Polis
 
Kwa bajeti ipi? Hiyo mitambo imeagizwa kutokana na fedha za uviko. Hakuna bilioni 700 alizotenga jiwe kwa kazi hiyo acheni kumpa sifa asizostahili.
Tunaofuatilia "hansard", tunajua hili lilizungumzwa bungeni. Ndio twauliza vi wapi hivyo vifaa vilivyopangiwa bajeti na kupitishwa bungeni 2020 - 2021!!???
 
Tunaofuatilia "hansard", tunajua hili lilizungumzwa bungeni. Ndio twauliza vi wapi hivyo vifaa vilivyopangiwa bajeti na kupitishwa bungeni 2020 - 202
Nafikiri viongozi na wataalamu wa wizara husika wangejikita kwenye kutatua chanagamoto na pia kuwa pro active
 
Mradi ulioshindikana toka enzi za Nyerere umewezekana chini ya SSH..

Bado mna maswali? Kwa wanawake.huyu ndio Rais atakayewapunguzia madhila ila wanaume zaidi ya kujitapa Hakuna kitu.
 
Hivi hivi vitu huwa haviwezi kufanya kazi hadi vizinduliwe na kiongozi kama Rais, Makamu wake au Waziri Mkuu?
Watajuaje kwamba walivyovila vimeshabalikiwa?

Walamba asali wajanja sana.
 
Wamesema pesa alizokopa Mh Samia kutoka IMF.
Hakuna kitu kinachonikera kama kumfanya hayati JPM kuwa ni mtakatifu halafu Samia ni shetani, naiona kama ni tabia ya kinafiki na ya watu waliozibiwa mianya yao ya kula kwani Samia kaingia na watu anaowapenda yeye.
 
Tangu lini ngombe wanasababisha ukame kwa kunywa maji??
 
Mradi unazinduliwa Kigamboni wakati wa kigamboni hawajawahi kutumia maji ya NUA, sijui DAWASCO sijui Duwasa, DAWASA--- tangu karne za Kitwana Kondo hadi muda huu navyoandika - aliyeliona bomba la maji kwenye nyumba ya mkazi wa kigamboni na aseme sasa... 98% wakazi wa huko wanajigemea kwa maji ya binafsi.

Siasa bana !!
 
cc: Mzee Sabodo
 

11 November 2022​

RAIS SAMIA AKIZINDUA MRADI WA MAJI KIGAMBONI NA KUGAWA MITAMBO YA KUCHIMBA VISAMA

Source : majiDigital Tanzania
 
Hii iingie kwenye rekodi haijawahi fanywa na Rais yeyote hapo kabla..

Hizi Ni Pesa za uviko 19,tunasubiria ambulances na magari ya kusambaza chanjo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…