Kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania , nyongeza ya mshahara wa wafanyakazi kila mwaka ni takwa la kisheria , limo ndani ya Katiba ya Nchi ambayo kila kiongozi mwenye akili timamu anapaswa kuifuata , hii ni kwa sababu aliapa kuilinda na kuitii .
Kwa Hiyo kwa Mama kuongeza mshahara kwa hizo 23.3 % si ajabu na wala si jambo la kushangaza , Kwa vile amefuata matakwa ya Katiba ya nchi kama inavyomuelekeza , nyongeza ya mshahara si mapendo ya Rais , amelazimishwa ndani ya Katiba , hakuna haja ya kumsifia as if Mshahara huo ameongeza kutoka nyumbani kwake , sana sana apongezwe kwa kuanza kuijua vizuri Katiba ya nchi .
Ikumbukwe kwamba sipingi nyongeza ya mshahara kwa Wafanyakazi wa Tanzania makapuku , waliosomeshwa namba kwa miaka 7 , isipokuwa nanyoosha tu maelezo kwamba KUPANDA KWA MSHAHARA SI HISANI YA RAIS , BALI NI MATAKWA YA KATIBA YA NCHI .
Naomba kuwasilisha .