Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Hivi Kwa nini hawa wafanya biashara wakubwa huwa wanakaa kudekadeka saana!!!

Huyu jamaa anaongoza Kwa kudeka, haishiwi kulalama kama litoto Fulani hivi, Mo, na Bakhlesa, sjawahi kuona wakideka hivyo
 
Afadhali,, cement itashuka bei, maana walimfanyia figisu mwanzoni, wakati ule cement ya dangote imeshamili mtaani, tulinunua mfuko wa saruji hadi Tsh 10,000 kutoka 15000.

Dikteta alimfanyia figisu za kutisha.
jiwe alikuwa na roho chafu ya uharibufu. roho yake haikupenda kuona vitu vipo stable.

alikuwa anafanya kila hila ku-destabilize.
 
Haya ndiyo majukumu ya Rais sasa, siyo kutafuta cheap popularity kwa watu wenye upeo finyu (Machinga, bodaboda, mamantilie na wauza nyanya wa Dumila), matokeo yake unaenda hadi kuzindua vyoo na kuwaambia watu waache mavi yao nyumbani. Hongera Mother
 
Yawezekana awamu ya tano hawakwenda sawa na huyu billionea !! Mama tunakusikuliza weye!! Mwendazake akitaka kuingia hadi uvunguni mwa hawa watu ili awakombe pesa zao.

December 2020 walikomba 500M kutoka kwenye account yake ya CRDB Mtwara branch, wanauliza wakaambiwa ni maelekezo kutoka juu. Jamaa wakachukia wakaona hizi Bank za kibongo hawafuati sheria wakahamishia account yao Bank Of Africa.

Mwendazake zake alikuwa akifanya ujambazi wa kimadaraka,kisha anajisifia mapato ya kodi yameongezeka kumbe ni unyang'anyi tu.
 
... huyu Mama PR iko juu sana kuliko mtangulizi! Chama kingekuwa makini, kama ilikuwa ni lazima wawili hawa washike madaraka ya juu, basi mtangulizi aliitakiwa awe msaidizi wa Mama toka mwanzo kabisa.
Hawezi akawa na PR kama ya Mkapa na Kikwete ambapo migodi ya Tanzania, serikali ilimiliki % ndogo sana na ushuru kiduchu. Wakati Magufuli share na kodi vilipanda exponentially!
Kama hatupigwi mahali popote sawa, lakini kama ni mtindo wa zile awamu 3&4 we are finished!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote

Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam

Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara

Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea

Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote

Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika

Kazi Iendelee

Jamaaa Lina Mihela kudadadeki........!!!!, kama ambavyo sina!
 
Hivi Kwa nini hawa wafanya biashara wakubwa huwa wanakaa kudekadeka saana!!!

Huyu jamaa anaongoza Kwa kudeka, haishiwi kulalama kama litoto Fulani hivi, Mo, na Bakhlesa, sjawahi kuona wakideka hivyo
Kamchape viboko au mkaripie aache kudeka mkuu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote

Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam

Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara

Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea

Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote

Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika

Kazi Iendelee

Safi sana MAMA. Mungu akulinde
 
Safi sana Rais samiah,mataifa kama amerika mara nyingine hukubali uwekezaji utakao lipa kodi zake pengine hata kuzisaidia(kampuni) katika kupunguza baadhi ya milolongo mirefu alimradi kampuni zinazalisha ajira nyingi na kujali wafanyakazi wake, sasa mjinga mwingine anaweza zuia kampuni inayoajiri watu 10,000 bila hata sababu za msingi that's mean haoni hatari za wananchi wake 10000 kukosa kazi,anaona sawa tu,tumetoka mbali sana tusirudie kosa.
 
Back
Top Bottom