Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Afadhali,, cement itashuka bei, maana walimfanyia figisu mwanzoni, wakati ule cement ya dangote imeshamili mtaani, tulinunua mfuko wa saruji hadi Tsh 10,000 kutoka 15000.

Dikteta alimfanyia figisu za kutisha.
never
 
Kodi pia ziangaliwe upya unakuta product moja inalipiwa kodi mpaka mara tatu au Nne

Katika hotuba za Raisi Samia ameongelea sana jinsi ya utitiri wa Kodi na Urasimu ulivyojaa
Kwa sisi Watu wa kawaida tunachoomba ni Ajira ili twende Choo kwa amani
Hakika mkuu, bila ajira au mazingira mazuri ya kujiajiri maisha yanakuwa magumu sana
 
Wawekezaji wanazidi kumiminika Tanzania kufuatia uwepo wa mazingira rafiki na ya kuvutia yatakayofaidisha pande zote mbili mwekezaji mgeni na nchi ya Tanzania.

Juzi pia wawezeshaji European Business Group Tanzania forum European Union Business Group Tanzania – European Union Business Group Tanzania walifanikisha kongamano la European Investors Dialogue Tanzania walikuwa na kikao na wizara mbalimbali na kongamano la kujadili uwekezaji Tanzania

Mambo yanazidi kunoga ktk awamu ya sita upande wa kuwapa imani, mazingira na sera za kiushawishi za uwekezaji pamoja na diplomasia ya uchumi kuanza kuzaa matunda.

"Mabeberuuu"..... Mwangwi unatokomea. Mataga mpo???!
 
Magufuli alimsaidia sana Dangote katika uwekazaji. Alimsaidia sana. Naona watu msiofuatilia mambo mnamchafua Magufuli. Hebu ingieni hata You-tube tu huko mtaona mazungumzo yake na Rais Magufuli. Muacheni Mama Samia afanye kazi na mmuache Hayati John Pombe Magufuli apumzike kwa amani.
Angemsaidia dangote asingelalamika CBS kwamba serikali yake inachukua 16% undiluted share kwenye kampuni zao
 
Magufuli alimsaidia sana Dangote katika uwekazaji. Alimsaidia sana. Naona watu msiofuatilia mambo mnamchafua Magufuli. Hebu ingieni hata You-tube tu huko mtaona mazungumzo yake na Rais Magufuli. Muacheni Mama Samia afanye kazi na mmuache Hayati John Pombe Magufuli apumzike kwa amani.
Yeye ndio chanzo cha Dangote kupunguza uwekezaji Nchini,,
Never kivipi Sasa???? Eti binti
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote

Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam

Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara

Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea

Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote

Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika

Kazi Iendelee
Soo far She seem to be strategic and serious in revamping the current business and economical situation.
Let's hope for the better.
 
Kuna uwezekano mkubwa, Ikulu ya Chamwino haitaendelea kutumika.
Ikulu ni popote ... Halafu sasa Ikulu ambayo ilikuwa imepoteza matumizi angalau itapata matumizi na hakuna haja kusumbua watu kwenda Dodoma, biashara ya mahoteli itaanza kufufuka .. Kazi iendelee.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote

Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam

Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara

Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea

Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote

Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika

Kazi Iendelee

Tushukuru tumepata wafanyabiashara kama hawa hawana skendo za rushwa na wanaamini Waafrica.
 
Back
Top Bottom