Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Alhaji Aliko Dangote amesaidia sekta ya Ujenzi Ethiopia kwa kuuza Saruji yake kwa bei nafuu sasa hivi Waethiopia wanajenga wameachana na Nyumba za tembe kama ilivyokuwa Mkoa wa Singida
 
Enzi za Prof. Palamagamba Kabudi kuhodhi na kuleta ukiritimba wa habari kupitia kutusimulia kwa (kiSwahili) huku akiwazuia wawekezaji kuzungumza zimepita.

Leo tumemsikia mwenyewe bilionea mwekezaji Aliko Dangote (chungulia utajiri wake hapa : Aliko Dangote ) akipewa fursa kusema yake moja kwa moja na wasikilizaji / watazamaji wa tv / video kuwa anaridhishwa na kuwa kuna mabadiliko makubwa.


Dangote atakuwa balozi wetu maalum kuitangaza Tanzania kwa klabu za mabilionea wawekezaji kuwa Tanzania sasa mambo yamenoga na kuna fursa nzuri za uwekezaji.
 
Hao middle men ndio wanatakiwa kutoa hayo mnayodai. Dangote ameshashift responsibility.

Middle men wanaweza kutoa vyote vinavyodaiwa. Hii model ipo sehemu nyingi hajaanzisha Dangote.

Marekani kwa mfano hii model inatumika sana, na hao middle men wanatoa kila kitu mpaka kuchangia mafao na bima za afya.
 
Hatimaye makamanda uchwara waukubali muziki wa chama tawala.
Sio kuukubali mziki,la hasha! mnalazimisha Tume Mapolisi Askari wa Magereza na Dola nzima

Tunataka Tume HURU halafu tuingie kwenye uwanja sawa mkitushinda ndio lianze kubwabwaja.
 
... huyu Mama PR iko juu sana kuliko mtangulizi! Chama kingekuwa makini, kama ilikuwa ni lazima wawili hawa washike madaraka ya juu, basi mtangulizi aliitakiwa awe msaidizi wa Mama toka mwanzo kabisa.
Kila zama na kitabu chake. JPM alitufaa kwa wakati ule ila sasa twende na mama yetu kipenzi.
 
CCM hoyee!
 
Magufuli alimsaidia sana Dangote katika uwekazaji. Alimsaidia sana. Naona watu msiofuatilia mambo mnamchafua Magufuli. Hebu ingieni hata You-tube tu huko mtaona mazungumzo yake na Rais Magufuli. Muacheni Mama Samia afanye kazi na mmuache Hayati John Pombe Magufuli apumzike kwa amani.
 
Hao wafanyabiashara nao walipe kodi kama inavyostahiki. Kukwepa kodi kwa nchi kama Sweden ni aibu kama vile kutembea mtupu mbele na watoto wadogo.
Kodi pia ziangaliwe upya unakuta product moja inalipiwa kodi mpaka mara tatu au Nne

Katika hotuba za Raisi Samia ameongelea sana jinsi ya utitiri wa Kodi na Urasimu ulivyojaa
Kwa sisi Watu wa kawaida tunachoomba ni Ajira ili twende Choo kwa amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…