Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Morogoro ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo,uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwa ujenzi wa miradi mbalimbali,utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi.
Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,katika hali ya kuteka hisia za watu ameweza kuonana ana kwa ana Na Mwalimu wake Mama Sabina Gellejah ,aliyemfundisha alipokuwa mwanafunzi katika chuo hicho Mwaka 1983-1986 ambacho kwa sasa kinafahamika kama Mzumbe.
Kwa hakika Mungu ni Mwema sana .ukiangalia katika picha hii namna mama huyu alivyokuwa anaonesha uso wake uliojaa furaha na tabasamu mpaka unaona anatamani kutoa machozi ya furaha inagusa sana kiukweli.
Maana bila shaka Mama huyu haamini kama Ameweza kukutana uso kwa uso na Rais na Mkuu wa Nchi aliyepita mikononi mwake kama mwalimu wake. Haamini kama leo anaweza kupata nafasi ya kusalimiana na Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu.Haamini kama ni yeye aliyeingia katika kitabu cha historia cha kufundisha Mwanafunzi ambaye amekuja kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu.
Bila shaka moyo wake umebubujikwa na machozi ya furaha sana kuona amepata bahati ambayo wengi hawapati katika Maisha yao yote mpaka wanakufa ,kuweza kupewa heshima ya hadhi ya juu kabisa kusimama na Rais Na kushikwa mkono kusalimiwa na kutambulishwa.
Leo Tanzania nzima imetambua na kumfahamu miongoni mwa watu waliompika na kumuivisha Mama yetu. Kwa hakika Mungu amjalie Maisha Marefu sana Mama na Mwalimu huyu aliyetupikia na kumfundisha Rais wetu Mh Dkt Mama Samia ,ambaye leo kama Taifa Tunajivunia uwepo wake madarakani.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.