Rais Samia akutana na Viongozi wa TEC - Ikulu, Chamwino

Ulivyozumgumza hapa ni kama serekali yetu ni tajiri sana. Naona unajichanganya hadi unatolea mfano wa papa dhidi ya mabavu ya Marekani. Kwa taarifa yako hiyo US kuivamia Iraq sio pope tu hawakumsikiliza, bali hata Russia yenye kura ya veto ilipuuzwa, itakuwa Pope? Na kwakukusaidia tu, hiyo miradi ya Roman yenye udhamini wa serekali, hata serekali ikiondoa ufadhili nayo itadhurika kisawasawa.

Mfano halisi ni hospitali ya Bugando maana wauguzi wengine wanalipwa na serekali, hao watapoteza ajira, na itabidi serekali iwatafutie ajira mwingine, huku matibabu kwenye hospitali hiyo yakipanda maradufu. Serekali inayoweza kuleta jeuri ni ile iliyo madarakani kwa ridhaa ya wananchi, sio hiyo ya kura 31m za uongo, na mauaji juu.
 
Kumbe kilikuwa cha kkkt!
Hata Lowassa alipohamia chadema kugombea urais alisikika akiwaambia wezake (KKKT) "jamani sasa ni zamu yetu". Usifikiri wakristo wa madhehebu mengi ni wajinga hawaoni hawajui kwamba Nyerere, Mkapa na Magufuli ni wakatoliki wote. Na unadhani hawajui kuwa Nchimbi na Lissu ni wakatoliki pia.
 
Kanisa Katoliki halikufurahishwa na mkakati wa Rais JPM kuimarisha shule na hospitali za umma. Kanisa halifurahishwi na kubinafsishwa kwa bandari ambayo sasa inaipa nguvu za kifedha serikali kuboresha huduma za kijamii ambazo zitavutia jamii itumie huduma za umma badala ya kanisa. Kanisa huwa linafanya ile kitu wachumi wanachokiita SWOT analysis kabla ya kuanzisha mradi wowote. Miradi mingi ya kanisa imejengwa kwa kutarajia udhaifu/umaskini wa serikali kushindwa kuhudumia watu wake ipasavyo. Moja kati ya threats kwa miradi ya kanisa ni serikali kuwa tajiri na kutoa huduma bora kwa watu wake. Hivyo kanisa huwa lingashangilia serikali kuwa maskini na kutoa huduma dhaifu (shule na matibabu) kwa watu wake.

Mfano, kanisa halikupenda Nyerere kutaifisha baadhi ya shule za makanisa na kuzifanya ziwe za umma, kanisa lilimkasirikia JPM kujenga hospitali kubwa kanda ya ziwa itakayoshindana na Bugando kwenye huduma, kanisa lilimtaka JPM kuondoa ule mfumo wa udahiri wa wanafunzi kujiunga vyuoni (CAS) moja kwa moja kutoka kwenye mfumo badala yake vyuo vyenyewe vichague badala ya kuletewa.
 
Kuna mtu alimtonya kwamba, huwezi kushindana na hawa jamaa, kwa hiyo bila kupoteza muda waite kisha, bow down to them.
Huwezi kushindana nao kivipi? Serikali ilikuwa inawaheshimu kwasababu baada ya uhuru wao walikuwa na miundombinu mingi iliyoachwa na wakoloni kama vile shule na hospitali, lakini sio wakati huu ambao serikali inajenga shule kila kona na hospitali za mikoa na wilaya kila mkoa na wilaya na kuweka vifaa na wataalam. Siku sio nyingi hakutakuwa tena na hospitali za ubia.
 
Hata sielewi umeongea utoto gani kwenye hii orodha yako. Kutokupenda kunazuia anayetaka kufanya jambo asifanye? Maana hata Simba haipendi Yanga ifanikiwe na kinyume chake. Kuna popote kanisa limezuia serekali kufanya wajibu wake kwa mujibu wa sheria?
 
Hata sielewi umeongea utoto gani kwenye hii orodha yako. Kutokupenda kunazuia anayetaka kufanya jambo asifanye? Maana hata Simba haipendi Yanga ifanikiwe na kinyume chake. Kuna popote kanisa limezuia serekali kufanya wajibu wake kwa mujibu wa sheria?
Kanisa kazi yake ni kuomba na kuabudu tu, siasa na uchumi ni mambo ya kaisari.
 
Provision ya huduma ikoje? Serikali vs Private sector
Hospital kama malolo tabora ina huduma Bora(customer care included) kuliko za serikali na kanisa,milambo hospital tabora ilikua na huduma Bora zaidi kuliko kitete ya mkoa na st Ann ya kanisa, mpaka ilipokuja malolo
 
2021 Oktoba 17
Ndanda
Filamu kuhusu kazi ya kielimu katika Abasia ya Ndanda, Tanzania, na P Christof Wolf SJ na P Maximilian Grund OSB


View: https://m.youtube.com/watch?v=ktAhF9YOmsQ
 

St Benedict Hospital Ndanda Songea, Tanzania
"Kuwatunza wagonjwa lazima kutangulie kuliko kila kitu kingine."


View: https://m.youtube.com/watch?v=Qm440tGi5Vo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…