wajingawatu
JF-Expert Member
- Jan 20, 2013
- 2,633
- 3,463
Leo tumemalizana na "TEKE"View attachment 3647791View attachment 3647792View attachment 3647793
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Agosti, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoigusa jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.
Aidha, mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na Viongozi wa Dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa.
Soma Pia: Rais Samia amefanya mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Dar es Salaam
Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha Viongozi wa Dini na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.
View attachment 3647795
Kanisa pendwa KAKAKETI halina haja ya kuitwa ikulu.
Next up ni wavaa makobazi na sheikh ubwabwa.