PostGE2025 Rais Samia aliongoza Bunge kusimama kwa dakika 1 kuwaombea waliofariki kwenye vurugu siku ya uchaguzi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Leo kajitahidi kuweka kiburi pembeni. Itakuwa hapo kapikwa mpaka. Maana kwa akili yake angetoa maneno ya shombo bado. Sasa akili zinawaingia kuwa wenye nchi ni wananchi. Walijawa na viburi hawa wakajiona wao ndio wako juu ya wananchi. Jana Mwigulu anaanza story ya kubeba zege, sijui nini, ali mradi sasa wanajidai ni wanyonge wako pamoja na wananchi. Hatukubali maigizo. Tunahitaji mabadiliko ya kweli, ya dhati. Mmeshatubagaza vya kutosha. Hatuelewi kitu sasa hivi.
 
Taarifa ya tume ya Mzee Ali Kibao iko wapi? Huyu asifanye maigizo kwenye maisha ya watu, mwisho wake ni mbaya. Utekaji wote uliofanyika, taarifa ziko wapi? Including utekaji wa Mh Polepole. Nani ameshawahi kuwajibishwa kwenye mauaji na utekaji wowote tangu kaanza madaraka?
 
Kaanza vizuri, lakini mengine baada ya kuombea radhi, ni bado hajakubali uchaguzi ulikuwa sio wa haki, na linaonyesha dhahiri kuna juhudi za kupoza mambo Maisha yao waendele na siasa chafu
 
Damu za ndugu/wapendwa wetu alizozimwaga hazitamuacha salama!

MUNGU NAOMBA UMPE PIGO TAKATIFU NA WALE WOTE WALIOTEKELEZA HAYA MAUAJI.
 
Kuna wale machawa (chama cha mawakili wa serikali, bakwata na the like) waliokuwa wanalaani na kuwaita wahuni wale walio kufa na walioandamana sasa sijui watasahisha maneno yao.

Muda mwingine ukiruhusu sana njaa unarharaurika sana.
aseee sijui watafanyaje kwakweli! Maana bosi amesema tofauti kabisa!
 
Nakubaliana na wewe. Angalau serikali imekubali kulikua na mauaji ya raia. Ni hatua muhimu.
 
Pole ya nini Kwa watanganyika ilihali waliokufa ni raia wa nchi jirani? Huyu ni muuaji,hatupaswi kukaa naye meza moja
 
Uchunguzi wa kuuwawa kwa Mzee Ali Kibao uliishia wapi?
 
Na kwa unafiki mkuuu sana taasisi nyingi na watu mbali mbali chawa+kupe wanaoishi kwa kumtegemea mwanadamu wataanza kutoa pole ... Nakaa pale pembeni mtaona... Soon
Watajazana kutoa pole mpaka wakanyagane
 
Chanzo cha tatizo ni kukithiri kwa utekaji, kupotezwa na mauaji ya wapinzani na wakosoaji wa serikali yake ya CCM na uchaguzi wa maigizo wa kiinimacho ambao hata haukufanyika ndio ulikuwa njiti ya kuwasha moto.
 
Kwahiyo Gen Z tunafanyaje, D9 imekufa au jambo letu liko pale pale??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…