Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Tatizo unafanya personofication badala ya kuangalia mantiki ya hoja na nini implication yake kwa taifa letu.

Ukiangalia ile picha hata utamaduni wetu watanzania uliwekwa rehani. Imagine mtu baki anamshika Mama yetu pasi staha, kweli!

Yaani mimi nilijisikia vibaya sana kuona mtu kama mama yangu anashikwa na libaba nisilolifahamu...Kwakweli hili jambo limenisononesha mimi kama mtanzania moja, sijui wenzangu.

Lakini kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi, dhamira ya Rais wetu pengine ilikuwa njema ila tu hakujua ita imply nini kwa raia...Na mimi nauliza kweli Rais wetu analindwa? Mpambe wake kwanini alikubali haya? Je inaruhusiwa mpambe kuondoka nyuma ya Mh. Rais iwe kwa namna yeyote ile?

Mkumbuke bado hatuja pona kwenye vidonda vya Rais wetu kuaga dunia akiwa katika kazi ya urais na kwa wiki nzima haikujulikana alikuwa wapi, kisha baadaye wanaibuka watu ambao wana chuki isiyokifani tena wanakiri hadharani kuwa walikuwa wanamchukia...Hivi tunapata somo gani hapa?

Tujitafakari kama taifa!
Sijui imetokeaje lakini ni dhahiri nchi yetu inaongozwa na under age wengi hasa kwenye institutions za uongozi wa nchi, naamini unaelewa uwezo wa kufikiri wa mtoto, kijana na mtu mzima...mambo mengi yanavyofanyika yanaonyesha tunaongozwa na vijana vijana...akili yao inaona vitu vichache sana na umakini wa kazi wanazofanya ni mdogo.
 
Wa-TZ wenzangu!

Wakati wa Wikileak nilitambua walioendelea na hasa US wanatumia maafisa wa ubalozini ili kuzifahamu nchi walimo. Balozi zao zinatumika sana kuwaelewesha tabia za viongozi wetu; uwezo na udhaifu wao.

Ina maana Peter Greenberg alikuja akiwa director wa film lakini naaamini kupitia ubalozi wake alishafahamu tabia za rais wetu hadi mambo ya ndani, na ukiangalia film hii, rais alichotwa akili hadi akamuona ni rafiki kuliko hata sisi wa-TZ.

Ukiangalia Film ya Royal Tour kiutu uzima, (Siyo kama mtoto anayefurahia wanyama) inatia kichefu-chefu jinsi rais wa nchi alivyopunguziwa thamani hadi kufikia kuwa mcheza film akiwa ikulu. Walifikia hatua ya kuitana majina kama wana mahusiano ya ziada. Peter! Mama Samia!

Haya yangeondolewa wakati wa ku-edit! Nadhani yaliachwa makusudi na naamini kwa uhusiano huu Peter sasa atatumika kiurafiki kuwasiliana na rais moja kwa moja.

Kule twitter Maria Sarungi kaibua jingine nami nimethibitisha. Wamasai wanaitwa ni 'PRIMITIVE' na huyo director wa film na ikaachwa kama sehemu ya maelezo ya film ya Tanzania! Yaani tuna raia PRIMITIVE! Rais Samia anaambiwa Magufuli alipatwa na COVID anakubali, Yeah! wakati wa-TZ hatujawahi kuambiwa jambo kama hilo. Kwa nini haya yote yametokea?

Ikulu yetu haina usalama. Namaanisha watu wanaostahili kumulazimisha rais aendane na matakwa ya taifa na siyo uamuzi wake, hawapo na hawana nguvu hizo. Ina maana rais mzembe anaweza angamiza taifa. Tabia zake binafsi zinatambaa na anazungukwa na watu wa aina yake bila kizuizi.

Very, Very Sorry!
Huyo Peter (pil:ar) alichiwa sana! Yaani Wamasai ni Primitive!!! Rais wetu aliona ni sawa tu! Nadhani tukubali, mchakato wa kupata viongozi wetu uko dhaifu sana, na udhibiti wa marais wetu ni dhaifu sana!

Imenijia kumbukumbu ya rais Mwinyi kwenda kuangalia mziki wa Kanda Bongoman wakati madaktari wamegoma. Nimekumbuka Mkapa Kualikwa arusi ya mhindi mmoja na akaoneshwa anakamata rumba na Anna Mkapa.
Nimekumbuka Kikwete kusukumwa kichwa aingie kwenye gari wakati akimzubalia binti wa pembeni yake.
Sikuwahi kumuona Magufuli at that belittled level.
Sikuwahi kumuona Nyerere kwa mambo kama hayo wakati ndiye aliyeshika madaraka akiwa mdogo kwa umri kuliko hawa wote!!!
 
Wivu tu sukuma gang
Hi Peter (Pila)!
Ukiona mtu anaiga matamshi ya kimarekani uzeeni wakati hajawahi hata kuishi kwa mwezi mmoja, ni dalili ya "lack of character". Ukiwa wa aina hiyo unahangaika bila kueleweka; Ukiishi na mvuta sigara, unaanza kuvuta. Ukiishi na mpenda disko, unakwenda. Ukiishi na mpenda swara, unaingia msikitini. Sijui ukikutana na mashoga inakuwaje! Kila kitu wewe ni kuiga tu! Jamani, rais anaiga hata matamshi?????? Shiiida!

sasa filamu inatangazwa mkoa kwa mkoa kwa wa-TZ, wasiojua kiingereza, ili waiangalie kama katuni!
 
Back
Top Bottom