Irene Darton
Member
- Feb 25, 2024
- 18
- 22
Afya bora au Afya dhaifu ni kigezo cha kutambua uhai wa Taifa lolote, Afya bora ni matokeo ya mambo mengi na moja wapo likiwa ni huduma bora katika nyanja mbalimbali. Miaka kadhaa iliyopita mgonjwa kufanyiwa CT SCAN ilikuwa nadra na kwa hospitali chache.
Kwa kutambua umuhimu wa huduma bora za Afya kwa watanzania, Rais Samia ametumia takribani miezi 36 tu kwa uongozi wake kuongeza upatikanaji wa CT Scan kutoka 13 hadi 45, hivyo kuwezesha huduma za kibingwa katika Mikoa mingi na hii imefanya baadhi ya Hospitali zinazopakana na nchi jirani kuruhusu utalii tiba ili majirani waje kunufaika pia.
Ni katika kipindi hiki pia, ujenzi mpya na umaliziaji wa vituo vya Afya umefanya ongezeko la vituo vya afya kuongezeka kutoka 8549 hadi 9610. Kwa wataalam wa hesabu wanaweza kusema huu ni wastani wa kujenga karibu vituo 30 kwa mwezi (vipya au umaliziaji) tangu Rais alipoingia madarakani. Sanjari na hii pia ameongeza vituo vya ICU kutoka 258 hadi 1300 ndani ya muda huo huo.
Maboresho haya ndio yanayofanya takwimu kuonyesha kuwa takribani 80% ya Watanzania wanaweza kupata huduma za afya ndani ya KM 5, hii ni rekodi kubwa. Ama kwa hakika huyu ndiye Rais Samia Suluhu. Ikiwa Afrika ina viongozi bora, basi hakuna shaka kuwa nyota inayong'aa zaidi inatokea kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, ikiakisi fukwe nzuri zenye mchanga mweupe wa Zanzibar.