Rais Samia ameamua kuwatolea uvivu Jeshi la Polisi na kuyaanika hadharani maovu yao!

Kweli Rais amewachoka Polisi na akaeleza wazi kuwa safari ijayo atakitumia kile cheo chale kingine, cha u-amiri jeshi mkuu, kutokana na vitendo vyao vya kutotenda Haki!
Je amewakomboa kutoka mikononi mwa CCM? Kwamba wawalinde raia na mali zao bila ubaguzi, wawatumikie wananchi wote bila ubaguzi, watoe haki na usawa kwa wote bila ubaguzi.
 
Anasema wazi asije akalalamikiwa akianza kuchukua hatua.
Hakuna kitu kama hicho, kama ni kusema ameshasema sana, ukiwa kiongozi maneno kidogo ila vitendo sana, Hapo huwa ndio nachoka unakuta kamanda mnayemtegemea kuchukua hatua na yeye anakuwa sehemu ya kulalamika!!
 
Hizi ndizo issue aanze kuzishugjulikia na siyo kuonhelee nyomi kujaa kwenye mikutano yake
 
Soma tena,ilitakiwa awaambie wakubwa wa hao watu,au alipokua alikua na watu wa rank moja?
 
Sasa ndiyo wa kuwaamini kweli watu wa aina hiyo?

Polisi ni kioo cha jamii, kwa hiyo ni lazima wafanye Kazi yao kwa Weledi mkubwa
Kiukweli ingekuwa ni amri yangu police ingefumuliwa na ajira zianze upya kabisa na kwa kuwaacha wale wenye maadili wachache na kuajiri wengine.
 
Kuyaanika NI jambo la kawaida kwani sote tunajua ila je hatua gani za kuchukua angesem hata alivunje jeshi kwa muda Kisha vituoni wakae wanajeshi ingekuwa safi
Sijawahi liamini Jeshi la Polisi. Iwe Kifo au Ajali kwa Raia kwao Fedha kwanza katika taratibu zozote zitakazowahusu.
 
Kuyaanika NI jambo la kawaida kwani sote tunajua ila je hatua gani za kuchukua angesem hata alivunje jeshi kwa muda Kisha vituoni wakae wanajeshi ingekuwa safi
Hitimisho baada ya kufanya ivyo iwe ni nini katika kuleta jeshi jipya la polisi
 
I am not convinced kama Yuko serious na hii, huwezi kuwa serious huku unam-promote KINGAI kuwa DCI
 
Akiishia kuongea tu na hakuna kitakachobadilika ni kazi bure, watu wapo huko wamekubuhu kwa kutokutenda haki
 
Kwa madudu wanayofanya maafisa wa polisi itoshe kusema wana bahati sana.
 
Na yeye analalamika? Hajui chakufanya? Na hili pia muende mkalitizame
 
Anawaanika wakati ndio hao hao baadae watamsaidia kuingiza kura zilizopigwa tayari kwenye mabegi?
 
Wale ni walarushwa tangia miongo na miongo tangu Nyerere amalize utawala wake. Solution ni kukagua mmoja bada mwingine, watakao baki tutakuwa na jeshi imara.
 
Rais Samia Suluhu anazingatia haki za binadamu na hataki viongozi wazembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…