Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke, Makamu wa Rais wa kwanza kurithi Urais

Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke, Makamu wa Rais wa kwanza kurithi Urais

Tasnia ya habari Tanzania ni kama Gaza ilivyokaliwa na Israeli.

Israeli wana uwezo wa kuzima maji, umeme na internet.

Hivyo ikiwa vyombo vya habari vyote viko chini ya uangalizi wa wizara ya habari, TCRA na MAELEZO, basi hapo hatuna vyombo huru vya habari.

Pia waandishi wengi wa habari wa sasa wameweka uandishi wa habari na miiko yake, kanuni na miongozo kapuni na wamebaki kuwa chawa na wapokea bahasha za khaki yaitwa “chequebook journalism”.
Vp kuhusu kina Jenerali Ulimwengu au Kwa mbali Saed Kubenea??
 
Utawala wa jiwe ulitupa somo juu ya ubovu wa katiba yetu. Hivyo ilibidi tuibadili baada ya kupewa hiyo golden chance. Lkn tunaleta mbwembwe.
Mnataka muibadili kwamba yote imeoza? Be specific mkuu! Kipi hasa ni kikwazo cha maendeleo kwa Watanzania ndani ya katiba?
 
Vp kuhusu kina Jenerali Ulimwengu au Kwa mbali Saed Kubenea??
Kwa sasa Mzee Jenerali Ulimwengu ndie mwandishi bora kabisa kuwahi kutokea na ni ile timu yake ya akina Johnson Mbwambo, Ayubu Rioba na wengine walokuwa wakiandika kwenye gazeti lao la RAI (original).

Waandishi wengi wa zamani wamepotea na tasnia ya habari ilo mahiri imepotea.

Pascal Mayalla nae ni mwandishi habari mwenye kipaji chake na nilimuona tangia aanze kuingia Chuo cha Uandishi kusomea tasnia hii maana kwa maana tayari shahada ya sheria alikuwa nayo.

Wakistaafu rasmi hawa basi Tanzania itakuwa umepoteza hili kundi bora la waandishi ingawa wengi wao walikuwa walitumikia vyombo vya serikali.
 
Mnataka muibadili kwamba yote imeoza? Be specific mkuu! Kipi hasa ni kikwazo cha maendeleo kwa Watanzania ndani ya katiba?
Kikwazo ni kikubwa ni rais kuwa juu ya katiba na kumfanya awe na uwezo wa kuikamata mihimili yote 3 na hivyo kutowajibishwa alikosea.

Huku kunasababsha na marafiki/wateule wake wote kuwa salama wakivunja sheria za nchi ama hata wakila rushwa. Mteule/rafiki atawajibishwa tu endapo rais atakwazika na kutaka awajibishwe. Mfano Sabaya, Nalaila Kiula (enzi za Mkapa), profesa Costa mahalu (,enzi za Kikwete), Harbinder Seth na Rugemalira (walikingiwa kifua na Kikwete enzi zake lkn Magufuli akaja kuwasulubu, kaingia Samia kawatoa).

Asipotaka hakuna mtu ama chombo kitakachomgusa mteule wa rais hata kama ameua ama amefuja mabilioni Mfano Makonda na wale wote waliotajwa na ripoti ya CAG.

Kwahiyo nchi inaongozwa kwa matakwa na hulka ya rais aliyepo madarakani. Kosoro kubwa Sana hii.
 
Mimi huko kwingine koote, siko. Isipokuwa niko hapa na nataka tujadiliane based on these grounds.

1. Kwanza, hicho ulichokisema hapo sio fact bali ni maoni (opinion) yako tu. Hii ni kwa sababu, unachokiita kuwa ni "fact" actually ni kauli tu ya kujipa moyo na kutoa tiba ya hofu ya muda mfupi ya walio madarakani kufurushwa kuachia hayo madaraka yaliyokwisha kuwashinda..

2. TANU ya kina Julius K. Nyerere ilipokuwa inapigania uhuru wa Tanganyika, actually mazingira yalikuwa magumu kweli. Hakuna mtu aliyeweza kuwaamini kina Nyerere kirahisi kuwa inawezekana siku moja utawala wa wazawa kuu - replace utawala wa kikoloni chini ya Mwingereza..

Watu kama wewe na kauli kama za, "...hakuna watu mbadala kum - replace mkoloni mwingereza" walikuwepo na leo wapo ukiwemo wewe unayesema na kuamini kuwa "...hakuna wa kui - replace CCM" ..

Lakini by then, out of nowhere, Mwingereza alifungasha virago na kuiacha huru Tanganyika..!

##Na actually kwa akili na ufahamu wa upeo wenu mko sahihi kabisa kufikiri hivyo kuwa "haya mambo hayawezekani, hakuna mbadala" maana ndivyo mnavyoona...

Yaani mnaiona CCM kama Goliath mwenye silaha zote na kina CHADEMA na kina Boniface Mwabukusi mnawaona kama Daudi mchunga kondoo wa porini anayeingia kwenye vita na Goliath akiwa na manati (kombeo) tu..

3. Mimi naamini kuwa, anguko la utawala wa CCM litakuja very unnoticed na watu watabaki na mdomo wazi wakijiuliza, hii kitu imekuaje..!!!

Mr Pascal Mayalla hii sasa ndiyo fact kwa sababu iko supported na;

√ Ukweli kuwa viumbe huzaliwa, kukua, kuzeeka na kisha hufa. CCM actual kimeshapita steps hizi zote. Kilishakufa kitambo. Kilichopo ni kivuli tu lakini nacho kinatoweka kwa sababu jua limekaribia kuzama..!

√ Historia ya vyama vya Ukombozi inakishitaki. Mfano hakuna aliyedhaniaga kuwa KANU ya Kenya ingeweza kupotea kirahisi vile..

Je, sasa yaweza kuwa kipindi hiki ni zamu ya CCM? Bila shaka maana ishara zote zinaonesha hivyo...
Uchambuzi mujarab!
 
Kwa upande wa urais, wapinzani wanashiriki kujifurahisha tuu, ila ubunge, udiwani, na serikali za mitaa ndio stahiki zao.

Kuelekea uchaguzi wa 2020 niliuliza, Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa uchaguzi wa 2025 tumeisha shauri Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli iachane na 2025 lengo liwe 2030

The real chances ni kuanzia 2030!, Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!

P
Mkuu kwa wanaoelewa na ukweli unaouficha ni kwamba, the real chance ni 2025! Shida unatumika kama hutumiki!
 
Back
Top Bottom