Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke, Makamu wa Rais wa kwanza kurithi Urais

Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke, Makamu wa Rais wa kwanza kurithi Urais

Mkuu Gulwa , it's true, no research no right to speak. Mimi kwa upande wangu I did my homework well, siku zote nawaambia watu humu kuwa Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
hawaamini!.

Mtu ukiishamjua ni chizi, usimshauri chochote bali jitahidi tuu kumsitiri.
P
Huenda hujui maana na matumizi ya neno milele, wahenga walishasema kubwa kila chenye mwanzo kina mwisho. Mungu pekee hana mwanzo na hatakuwa na mwisho
 
Hayo mawili ya mwanzo yako wazi, ila hili tatu linahitaji watu wenye akili tulivu kulikubali na kulielewa. Hatakuwa rais wa kwaza kushindwa uchaguzi kwani wapo walioshindwa na kuendelea kubaki madarakani. 2015, 2020 ni mifano hai, ila kwa sasa hali imebadilika, atalazimika kukubali na kuyapokea matokeo halali.

Tuombe uzima
Nani wa kushindana nae?

Mdudu au mwambulukuku?
 
Acheni kumwita 'mama' mnaendeleza hisia za mfumo dume, inapotokea dosari kwake inavishwa kundi la wanawake badala ya kumtreat kama Rais wa nchi.

Mtuambie, ninyi ndio mnamsanifu, kwa kumwita 'mama' ili kumjengea mtazamo kwamba ni 'dhaifu'.

Nani asiefahamu kwamba Afrika ukisema 'mama' unamuhusianisha na udhaifu, ulegevu na kushindwa kujisimamia mpaka awepo baba?
Mama ni neno la heshima usikasirike wewe kwenu hamna wakubwa?
 
Hayo mawili ya mwanzo yako wazi, ila hili tatu linahitaji watu wenye akili tulivu kulikubali na kulielewa. Hatakuwa rais wa kwaza kushindwa uchaguzi kwani wapo walioshindwa na kuendelea kubaki madarakani. 2015, 2020 ni mifano hai, ila kwa sasa hali imebadilika, atalazimika kukubali na kuyapokea matokeo halali.

Tuombe uzima
Utamshinda kwa tume ambayo kaiteua yeye mwenyewe?
 
Mkuu Gulwa , humu JF, rukhsa kujifurahisha!, kama unaamini 2015 na 2020, CCM ilishindwa ikapiga bao la mkono!, endelea kuamini hivyo!, hicho chama cha kuishinda CCM kwenye sanduku la kura, kwa Tanzania bara, bado sana!.

Sababu inayoifanya CCM isishindwe ni kwasababu CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola! hivyo CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?
P
Kama tume itakuwa huru CCM itaondoka mchana kweupe
 
Kwa JPM ilitokea kama golden chance tu lkn hatukuitumia vizuri. Na hii golden chance huwa haiji mara 2.
Si nasikia walitaka kuitumia former mkuu wa mabaka akatibua!!?

Watasahihisha makosa coz walisha plan tangu zamani kuingiza ambae hajawahi gombea!

Tuwasubiri tuone!

Yule jamaa si alisema operation ipo on!!?

We hujaona dalili kwani!!?

Malkia ESTA ni kama anachechemea hivi upande shoto au ninini hiyo!!?

"Mpango ndio mpango mzima"wawangaji nao wameshaanza kuwanga na nyuzi zao humu!!
 
Mama ni neno la heshima usikasirike wewe kwenu hamna wakubwa?
Wapo, ijapokuwa kwenye vyombo vya dola hakuna nafasi inayoitwa 'mama'.

Wacha akina Abdul na Mchengerwa wamwite kwa utambulisho huo nyumbani huko!

Katika muktadha huu, apewe heshima yake Mhe. Rais

Sina shida na wewe kumuita 'mama' ispokuwa muktadha huu sio sahihi mkuu!

Mnamwondolea hadhi yake.
 
Mimi huko kwingine koote, siko. Isipokuwa niko hapa na nataka tujadiliane based on these grounds.

1. Kwanza, hicho ulichokisema hapo sio fact bali ni maoni (opinion) yako tu. Hii ni kwa sababu, unachokiita kuwa ni "fact" actually ni kauli tu ya kujipa moyo na kutoa tiba ya hofu ya muda mfupi ya walio madarakani kufurushwa kuachia hayo madaraka yaliyokwisha kuwashinda..

2. TANU ya kina Julius K. Nyerere ilipokuwa inapigania uhuru wa Tanganyika, actually mazingira yalikuwa magumu kweli. Hakuna mtu aliyeweza kuwaamini kina Nyerere kirahisi kuwa inawezekana siku moja utawala wa wazawa kuu - replace utawala wa kikoloni chini ya Mwingereza..

Watu kama wewe na kauli kama za, "...hakuna watu mbadala kum - replace mkoloni mwingereza" walikuwepo na leo wapo ukiwemo wewe unayesema na kuamini kuwa "...hakuna wa kui - replace CCM" ..

Lakini by then, out of nowhere, Mwingereza alifungasha virago na kuiacha huru Tanganyika..!

##Na actually kwa akili na ufahamu wa upeo wenu mko sahihi kabisa kufikiri hivyo kuwa "haya mambo hayawezekani, hakuna mbadala" maana ndivyo mnavyoona...

Yaani mnaiona CCM kama Goliath mwenye silaha zote na kina CHADEMA na kina Boniface Mwabukusi mnawaona kama Daudi mchunga kondoo wa porini anayeingia kwenye vita na Goliath akiwa na manati (kombeo) tu..

3. Mimi naamini kuwa, anguko la utawala wa CCM litakuja very unnoticed na watu watabaki na mdomo wazi wakijiuliza, hii kitu imekuaje..!!!

Mr Pascal Mayalla hii sasa ndiyo fact kwa sababu iko supported na;

√ Ukweli kuwa viumbe huzaliwa, kukua, kuzeeka na kisha hufa. CCM actual kimeshapita steps hizi zote. Kilishakufa kitambo. Kilichopo ni kivuli tu lakini nacho kinatoweka kwa sababu jua limekaribia kuzama..!

√ Historia ya vyama vya Ukombozi inakishitaki. Mfano hakuna aliyedhaniaga kuwa KANU ya Kenya ingeweza kupotea kirahisi vile..

Je, sasa yaweza kuwa kipindi hiki ni zamu ya CCM? Bila shaka maana ishara zote zinaonesha hivyo...
Well said!
Well said!

Tanganyika tuna changamoto mbili kuu, changamoto ya kwanza ni CCM na changamoto ya pili ni huu Muungano.
 
Mods tena katika moja na mbili.
Kama vipi moderators ndiyo wawe wanaanzisha mada.
Mada ililetwa nzuri mnajikuta wajuaji wa kuedit.
 
Hayo mawili ya mwanzo yako wazi, ila hili tatu linahitaji watu wenye akili tulivu kulikubali na kulielewa. Hatakuwa rais wa kwaza kushindwa uchaguzi kwani wapo walioshindwa na kuendelea kubaki madarakani. 2015, 2020 ni mifano hai, ila kwa sasa hali imebadilika, atalazimika kukubali na kuyapokea matokeo halali.

Tuombe uzima
Mods hamjanitendea haki, mmehariri na kupotosha kichwa cha uzi wangu bila kunipa sababu.
 
Mods tena katika moja na mbili.
Kama vipi moderators ndiyo wawe wanaanzisha mada.
Mada ililetwa nzuri mnajikuta wajuaji wa kuedit.
Hawatendi haki tena, hii siyo JF tuliyoizoea, kama imekuwa compromised vile
 
Back
Top Bottom