Mimi huko kwingine koote, siko. Isipokuwa niko hapa na nataka tujadiliane based on these grounds.
1. Kwanza, hicho ulichokisema hapo
sio fact bali ni
maoni (opinion) yako tu. Hii ni kwa sababu, unachokiita kuwa ni "fact" actually ni kauli tu ya kujipa moyo na kutoa tiba ya hofu ya muda mfupi ya walio madarakani kufurushwa kuachia hayo madaraka yaliyokwisha kuwashinda..
2. TANU ya kina Julius K. Nyerere ilipokuwa inapigania uhuru wa Tanganyika, actually mazingira yalikuwa magumu kweli. Hakuna mtu aliyeweza kuwaamini kina Nyerere kirahisi kuwa inawezekana siku moja utawala wa wazawa kuu - replace utawala wa kikoloni chini ya Mwingereza..
Watu kama wewe na kauli kama za, "...
hakuna watu mbadala kum - replace mkoloni mwingereza" walikuwepo na leo wapo ukiwemo wewe unayesema na kuamini kuwa "...
hakuna wa kui - replace CCM" ..
Lakini by then, out of nowhere, Mwingereza alifungasha virago na kuiacha huru Tanganyika..!
##Na actually kwa akili na ufahamu wa upeo wenu mko sahihi kabisa kufikiri hivyo kuwa "
haya mambo hayawezekani, hakuna mbadala" maana ndivyo mnavyoona...
Yaani mnaiona CCM kama Goliath mwenye silaha zote na kina CHADEMA na kina Boniface Mwabukusi mnawaona kama Daudi mchunga kondoo wa porini anayeingia kwenye vita na Goliath akiwa na manati (kombeo) tu..
3. Mimi naamini kuwa, anguko la utawala wa CCM litakuja very unnoticed na watu watabaki na mdomo wazi wakijiuliza, hii kitu imekuaje..!!!
Mr
Pascal Mayalla hii sasa ndiyo fact kwa sababu iko supported na;
√ Ukweli kuwa viumbe huzaliwa, kukua, kuzeeka na kisha hufa. CCM actual kimeshapita steps hizi zote. Kilishakufa kitambo. Kilichopo ni kivuli tu lakini nacho kinatoweka kwa sababu jua limekaribia kuzama..!
√ Historia ya vyama vya Ukombozi inakishitaki. Mfano hakuna aliyedhaniaga kuwa KANU ya Kenya ingeweza kupotea kirahisi vile..
Je, sasa yaweza kuwa kipindi hiki ni zamu ya CCM? Bila shaka maana ishara zote zinaonesha hivyo...