Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza mwanamke, Makamu wa Rais wa kwanza kurithi Urais

Vp kuhusu kina Jenerali Ulimwengu au Kwa mbali Saed Kubenea??
 
Utawala wa jiwe ulitupa somo juu ya ubovu wa katiba yetu. Hivyo ilibidi tuibadili baada ya kupewa hiyo golden chance. Lkn tunaleta mbwembwe.
Mnataka muibadili kwamba yote imeoza? Be specific mkuu! Kipi hasa ni kikwazo cha maendeleo kwa Watanzania ndani ya katiba?
 
Vp kuhusu kina Jenerali Ulimwengu au Kwa mbali Saed Kubenea??
Kwa sasa Mzee Jenerali Ulimwengu ndie mwandishi bora kabisa kuwahi kutokea na ni ile timu yake ya akina Johnson Mbwambo, Ayubu Rioba na wengine walokuwa wakiandika kwenye gazeti lao la RAI (original).

Waandishi wengi wa zamani wamepotea na tasnia ya habari ilo mahiri imepotea.

Pascal Mayalla nae ni mwandishi habari mwenye kipaji chake na nilimuona tangia aanze kuingia Chuo cha Uandishi kusomea tasnia hii maana kwa maana tayari shahada ya sheria alikuwa nayo.

Wakistaafu rasmi hawa basi Tanzania itakuwa umepoteza hili kundi bora la waandishi ingawa wengi wao walikuwa walitumikia vyombo vya serikali.
 
Mnataka muibadili kwamba yote imeoza? Be specific mkuu! Kipi hasa ni kikwazo cha maendeleo kwa Watanzania ndani ya katiba?
Kikwazo ni kikubwa ni rais kuwa juu ya katiba na kumfanya awe na uwezo wa kuikamata mihimili yote 3 na hivyo kutowajibishwa alikosea.

Huku kunasababsha na marafiki/wateule wake wote kuwa salama wakivunja sheria za nchi ama hata wakila rushwa. Mteule/rafiki atawajibishwa tu endapo rais atakwazika na kutaka awajibishwe. Mfano Sabaya, Nalaila Kiula (enzi za Mkapa), profesa Costa mahalu (,enzi za Kikwete), Harbinder Seth na Rugemalira (walikingiwa kifua na Kikwete enzi zake lkn Magufuli akaja kuwasulubu, kaingia Samia kawatoa).

Asipotaka hakuna mtu ama chombo kitakachomgusa mteule wa rais hata kama ameua ama amefuja mabilioni Mfano Makonda na wale wote waliotajwa na ripoti ya CAG.

Kwahiyo nchi inaongozwa kwa matakwa na hulka ya rais aliyepo madarakani. Kosoro kubwa Sana hii.
 
Uchambuzi mujarab!
 
Mkuu kwa wanaoelewa na ukweli unaouficha ni kwamba, the real chance ni 2025! Shida unatumika kama hutumiki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…