Rais Samia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya

Rais Samia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhes. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.

Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.

WhatsApp Image 2023-05-06 at 21.59.17.jpeg
 
Msisahau kuhusisha wananchi katiba sio ya wanasiasa.

Haya mambo ya kila kitu kuhodhiwa na wanasiasa sio sawa.

Tunahitaji katiba ya warioba iboreshwe sio kutumia pesa za walipa kodi kuhudumia matumbo ya wanasiasa tena kwa mara ya pili!!!.

Katiba tunahitaji lakini sio lazima tuingie tena hasara ya mabilioni wakati tulishapata hasara uko nyuma ebu tuendelee mchakato sio kuanza upya.!
 
Kama kuna mmoja anayetagemea kuwepo kwenye kikao kijacho tafadhali sana tena sana, wasilisha ombi la wananchi kuwa...
"TUNATAKA RASIMU YA KATIBA YA JAJI WARIOBA" hayo mengine itakuwa ni sawa na kujilisha upepo.
 
Timing nzuri sana Wallah

Remote controller anatisha aisee

Ccm kwa kushirikiana na vyama Rafiki wanaenda kutuletea Katiba mpya itayoridhiwa na wanasiasa wote wa vyama vikubwa ukiacha vikundi vichache vichache vya wahafidhina

hasa 'Asasi za kiraia' zote zipo mguu sawa kubariki Katiba mpya

I'm proud to be Tanzanian
 
Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa
na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Habari hii akiiona ama kuisikia Tulia Akson atavaa mpk pampasi kuzuia kubwa isichafue nguo maana salama na hatima ya uspika wake ulitegemea sana ubovu wa katiba iliyopo.
 
Msisahau kuhusisha wananchi katiba sio ya wanasiasa.

Haya mambo ya kila kitu kuhodhiwa na wanasiasa sio sawa...
Kabisa ndugu yangu, hakuna haja ya kupoteza tena pesa ya watanzania, chukueni katiba ya Warioba na iboreshwe na wawakilishi wa wananchi tu kulingana na wakati huu, iletwe Kwa wananchi, waijadili na kuipitisha katiba sio ya vyama tu ni wananchi wote.

Kwanza huyo Jaji Mutungi hivi naye bado yupo hajabadilishwa tu, manake ndo walewale wanaokwaza katiba mpya yenye kuleta tija Tz....kaazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom