Rais Samia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya

Rais Samia amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya

Katiba mpya ni sawa na kutanguliza mkokoteni mbele ya farasi.

Bila kupanua uelewa wa wananchi katika mambo yao ya msingi katiba mpya haitawanufaisha kwa lolote lile zaidi sana ni kwa manufaa ya watu wale wale wanaonufaika nayo kwa Sasa.
 
"kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa" Yenye lengo..." lakutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini"
Kwa hayo,;Kuh:Baraza la Vyama la Siasa, Upande mmoja ni kutokana na vuta nikuvute ya yanyojiri nyuma ya pazia ya kinachoitwa "maridhiano"(mashauri) au kwa lugha nyepesi, mikutano ya siri kati ya CHADEMA na CCM na Upande wapili Ni danadana za, Kwanza, Mwenyekiti wa CCM na, Pili, RaisiAmiriJeshiMkuu Dakta Mama. Yaani ndie atakayechukua Credit hapa kama nipe nikupe. [I am assuming A give and take scenario.] CCM au Raisi au Mwenyekiti-take your pick-anatoa maelekezo! pili CHADEMA wanasita-wanakoma kuwa vinara, manake bila hivyo mchakato mzima unaweza kususiwa na Vyama Vingine....CUF, ACT, Umoja?? kwa kutokuhusishwa, kwani tuliona hata pale Bwana Tundu alivyoondoka ghafla kwa kile ninachokiona kama[alijisikia kama mtazamaji]kwani hakuhusishwa na wala hakuwa na usemi kwenye mikutano ya siri(maridhiano) au kwa Lugha ya CHADEMA "Kivutio" tu n.k Ila basi.
Nevertheless, naona Inawapunguzia umuhimu na uhuru Kikosi kazi wa kutoa Taarifa(labda kanuni haziruhusu) vilevile inampunguzia umuhimu na uhuru wa Msajili wa Vyama kufanya Vivyohivyo(kutoa maelekezo ya kuitisha kikao hicho cha Baraza la Vyama vy Siasa.?? Ndio kusema, CCM takes CHADEMA giveth

Sasa hayo ni ya Wakuu. Sisi Wananchi Je?
Ndio tunapewa mifupa sasa?
Halafu..."wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya."

Kwa mtazamo wangu wa siku nyingi; huo mda haupo! kati ya sasa na Uchaguzi Ujao. Isitoshe, Umekuwa mtazamo wa wengi sasa. Yaani inakubalika.

Wakati huo huo....
Mpira upo kwenye "tathmini" ya utekelezaji, ikiwa ina maana Mapendekezo yapo, Je, Vyama Vya Siasa vinakubalina na Mapendekezo ya Kikosi kazi yaliyojumuishwa na mashauri ya CCM CHADEMA? Sasa Vyama vikubaliane, mapendekezo yatekelezwe na kukubaliana, Bunge maalum liitwe(emergency?) muswada wa marekebisho fulani yafanyike, huu wote ni muda(CAG RPTkalaghabao) Uchaguzi ufanyike angalabu wa mitaa halafu ndio Mchakato uanze? Aisee-nakubalina na wengi hapa ni kuchezea muda.

Siwadharau CHADEMA kwa hili, at the same time not underestimating CCM chair lakini watujuze kwani as Raisi alitoa ahadi Kikosi kazi kije Itueleweshe Wananchi kuhusu yanayojiri, na CHADEMA waseme at what cost? wanataka kufunika uchafuzi wa mazingira yaliyopita kwa kukubali CREDIT apewe CCM
 
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhes. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.

Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.

View attachment 2612539
Kumbe katiba ni ya wanasiasa! Siyo ya wananchi?
 
Katiba mpya ni sawa na kutanguliza mkokoteni mbele ya farasi.

Bila kupanua uelewa wa wananchi katika mambo yao ya msingi katiba mpya haitawanufaisha kwa lolote lile zaidi sana ni kwa manufaa ya watu wale wale wanaonufaika nayo kwa Sasa.
Sio kweli, mchakato ukianza mwamko utakuwa mkubwa kweli kweli Watanzania sio wajinga ki vile kama unavyowafikiria.
 
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhes. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.

Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.

View attachment 2612539
danganya toto
 
Msisahau kuhusisha wananchi katiba sio ya wanasiasa.

Haya mambo ya kila kitu kuhodhiwa na wanasiasa sio sawa.

Tunahitaji katiba ya warioba iboreshwe sio kutumia pesa za walipa kodi kuhudumia matumbo ya wanasiasa tena kwa mara ya pili!!!.

Katiba tunahitaji lakini sio lazima tuandike tena hasara ya mabilioni wakati tulishapata hasara uko nyuma ebu tuendelee mchakato sio kuanza upya.!
Maoni ya Wananchi anayo Warioba loooongi!
 
Hii sio ya wanasiasa pekee ni ya watanganyika na wazanzibari sasa swala linalo husu nchi yao, washirikishwe, wabunge sio wawakilishi wa wananchi wote wapo kwaajili ya maslahi ya vyama vyao. Sisi raia tusio fungamana na chama chochote tuna haki ya kutoa maoni ya katiba mpya na muungano.
 
Vile "Mama" anawasisitizia CCM kuwa katiba mpya ni lazima na ni sasa👇😁😁😁
 
Back
Top Bottom