Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
π π πKufufua katiba mpya ni kuua Legacy ya Magufuli. Sisi wafuasi wake tunashangazwa sana na kutomuenzi hayati
Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani. Kwa taarifa yako mchakato wa katiba mpya haukusimama bali uliendelea hadi kupatikana katiba pendekezwa. Ikawa imebaki hatua ya kura ya maoni, ambayo ilisimama kupisha uchaguzi mkuu wa 2015, kisha rais ajaye amalize kura ya maoni.Wapinzan ndiyo walioharibu mchakato sasa hivi tungekuwa na Katiba mpya walisusa wakatoka nje
Ameeni ameeniSawa, tunaombea mambo mema yafanyike, kwa ajili ya nchi yetu.
Hakuna katiba ya Warioba. Ile ilikuwa rasimu tu.Msisahau kuhusisha wananchi katiba sio ya wanasiasa.
Haya mambo ya kila kitu kuhodhiwa na wanasiasa sio sawa.
Tunahitaji katiba ya warioba iboreshwe sio kutumia pesa za walipa kodi kuhudumia matumbo ya wanasiasa tena kwa mara ya pili!!!.
Katiba tunahitaji lakini sio lazima tungie tena hasara ya mabilioni wakati tulishapata hasara uko nyuma ebu tuendelee mchakato sio kuanza upya.!
Sasa iko wazi Katiba mpya inakuja.TANZANIA oyee!!
Habari kama hizi Tukia Ackson anaweza kutoroka nchi kwa kihoro..... Huyu ndio Mama wa [emoji1241][emoji1241]
Kiongozi wa mfano ambaye dunia ilikuwa inamsubiri kwa hamu kuu.
Halafu kuna mtu anataka kumfananisha Dr Samia Suluhu Hassani na matakataka mengine yale yaliyopita kuleeee
Sent from my SOV37 using JamiiForums mobile app
Nani kama mama!Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhes. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.
Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.
Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.
Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.
View attachment 2612539
Kwan watu wanakula katiba jamani .mbona matatizo mengi ya watanzai you yale ya msingi sana.... Huyu ndio Mama wa [emoji1241][emoji1241]
Kiongozi wa mfano ambaye dunia ilikuwa inamsubiri kwa hamu kuu.
Halafu kuna mtu anataka kumfananisha Dr Samia Suluhu Hassani na matakataka mengine yale yaliyopita kuleeee
Sent from my SOV37 using JamiiForums mobile app
Ulitaka afanye haraka nani!? Kwani mama ameingia lini mjengoni!? Kw nini tusishukuru hata kwa mawazo yake tu ya kufikiria kurejesha mchakato wa katiba mpya kwa kipindi hiki kifupi tu cha uongozi wake!?Huu muda uliobaki kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na Uchaguzi Mkuu wa 2025, napata mashaka kama utatosha kwetu kuipata hiyo Katiba Mpya..
Sijui ni kitu gani kinachochelewesha hili zoezi, linaonekana kwenda taratibu bila sababu za maana licha ya kuwa na hatua nyingi na ngumu mbele ya safari, mfano mpaka leo tunaimbishwa tu Katiba Mpya, lakini wengi bado hatujajua kama itakuwa ni ile Rasimu ya Warioba, au Katiba Pendekezwa ya CCM.
Naamini huu ucheleweshwaji wa makusudi unaoendelea yote ni mipango inafanyika kwa manufaa ya mtawala, ajabu wengi mnaonekana kushangilia hatua hizi zinazokwenda taratibu zikisubiri mpaka "michakato" isiyojulikana itakwisha lini ikamilike!.
Hakuna hoja ambayo haina mashiko kwasababu hoja zote zinajadilika.Katiba sio ya wapinzani ni katiba ya nchi.Endelezeni hoja zenu zisizo na mashiko halafu mgomee mchakato wa katiba mpya Kama mlivyofanya kipindi kile
Inahitaji maboresho kwasababu mambo mengi yalishajadiliwa.Ile ishapitwa na wakati na haitufai kwa wakati huu.
Yale maoni yana miaka 9 kuelekea 10
Mi naona sehemu ambayo italetea taifa shida ni swala la 50/50 kuna vihiyo wengi watapita na itakuw ahasara kwa taifaInahitaji maboresho kwasababu mambo mengi yalishajadiliwa.
Wapinzani waliharibu vip wakati wao walikua wajumbe tu?.Mwenye mamlaka yakuanzisha mchakato ndiye aliyeharibu mchakato.Aliyeanzisha mchakato angekua na nia yakuuendeleza mchakato katiba mpya ingepatikana kwasababu katiba mpya ni ya nchi sio wapinzani au wanasiasa.Wanaotakiwa kuulizwa ni Ccm na serikali yake,kwasababu wao ni wa kwanza wanaotakiwa wanaipatia nchi katiba bora.Wapinzan ndiyo walioharibu mchakato sasa hivi tungekuwa na Katiba mpya walisusa wakatoka nje
Takataka ya chooni inatupotezea muda wetu bure[emoji90][emoji90][emoji90]Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhes. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi, kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa.
Lengo ni kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilichokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.
Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali na hasa ushirikishwaji wa wananchi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.
Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya, masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi; zikiwemo Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na watendaji wa taasisi mbalimbali.
View attachment 2612539
Sasa naanza kumuamini Samia.Sasa iko wazi Katiba mpya inakuja.
Maridhiano hoyeee!