Rais Samia amenikosha sana kwa kutangaza azma yake, watoto wa mjini wanaita kupindua meza kibabe

James Martin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2016
Posts
1,206
Reaction score
1,509
Nimefurahishwa sana na kitendo cha Rais wetu mpendwa cha kutangaza bayana azma yake ya kukalia kiti cha urais kwa muhula mwingine.

Binafsi nafikiri amefanya kitu cha msingi kwa kuwakatisha tamaa wale wenye uchu wa madaraka ili wapate kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Bila shaka sasa watu wataanza kufanya kazi za kujenga nchi na kuachana na mawazo ya kugombea urais 2025.
 
Nimefurahishwa sana na kitendo cha mama yetu mpendwa cha kutangaza bayana azma yake ya kukalia kiti cha urais kwa muhula mwingine. Bibafsi nafikiri amefanya kitu cha msingi kwa kuwakatisha tamaa wale wenye uchu wa madaraka ili wapate kuendelea na shughuli zao za kawaida. Bilashaka sasa watu wataanza kufanya kazi za kujenga nchi na kuachana na mawazo ya kugombea urais 2025.
Kiukweli amefanya la maana Sana, sukuma gang kwisha habari yaoo
 
Tofautisha sentensi zako " Raisi wetu Magufuli(RIP)" na "mama yako",hata hivyo Magufuli(JPM) alichaguliwa na wananchi wote(80%plus).
Hata Mama yetu mpendwa alichaguliwa na wananchi acha Nongwa
 
Sema amekula matapishi yake kibabe.
 
Nimefurahishwa sana na kitendo cha mama yetu mpendwa cha kutangaza bayana azma yake ya kukalia kiti cha urais kwa muhula mwingine.

Binafsi nafikiri amefanya kitu cha msingi kwa kuwakatisha tamaa wale wenye uchu wa madaraka ili wapate kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Bilashaka sasa watu wataanza kufanya kazi za kujenga nchi na kuachana na mawazo ya kugombea urais 2025.
Bro nisamehe lakini kuna vitu vimeashiria kuwa ubongo wako unahitaji msaada wa chakula chake.
1. Kila Mtanzania ana haki kuutaka urais hii ni HAKI kuwaita wana uchu unakosea.

2. 2025 iko wazi kwa wana ccm na upinzani...mama Hangaya hana ile amalizie 10 ya ccm kwasababu anamalizia awamu ya 5, na yeye amekiri ni rais wa katiba, hivyo atahitaji kupitia mchakato wa chama chake...je atashinda ccm?

Mnampa moyo lakini safari ni ngumu zaidi ya kudra iliyomdondokea
 
Leo nimemsikia Mwigulu akihojiwa BBC kuhusu fedha za Mkopo kutoka Benki ya dunia, jamaa kapoa mno, nadhani tangazo la Rais Jana limempooza.
 
Nimefurahishwa sana na kitendo cha mama yetu mpendwa cha kutangaza bayana azma yake ya kukalia kiti cha urais kwa muhula mwingine.

Binafsi nafikiri amefanya kitu cha msingi kwa kuwakatisha tamaa wale wenye uchu wa madaraka ili wapate kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Bilashaka sasa watu wataanza kufanya kazi za kujenga nchi na kuachana na mawazo ya kugombea urais 2025.
Mbona wapinzani hawaruhusiwi hata mikutano ya ndani wakati Samia yeye kashaanza kampeni?!!!
 
Nimefurahishwa sana na kitendo cha mama yetu mpendwa cha kutangaza bayana azma yake ya kukalia kiti cha urais kwa muhula mwingine.

Binafsi nafikiri amefanya kitu cha msingi kwa kuwakatisha tamaa wale wenye uchu wa madaraka ili wapate kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Bilashaka sasa watu wataanza kufanya kazi za kujenga nchi na kuachana na mawazo ya kugombea urais 2025.
Angalizo tu ni kuwa gonjwa la UVIKO 19 limekuja na tishio jipya la wimbi la nne, yaani "Mu variant". Ni vyema kuwa na matamanio ya uongozi kwa siku zijazo, lakini ni vyema pia majaliwa yakawekwa mikononi mwa Mola.
 
Hata Mama yetu mpendwa alichaguliwa na wananchi acha Nongwa
Hata mwenyewe amesema hajachaguliwa Bali amefurahia kudra za Mwenyezi Mungu zilizomuwezesha kuwa rais .
Hivyo ndio anafanya kampeni kwa wanawake wenzake wamchague mwanamke mwenzao awe rais ili wanawake wale Neema ya nchi.
Wanasiasa wa bongo ni kichefuchefu sana
 
Bro nisamehe lakini kuna vitu vimeashiria kuwa ubongo wako unahitaji msaada wa chakula chake.
1. Kila Mtanzania ana haki kuutaka urais hii ni HAKI kuwaita wana uchu unakosea.

2. 2025 iko wazi kwa wana ccm na upinzani...mama Hangaya hana ile amalizie 10 ya ccm kwasababu anamalizia awamu ya 5, na yeye amekiri ni rais wa katiba, hivyo atahitaji kupitia mchakato wa chama chake...je atashinda ccm?

Mnampa moyo lakini safari ni ngumu zaidi ya kudra iliyomdondokea
JK amemhakikishia atampigania apitishwe bila kupingwa
 
Back
Top Bottom