Rais Samia amepoteza mwelekeo mapema sana, hawezi kutoboa!

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Nimekuja na hii mada kwa makusudi mawili, moja kuwapa angalizo watanzania wenzangu na pili kujiandaa kwa mengi na makubwa yatakayofuata hapa Tanzania.

Kwa sasa sio siri tena, matazamio ya mabadiliko makubwa yenye tija kwenye uchumi na siasa hapa Tanzania chini ya utawala wa mama Samia yameyuka ghafla na kwa haraka sana. Tayari mama Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka kwenye makundi makubwa ya kijamii na kisiasa. Matumaini hayapo tena.

Wataalamu wa siasa wanasema siasa ni agenda, na mwanasiasa ukipoteza agenda inayokubeba maana yake umepoteza mwelekeo. Wakati mama Samia Suluhu anaingia madarakani, agenda nne muhimu (Haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza, Maridhiano ya kisiasa na Uchumi binafsi) zilikuwa mkononi mwake na alionekana kuwa na fikra chanya za kuzitumia vyema katika safari yake ya kisiasa, bahati mbaya sana kwa sasa karibu agenda zote zimemponyoka ghafla kutoka mikononi mwake, hana tena pa kushika. Rangi halisi ya utawala wa mama Samia tumeweza kuijua sasa, ni utawala wa ovyo ovyo, hauna kipya wala chema cha maana sana cha tofauti na utawala uliopita wa Magufuli.

Kupanda kwa nishati (mafuta ya petrol na diesel) na miamala ya simu kulikofanywa kimakusudi na serikali ya mama Samia Suluhu kumeua matumaini yote ya vyuma kuachia. Maisha ya msoto yameongezeka zaidi kwa watanzania kuliko kipindi cha Magufuli na wakati huo huo ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa umma umeporomoka. Mambo ni ovyo ovyo.

Kupigwa kumbo kwa mchakato wa katiba mpya (ambao upo kisheria) na kuzuiwa kwa shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani (ambapo kupo kikatiba) ni kosa kubwa zaidi lililofanywa na utawala wa mama Samia Suluhu. Hakuna namna ataweza kupambana kinguvu kupingana na harakati za wanasiasa wa upinzani na wanaharakati, mama huenda akapelekwa mchaka mchaka mpaka ajute.

Mama Samia kwa sasa anajaribu kuiga mbinu mbovu na mbaya za kisiasa na kiuchumi za utawala wa Magufuli wakati yeye sio Magufuli na hawezi kuwa kama Magufuli. Njia aliyoichagua mama Samia ni njia mbovu, mbaya na yenye mwisho mbaya. Poor and dead ended path, kwa lugha rahisi hawezi kutoboa.

Waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita!
 
Hakuna lolote! Mama yuko njia sahihi kwa agenda alizojiwekea.

Kawafanyia CHADEMA mengi kwa muda mchache mkaanza dharau na matusi.

Tukawaonya ya kuwa mtafanya mama akaze kamba na wahanga mtakuwa nyie!

Mama endelea kuupigia mwingi. HAKI, NIDHAMU, NA WAJIBU!

Kazi Iendelee!
 
Miluzi mingi humpoteza mbwa. Hajui amfurahishe nani matokeo yake anapotea kabisa. Hana vision yake mwenyewe, makada na mafisadi wamemzunguka na kumshauri kwa manufaa yao wenyewe kitu ambacho kimemuingiza chaka vibaya mno hata kabla ya dakika ya 10.

Alianza vizuri mno ila alipoanza kuwasikiliza ndio kaharibu na bahati mbaya anafuata tu sijui ndio hofu ya kuendesha gari kubwa
 
Nimekuja na hii mada kwa makusudi mawili, moja kuwapa angalizo watanzania wenzangu na pili kujiandaa kwa mengi na makubwa yatakayofuata hapa Tanzania.

Kwa sasa sio siri tena, matazamio ya mabadiliko makubwa yenye tija kwenye uchumi na siasa hapa Tanzania chini ya utawala wa mama Samia yameyuka ghafla na kwa haraka sana. Tayari mama Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka kwenye makundi makubwa ya kijamii na kisiasa. Matumaini hayapo tena.

Wataalamu wa siasa wanasema siasa ni agenda, na mwanasiasa ukipoteza agenda inayokubeba maana yake umepoteza mwelekeo. Wakati mama Samia Suluhu anaingia madarakani, agenda nne muhimu (Haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza, Maridhiano ya kisiasa na Uchumi binafsi) zilikuwa mkononi mwake na alionekana kuwa na fikra chanya za kuzitumia vyema katika safari yake ya kisiasa, bahati mbaya sana kwa sasa karibu agenda zote zimemponyoka ghafla kutoka mikononi mwake, hana tena pa kushika. Rangi halisi ya utawala wa mama Samia tumeweza kuijua sasa, ni utawala wa ovyo ovyo, hauna kipya wala chema cha maana sana cha tofauti na utawala uliopita wa Magufuli.

Kupanda kwa nishati (mafuta ya petrol na diesel) na miamala ya simu kulikofanywa kimakusudi na serikali ya mama Samia Suluhu kumeua matumaini yote ya vyuma kuachia. Maisha ya msoto yameongezeka zaidi kwa watanzania kuliko kipindi cha Magufuli na wakati huo huo ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa umma umeporomoka. Mambo ni ovyo ovyo.

Kupigwa kumbo kwa mchakato wa katiba mpya (ambao upo kisheria) na kuzuiwa kwa shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani (ambapo kupo kikatiba) ni kosa kubwa zaidi lililofanywa na utawala wa mama Samia Suluhu. Hakuna namna ataweza kupambana kinguvu kupingana na harakati za wanasiasa wa upinzani na wanaharakati, mama huenda akapelekwa mchaka mchaka mpaka ajute.

Mama Samia kwa sasa anajaribu kuiga mbinu mbovu na mbaya za kisiasa na kiuchumi za utawala wa Magufuli wakati yeye sio Magufuli na hawezi kuwa kama Magufuli. Njia aliyoichagua mama Samia ni njia mbovu, mbaya na yenye mwisho mbaya. Poor and dead ended path, kwa lugha rahisi hawezi kutoboa.

Waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita!
Hizo ni fikra zako na mtazamo wako South Africa wana katiba bora kabisa cha ajabu mtu aliyefanya ufisadi anatetewa na wafuasi wake katiba siyo muarubaini, Kenya pia kuja katiba mpya lakini ufisadi kama kawaida.
 
Back
Top Bottom