Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe, bila ya kujali kada zetu na kwa wakati huu haswa viongozi wa chama tawala na serikali ndiyo waonyeshe mfano katika kuchangia uchumi wa nchi wajitolee hali na mali kwani wao ndiyo wawakilishi wa wananchi na ndiyo wenye vipato vya uhakika.
Uongozi ni jukumu kubwa, na miongoni mwa majukumu hayo ni kuhakikisha hali za wanao ongozwa zina kuwa nzuri, CCM inabidi ijitathmini kwani takriban miaka 60 inaongoza nchi bado wananchi wanalalamika kuhusu maisha, bali tunawaona viongozi wa chama na serikali ndiyo wanakuwa na maendeleo, kwa kweli inatia uchungu kuona nchi iliyokuwa na kila neema lakini asilimia kubwa ya watu wake wapo kwenye umasikini mkubwa. Na tatizo lingine ni kutumia kila kitu kuwa ni siasa, tumepika takwimu za ajabu na sasa tunaambiwa kuwa tupo kwenye uchumi wa kati, tukaamini uongo wetu, sasa inatugharimu kwa uongo huo, tungekuwa tuna uchumi wa kati tusingesikia haya malalamiko mitaani.