Tatizo letu ni lile lile la kudhani kuwa Tanzania inakwisha sisi tulio hai tunapokufa!. Ni tatizo la mtazamo wetu wa kiafrika.
Kila kitu ni muhimu, kuendeleza elimu ni muhimu, kujenga SGR ni muhimu pia, kumbuka kuwa hiyo bahari ni mtaji mkubwa sana tukiwa na mataifa yanayotuzunguka yaliyo mbali na maji ya bahari.
Hakuna njia ya mkato ya kuinua uchumi wa nchi, tukiwa na mawazo ya kibinafsi tunaweza tusione umuhimu wa kodi lakini tukiitazama nchi na mustakabali wake tutakuwa wepesi kutambua kuwa hatuna ujanja zaidi ya kuweka msisitizo kwenye makusanyo ya kodi.
Maendeleo ya kweli yana gharama zisizokwepeka, hao wanaotusaidia kila mwaka kuna wakati unafika wanatuchoka.
Bukililo plz usifunge ubongo wako kuona uko sahihi 100%
Jaribu kufungua akili yako usikilize hata ambayo akili yako haitakibkusikia.
Mfano;
Wewe una milioni 10
Unataka;
Ujenge nyumba nzuri
Ununue gari
Uwe na bishara kubwa at the same time unaweza?
Utakachofanya utaanza na biashara ndipo ununue kiwanja kutokana na faida then mengine yataendelea.
Kwa mifano ya Shigongo kuwa uchumi umeshuka na kuwa kwa 4.8% toka 6.8%
Akatoa sababu kuwa utalii umeshuka nk.
Serikali ilitakiwa ijiongeze namna ya kuinua uchumi...
sio kuwa watalii hakuna bali wamepungua, yaani tunagawana watalii wachache...wengine Kenya, Uaganda nk.
Hapa inahitaji kuongeza tozo?
Hapana, hapa ni kupunguza baadhi za tozo kwa watalii ili kuwavutia wengi kuichagua Tz.
Faida yake ni kuongeza pesa mtaani na serikali inaongeza mapato pia.
Je kulipa kodi ni vibaya? Hasha
Kulipa kodi ni sahihi 100%
Lakini utaongezaje kodi wakati wa mdororo?
Hali za wananchi ni taabani tena unawaongezea kodi?
Miradi ya maendeleo ni kosa?
Hapana, bali kulingana na mdororo wa uchumi chagua michache ifanyike awamu hii na ikamilike 100% ianze kuleta matokeo chanya na ndipo mingine iendelee kujengwa.
Sasa unataka kuinua elimu, bwawa la nyerere, sgr, maji huku pesa huna utaweza?
Priority ni muhimu katika kufanikisha jambo lolote.
Naunga mkono kodi lakini sio kwa kiwango hiki cha unyonyaji