Rais Samia amepoteza mwelekeo mapema sana, hawezi kutoboa!

Rais Samia amepoteza mwelekeo mapema sana, hawezi kutoboa!

Miluzi mingi humpoteza mbwa. Hajui amfurahishe nani matokeo yake anapotea kabisa. Hana vision yake mwenyewe, makada na mafisadi wamemzunguka na kumshauri kwa manufaa yao wenyewe kitu ambacho kimemuingiza chaka vibaya mno hata kabla ya dakika ya 10.

Alianza vizuri mno ila alipoanza kuwasikiliza ndio kaharibu na bahati mbaya anafuata tu sijui ndio hofu ya kuendesha gari kubwa
Upo sahihi mkuu
 
Tuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Mkuu hilo OBWE hata CCM wenyewe wanalijua ndio maana sasa wanawateua na kuwapa vyeo wapinzani kwa mgongo wa kuunga JUHUDI. Hawakuwatayarisha vijana wao vyema, ndio maana unaona wanaotumbukiwa ni wa ccm na sio WAUNGA JUHUDI
 
Tatizo wenye nia mbaya walikuwa wanategesha ili wapate agenda ya kuisimamia ili kumkwamisha hata angefanyake Bado wangemtafutia sababu.

Hii ni sawa na Mkulima kupanda mbegu leo kwa matarajio ya kuvuna baada ya siku mbili.

Wacha mapambano yaendelee atakayeshinda atapigiwa makofi na dhambi ileile atakayoitumia kushinda itatumika kwa kiwango kilekile kumtafuna.

Haya yote yanatakiwa kupimwa kwa kipindi kimoja Cha bajeti kelele zozote kabla ya kipindi hicho hazisaidii ni sawa na refa akishaamuru penati lazima mpira uwekwe Kati hata kama hutakubaliana naye.
Mkuu katali hakuna mkulima hata mmoja mwenye akili mbovu kama unavyodhani kwamba akipanda mbegu leo atavuna kesho, wakulima hawana akili hizo labda wanasiasa uchwara wanao hamahama vyama. Mkulima ndio anayekufanya uendelee kuishi.
 
CHADEMA ni li Chama la Wapuuzi wengi sana! Wanadhani kiongozi bora lazima afuate matakwa yao ! Rais Samia yuko sawa sana , aachane na hawa wapuuzi na mediocres wasio na ajenda za muda mrefu! Mama piga kazi na tuko nyuma yako 100%.
 
Nimekuja na hii mada kwa makusudi mawili, moja kuwapa angalizo watanzania wenzangu na pili kujiandaa kwa mengi na makubwa yatakayofuata hapa Tanzania.

Kwa sasa sio siri tena, matazamio ya mabadiliko makubwa yenye tija kwenye uchumi na siasa hapa Tanzania chini ya utawala wa mama Samia yameyuka ghafla na kwa haraka sana. Tayari mama Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka kwenye makundi makubwa ya kijamii na kisiasa. Matumaini hayapo tena.

Wataalamu wa siasa wanasema siasa ni agenda, na mwanasiasa ukipoteza agenda inayokubeba maana yake umepoteza mwelekeo. Wakati mama Samia Suluhu anaingia madarakani, agenda nne muhimu (Haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza, Maridhiano ya kisiasa na Uchumi binafsi) zilikuwa mkononi mwake na alionekana kuwa na fikra chanya za kuzitumia vyema katika safari yake ya kisiasa, bahati mbaya sana kwa sasa karibu agenda zote zimemponyoka ghafla kutoka mikononi mwake, hana tena pa kushika. Rangi halisi ya utawala wa mama Samia tumeweza kuijua sasa, ni utawala wa ovyo ovyo, hauna kipya wala chema cha maana sana cha tofauti na utawala uliopita wa Magufuli.

Kupanda kwa nishati (mafuta ya petrol na diesel) na miamala ya simu kulikofanywa kimakusudi na serikali ya mama Samia Suluhu kumeua matumaini yote ya vyuma kuachia. Maisha ya msoto yameongezeka zaidi kwa watanzania kuliko kipindi cha Magufuli na wakati huo huo ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa umma umeporomoka. Mambo ni ovyo ovyo.

Kupigwa kumbo kwa mchakato wa katiba mpya (ambao upo kisheria) na kuzuiwa kwa shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani (ambapo kupo kikatiba) ni kosa kubwa zaidi lililofanywa na utawala wa mama Samia Suluhu. Hakuna namna ataweza kupambana kinguvu kupingana na harakati za wanasiasa wa upinzani na wanaharakati, mama huenda akapelekwa mchaka mchaka mpaka ajute.

Mama Samia kwa sasa anajaribu kuiga mbinu mbovu na mbaya za kisiasa na kiuchumi za utawala wa Magufuli wakati yeye sio Magufuli na hawezi kuwa kama Magufuli. Njia aliyoichagua mama Samia ni njia mbovu, mbaya na yenye mwisho mbaya. Poor and dead ended path, kwa lugha rahisi hawezi kutoboa.

Waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita!
True
 
Mambo Mema aliyo yafanya kwa muda mfupi si ajabu sasa yakafunikwa na makosa kidogo ya kiufundi ambayo ukiyatizama utaona kabisa wasaidi wake ndio wanasitahili wakinywe hiki kikombe badala yake, tozo na milipko ya bei wasaidizi wake wanao Shinda bungen ndio walipaswa kuliona hili LA miamala ya pesa kama Lina athari au la, vinginevyo inabidi alitizame upya koti alilofaa
 
Hizo ni fikra zako na mtazamo wako South Africa wana katiba bora kabisa cha ajabu mtu aliyefanya ufisadi anatetewa na wafuasi wake katiba siyo muarubaini, Kenya pia kuja katiba mpya lakini ufisadi kama kawaida.
Ona kama huyu eti nae ni mpinzani!

Ni ujinga mtupu mkuu
Screenshot_20210714-160521_Telegram.jpg
 
Akina mkwere wanamwendedha kama gari bovu, Yaani kushoto, kulia, kushota, kulia yaani ameanza kupoteza mwelekeo!
 
Hakuna lolote! Mama yuko njia sahihi kwa agenda alizojiwekea.

Kawafanyia CHADEMA mengi kwa muda mchache mkaanza dharau na matusi.

Tukawaonya ya kuwa mtafanya mama akaze kamba na wahanga mtakuwa nyie!

Mama endelea kuupigia mwingi. HAKI, NIDHAMU, NA WAJIBU!

Kazi Iendelee!
Kwa hiyo maadhara wanayapata CHADEMA peke yao?,..Petroli/Dizeli ina bei ya CHADEMA na ambao sio CCM?,makato ya miamala yapo ya wana CHADEMA na kwa wana CCM?
 
Bukililo plz usifunge ubongo wako kuona uko sahihi 100%
Jaribu kufungua akili yako usikilize hata ambayo akili yako haitakibkusikia.
Mfano;
Wewe una milioni 10
Unataka;
Ujenge nyumba nzuri
Ununue gari
Uwe na bishara kubwa at the same time unaweza?
Utakachofanya utaanza na biashara ndipo ununue kiwanja kutokana na faida then mengine yataendelea.

Kwa mifano ya Shigongo kuwa uchumi umeshuka na kuwa kwa 4.8% toka 6.8%
Akatoa sababu kuwa utalii umeshuka nk.
Serikali ilitakiwa ijiongeze namna ya kuinua uchumi...
sio kuwa watalii hakuna bali wamepungua, yaani tunagawana watalii wachache...wengine Kenya, Uaganda nk.
Hapa inahitaji kuongeza tozo?

Hapana, hapa ni kupunguza baadhi za tozo kwa watalii ili kuwavutia wengi kuichagua Tz.

Faida yake ni kuongeza pesa mtaani na serikali inaongeza mapato pia.

Je kulipa kodi ni vibaya? Hasha
Kulipa kodi ni sahihi 100%
Lakini utaongezaje kodi wakati wa mdororo?
Hali za wananchi ni taabani tena unawaongezea kodi?

Miradi ya maendeleo ni kosa?
Hapana, bali kulingana na mdororo wa uchumi chagua michache ifanyike awamu hii na ikamilike 100% ianze kuleta matokeo chanya na ndipo mingine iendelee kujengwa.
Sasa unataka kuinua elimu, bwawa la nyerere, sgr, maji huku pesa huna utaweza?

Priority ni muhimu katika kufanikisha jambo lolote.
Naunga mkono kodi lakini sio kwa kiwango hiki cha unyonyaji
WELL SAID MKUU👊
 
Back
Top Bottom