Rais Samia amepoteza mwelekeo mapema sana, hawezi kutoboa!

Nimekuja na hii mada kwa makusudi mawili, moja kuwapa angalizo watanzania wenzangu na pili kujiandaa kwa mengi na makubwa yatakayofuata hapa Tanzania.

Kwa sasa sio siri tena, matazamio ya mabadiliko makubwa yenye tija kwenye uchumi na siasa hapa Tanzania chini ya utawala wa mama Samia yameyuka ghafla na kwa haraka sana. Tayari mama Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka kwenye makundi makubwa ya kijamii na kisiasa. Matumaini hayapo tena.

Wataalamu wa siasa wanasema siasa ni agenda, na mwanasiasa ukipoteza agenda inayokubeba maana yake umepoteza mwelekeo. Wakati mama Samia Suluhu anaingia madarakani, agenda nne muhimu (Haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza, Maridhiano ya kisiasa na Uchumi binafsi) zilikuwa mkononi mwake na alionekana kuwa na fikra chanya za kuzitumia vyema katika safari yake ya kisiasa, bahati mbaya sana kwa sasa karibu agenda zote zimemponyoka ghafla kutoka mikononi mwake, hana tena pa kushika. Rangi halisi ya utawala wa mama Samia tumeweza kuijua sasa, ni utawala wa ovyo ovyo, hauna kipya wala chema cha maana sana cha tofauti na utawala uliopita wa Magufuli.

Kupanda kwa nishati (mafuta ya petrol na diesel) na miamala ya simu kulikofanywa kimakusudi na serikali ya mama Samia Suluhu kumeua matumaini yote ya vyuma kuachia. Maisha ya msoto yameongezeka zaidi kwa watanzania kuliko kipindi cha Magufuli na wakati huo huo ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa umma umeporomoka. Mambo ni ovyo ovyo.

Kupigwa kumbo kwa mchakato wa katiba mpya (ambao upo kisheria) na kuzuiwa kwa shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani (ambapo kupo kikatiba) ni kosa kubwa zaidi lililofanywa na utawala wa mama Samia Suluhu. Hakuna namna ataweza kupambana kinguvu kupingana na harakati za wanasiasa wa upinzani na wanaharakati, mama huenda akapelekwa mchaka mchaka mpaka ajute.

Mama Samia kwa sasa anajaribu kuiga mbinu mbovu na mbaya za kisiasa na kiuchumi za utawala wa Magufuli wakati yeye sio Magufuli na hawezi kuwa kama Magufuli. Njia aliyoichagua mama Samia ni njia mbovu, mbaya na yenye mwisho mbaya. Poor and dead ended path, kwa lugha rahisi hawezi kutoboa.

Waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita!
Mkome naona wapinzan mliona mmepata dirisha! Dirisha closed mnahaha.

Aliyekuwa anajua mafanikio mazuri na aliyekuwa anatupeleka vzr ni JPM.

Hakuna kitu kizuri kama unatoa kodi na unaona mabadiliko katika nch yako.
Hapa saivi ni kuombeleza misaada kila siku tumeongea na nchi fulani...tumeongea na nchi fulani wameahid kutisaidia
(Back utumwani)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo Mema aliyo yafanya kwa muda mfupi si ajabu sasa yakafunikwa na makosa kidogo ya kiufundi ambayo ukiyatizama utaona kabisa wasaidi wake ndio wanasitahili wakinywe hiki kikombe badala yake, tozo na milipko ya bei wasaidizi wake wanao Shinda bungen ndio walipaswa kuliona hili LA miamala ya pesa kama Lina athari au la, vinginevyo inabidi alitizame upya koti alilofaa
 
Tumuombee peke yake hawezi. Yeye ni mwanadamu tuu.Mungu ampe unyenyekevu na busara.
Tumuombee MTU mwenye kiburi?.wewe MTU anatusalimia kwa jina LA jamuhuri tunamuombea kwa Mungu yupi?,wa jamuhuri au?.acha ademke anavyoweza tutakutana 2025
 
Huyu Mama wa kambo tunatakiwa tumuue kama yule Baba wa kambo kutoka Chato.
 
Nimekuja na hii mada kwa makusudi mawili, moja kuwapa angalizo watanzania wenzangu na pili kujiandaa kwa mengi na makubwa yatakayofuata hapa Tanzania.

Kwa sasa sio siri tena, matazamio ya mabadiliko makubwa yenye tija kwenye uchumi na siasa hapa Tanzania chini ya utawala wa mama Samia yameyuka ghafla na kwa haraka sana. Tayari mama Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka kwenye makundi makubwa ya kijamii na kisiasa. Matumaini hayapo tena.

Wataalamu wa siasa wanasema siasa ni agenda, na mwanasiasa ukipoteza agenda inayokubeba maana yake umepoteza mwelekeo. Wakati mama Samia Suluhu anaingia madarakani, agenda nne muhimu (Haki za binadamu, Uhuru wa kujieleza, Maridhiano ya kisiasa na Uchumi binafsi) zilikuwa mkononi mwake na alionekana kuwa na fikra chanya za kuzitumia vyema katika safari yake ya kisiasa, bahati mbaya sana kwa sasa karibu agenda zote zimemponyoka ghafla kutoka mikononi mwake, hana tena pa kushika. Rangi halisi ya utawala wa mama Samia tumeweza kuijua sasa, ni utawala wa ovyo ovyo, hauna kipya wala chema cha maana sana cha tofauti na utawala uliopita wa Magufuli.

Kupanda kwa nishati (mafuta ya petrol na diesel) na miamala ya simu kulikofanywa kimakusudi na serikali ya mama Samia Suluhu kumeua matumaini yote ya vyuma kuachia. Maisha ya msoto yameongezeka zaidi kwa watanzania kuliko kipindi cha Magufuli na wakati huo huo ufanisi wa utendaji kwa watumishi wa umma umeporomoka. Mambo ni ovyo ovyo.

Kupigwa kumbo kwa mchakato wa katiba mpya (ambao upo kisheria) na kuzuiwa kwa shughuli za siasa kwa vyama vya upinzani (ambapo kupo kikatiba) ni kosa kubwa zaidi lililofanywa na utawala wa mama Samia Suluhu. Hakuna namna ataweza kupambana kinguvu kupingana na harakati za wanasiasa wa upinzani na wanaharakati, mama huenda akapelekwa mchaka mchaka mpaka ajute.

Mama Samia kwa sasa anajaribu kuiga mbinu mbovu na mbaya za kisiasa na kiuchumi za utawala wa Magufuli wakati yeye sio Magufuli na hawezi kuwa kama Magufuli. Njia aliyoichagua mama Samia ni njia mbovu, mbaya na yenye mwisho mbaya. Poor and dead ended path, kwa lugha rahisi hawezi kutoboa.

Waswahili wanasema mkataa pema pabaya panamwita!
Maneno mengi kumbe essense ni hiyo mambo ya Katiba ya kuibeba Chadema.

Hiyo mtaipata labda 2125, mengine unayoongea ni hadithi za kufikirika unazotaka zitokee unfortunately itaishia kuwa Dua la kuku
 
Back
Top Bottom