Kukopa ni aibu yetu sote kama watanzania. Na hatujapata suluhisho la kudumu.
Kumshambulia SSH kwa kukopa ni kutomtendea haki tukizingatia ukweli kuwa sio wa kwanza kukopa. Na anakopa kufanya kazi zinazoonekana.
Kusema kukopa ni laana wakati huna wazo mbadala litakaloingiza pesa hazina ya nchi , ni kujidanganya. Ni fikra zile zile za JPM za sisi ni matajiri wakati huo utajiri bado upo ardhini na anamtegemea Dotto James aongee na wazungu ili tupate mikopo.
Hakuna dhambi yoyote ya kuchukua mikopo, ikiwa JPM mwenyewe alikuwa akijisifu kuwa mabosi wa benki ya dunia walikubali kutupa mkopo wa kujenga flyover ya Ubungo na akisema hivyo pembeni yake akiwa amekaa bosi wa benki ya dunia!.
SSH akikopa ni nongwa ya kuanzishia uzi kabisa lakini JPM akifanya hivyo ni suala zuri tu, unafiki ni wa kwako wewe.