Rais Samia ameshindwa kutolea tamko matatizo ya Umeme na Maji yanalolikumba Taifa?

Rais Samia ameshindwa kutolea tamko matatizo ya Umeme na Maji yanalolikumba Taifa?

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Ukimya sawa na pengine ana kazi nyingi ambazo kwalo huenda wasaidizi wake wanamjazia mafaili ili kumzubaisha na ili asitambue changamoto za hapa na pale ziwahusuzo Watanzania.

Lakini kwa changamoto ya umeme na maji inaloikumba Taifa kwa sasa si kitu kilichojificha na ni ukweli kwamba Samia anafahamu ila amechagua kuwa kimya kwa makusudi kabisa kwa sababu anazozijua yeye.

Jamani tupeni maji na umeme hayo mengine kama upigaji wa Bandari ya Bagamoyo endeleeni nayo wala hayupo wa kuwauliza.
 
Madhara ya kuteau mtu kwenye uwaziri kwa vigezo mtoto wa kada wa CCM.

Unamuondoaje waziri wa nishati unataka kutangaza vita na Wazee wa Chama.

Vimemo vinateu nafasi

Rais lazima akae kimya hana namna ya kufanya
 
Ndio tutambue kuwa na mifumo mizuri ya kuwa andaa viongozi (vetting) na hii mentality ya kila jambo rais, rais hatuwezi fika kwa njia hii wakuu
 
Lingine linaunguruma KEKEKE, hayo ndiyo yatakuwa maisha yetu

nchi itapaa kiuchumi, jenereta zitanunuliwa sasa, lita moja ya petroli kuna 700 ya kodi na tozo
 
Mbona wenzetu Zanzibar hawanung'uniki kama sisi huku Nchi kavu au wao mambo yao ni sawia?
 
Ukimya sawa na pengine ana kazi nyingi ambazo kwalo huenda wasaidizi wake wanamjazia mafaili ili kumzubaisha na ili asitambue changamoto za hapa na pale ziwahusuzo Watanzania.

Lakini kwa changamoto ya umeme na maji inaloikumba Taifa kwa sasa si kitu kilichojificha na ni ukweli kwamba Samia anafahamu ila amechagua kuwa kimya kwa makusudi kabisa kwa sababu anazozijua yeye.

Jamani tupeni maji na umeme hayo mengine kama upigaji wa Bandari ya Bagamoyo endeleeni nayo wala hayupo wa kuwauliza.

Anashughulikia ajira za wazanzibari kwanza. Tayari 21% wanapaswa kuwa wao JMT.

Na akaze zaidi hadi ile misukule iweze kutoka usingizini huko iliko.
 
MAJI NI UHAI NDUGU ZANGU. NARUDIA TENA, MAJI NI UHAI. BILA MAJI HAKUNA UHAI......
 
Back
Top Bottom