Rais Samia ametoa kiasi cha Tsh. Milioni 500 baada ya taifa Stars kufuzu 16 bora

Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 03, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu walipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa, Mheshimiwa Rais amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.

Zimetokana na fungu gani la bajeti? Inaonekana kuwa Bajeti ya serikali yetu huwa inakuwa na pesa nyingi zisizokuwa na matumizi zinaishia kufyekwa tu. Ni kweli wachezaji wanahitaji kupewa motisha lakini siyo kwa njia hiyo. Angehamasisha harambee ya kuchangisha kutoka makampuni na raia kwa ajili hiyo kama alivyoitisha harambee ya CCM, ingekuwa na mantiki kidogo
 
Vipi angenunulia madaftari, kuwashonea sare, na ada kwa watoto wasio na uwezo..?
 
Mama ma maeeee... jumla ni milioni 800, kuna shule wanafunzi wanakaliq mawe, kuna sehemu maji ni kipengele.
Kuna shule niliiona mbagala kizuiani,yaani imeozaaaa ukiambiwa ipo Dsm unaweza ukalia.
Halafu unakuja kusoma ujinga kama huu 😭 kama vipi trump atupe nyukilia Tz ianze upya tu!
 
Kuna watu wamekuwa machawa, macho wamefumba.. taifa hili ni matusi makubwa kutoa milioni 800 kwa ajili ya timu..
 
Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 03, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu walipotembelewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa, Mheshimiwa Rais amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco.

Nilitamani itoke 500 mln $.Kwani utajiri tunao
 
Back
Top Bottom