tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Kabla sijaenda mbali naomba ku declare interest kwamba mm ni mtu mwenye asili ya Zanzibar. Nimesikitishwa sana na aina ya uwekezaji ambao mama Samia ameufanya hapa Kizimkazi. Inasikitisha sana.
Tangu Zanzibar iungane na Tanganyika, waZanzibar hawajawahi kuenjoy rasilimali za Tanzania ndewe wala sikio. Kila siku matanganyiko ndio yanafaidi rasilimali za nchi. Nilitegemea baada ya mzanzibar kupokea kijiti cha urais, Zanzibar ingepata afueni lakini kila kukicha inazidi kudidimia kwenye dimbwi la umasikini.
Rais Magufuli aliposhika usukani wa nchi alipeleka nyumbani kwao Chato maendeleo makubwa sana. Alijenga International Airport, barabara na madaraja makubwa. Pia alisogeza huduma kwa wananchi kwa kuwajengea benki, chuo cha VETA na hospitali ya rufaa. Kana kwamba haya hayatoshi, Magufuli alianzisha mbuga ya wanyama Chato na kujenga ikulu ndogo. Haya ni baadhi ya mambo machache ninayoweza kuyakumbuka ambayo Magufuli aliwafanyia wananchi wake.
Sasa tukirejea kwa Rais Samia alichowafanyia wanaKizimkazi ni kichekesho na kituko cha mwaka. Eti kawajengea Football Academy na kuwapelekea tamasha! What kind of nonsense is this? Ndio maana nasema Wazanzibar hawaji kuendelea kamwe hata wakimpata Rais wa dunia. Mama Samia anashindwaje kuiga kwa mtangulizi wake anakuja kuwaletea wanaKizimkazi miradi uchwara ambayo hailingani hata kwa asilimia moja na miradi ambayo Magufuli aliwapelekea wanaChato?
Wazanzibar wataendelea kubaki hivi hivi hadi kiyama. Kila mtu mwenye nia njema alipoona mzanzibar kaingia ikulu alisema hewallah Mola atupe nini! Matokeo yake mzanzibar kabisa tena anayetarajiwa kuwanyanyua wazanzibar wenzake anawafanyia dhihaka. Yakhe unyonge huu hadi lini?
Wakati anahangaika kuwahamisha wamasai kutoka Ngorongoro kwenda Msomela tulidhani labda angewaacha wakae huko huko lakini ahamishe wanyama awalete Kizimkazi aanzishe mbuga ya Kizimkazi lakini ameamua kukomaa na wamasai na kuwaacha wanyama.
Zanzibar hawana hata mbuga moja ya wanyama. Rais Samia anashindwa nini kumzuia Rais Hussein Mwinyi asiuze visiwa vyote walau aache kisiwa kimoja tukibadilishe kuwa mbuga ya wanyama? Mbuga zote zipo Tanganyika, sisi hatunayo hata moja. Kama Magufuli aliweza kuhamisha wanyama akaanzisha mbuga yeye anashindwaje?
Kusema kweli Rais Samia anapaswa awaombe radhi wazanzibar kwa hii dharau aliyowafanyia kuwapelekea miradi uchwara huku akiwaacha watanganyiia wakijipendelea kwa miradi mikubwa mikubwa. Inauma na inasikitisha sana.