Rais Samia amewateua Diamond na Shilole kuwa Wajumbe wa Baraza la Malaria

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mwimbaji Staa wa Bongofleva Naseeb Abdul Diamond Platnumz @diamondplatnumz na Msanii Zuwena Mohamed Shilole @officialshilole kuwa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu ametangaza uteuzi huo katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Dar es salaam ambapo Mgeni rasmi ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

"Asilimia 77 ya Watanzania ni Vijana imempendeza Rais Dkt. Samia kumteua Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwa Mwakilishi wa Vijana katika Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria akiwakilisha Wasanii wa kiume, Diamond ana followers Mil 15.9 kwahiyo akiandika tu ‘Sio kila homa ni Malaria’ inawafikia Watu Mil 15.9 ndani ya sekunde moja”

"Rais amemteua Zuwena Mohamedi Shilole Mwakilishi wa Vijana Wasanii Wanawake kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria”
 
Mantiki ya uteuzi huo imekaa kiuupuzi na kijinga kabisa. Sitaki kuamini Rais Samia na washauri wake wako very low kiasi hicho.

Ngoja tuchambue hapa.
1. Kama sababu ya uteuzi huo ni kuwa na followers wengi mitandaoni, mbona Shilole hana followers wengi mtandaoni kupita wasanii wengine wa kike na bado wamemteua?

2. Kama sababu ni kuhakikisha ujumbe unawafikia watu wengi kupitia followers wake kwa muda mfupi, kwanini serikali isimpe Diamond mkataba na ubalozi wa heshima wa malaria ili aifanye hiyo kazi ya kutumia ukurasa wa mtandao wake kuandika malaria?

3. Ni kwa vipi Diamond kuwa mjumbe wa baraza la Malaria automatically ataanza kuandika mambo ya malaria kwenye ukurasa wake mtandani?
Hizi serikali inajua ni gharama kiasi gani za kiusanii Diamond ametumia na anatumia kuwapata na kuwatunza hao followers zake?
Hizi serikali inajua hao followers wa Diamond wataanza kupungua kwa kasi kadri Diamond atakavyoanza kuwawekea vitu irrelevant (kama jumbe za malaria) na kile kilichowavutia mpaka kumfollow yeye?

4. Toka lini majukumu ya msingi ya mjumbe wa baraza la malaria yakawa ni kupost habari za Malaria mtandaoni?
 
Mdogoangu kamaliza public health miaka mitatu yupoo tuu mtaani, hata kupewa kijitenda cha kuelimisha jamii na M/kata Hollaaa.
 
Wanateuliwa watu ambao hata elimu ya malaria hawaijui
Duh aise,mambo ni bora liende

Hivi wanawalipa au wanajitolea

Ova
 
Back
Top Bottom