BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mwimbaji Staa wa Bongofleva Naseeb Abdul Diamond Platnumz @diamondplatnumz na Msanii Zuwena Mohamed Shilole @officialshilole kuwa Wajumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu ametangaza uteuzi huo katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Dar es salaam ambapo Mgeni rasmi ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
"Asilimia 77 ya Watanzania ni Vijana imempendeza Rais Dkt. Samia kumteua Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz kuwa Mwakilishi wa Vijana katika Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria akiwakilisha Wasanii wa kiume, Diamond ana followers Mil 15.9 kwahiyo akiandika tu ‘Sio kila homa ni Malaria’ inawafikia Watu Mil 15.9 ndani ya sekunde moja”
"Rais amemteua Zuwena Mohamedi Shilole Mwakilishi wa Vijana Wasanii Wanawake kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Kutokomeza Malaria”