Rais Samia amewezaje kufanya haya yaliyowashinda Marais wote?

NUMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2019
Posts
807
Reaction score
1,164
Nipo jijini mwanza kiukweli mji unapendeza. Nimepita maeneo karibia yote makoroboi, nyasaka, nyamhongolo, buhongwa. Dah!

Siamini machinga wote wamehama tena wenyewe kwa mikono Yao, wamebomoa wenyewe bila vurugu zozote.

Mama Samia amewezaje ilihali watangulizi wake wote walishindwa na walipojaribu lilikuwa ni bomu hatari Sana...#raissamiaisaluteyou

Hizi ni picha nilizopiga maeneo ya buhongwa ambapo lilikuwa ni eneo hatari Sana kuwaondoa machinga!

January aliwezaje kutoa mifuko ya plastic? amekutuma uje umsifie hapa?
Mkuu cheki picha hapo juu...Wala Mimi sijatumwa na mtu...Mimi ni mtu wa KAWAIDA Sana..Ila nashindwa kuamini ametumia uchawi gani? Kumbuka waliokuwa wanaondolewa Kisha wanarudi Ila now ni tofauti....wewe huko uliko Hali ikoje?
 
Subiri baada ya mwaka ndio useme kafanikiwa.
 
Pumbavu Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete hawakuwaleta Machinga barabarani.

Samia anatatua tatizo aliloanzisha Magufuli tena yeye akiwa Number 2.
Kwani huwezi kujibu hoja bila kutukana? Ndo shida ya kuishi kwa mume wa dada yako!
 
Walirudi itakuwa ujinga wa mamlaka zote anzia manispaa halmashauri police DC RC wote watakuwa hovyo
 
Kwa akili yako ilivyo fupi hao wamachinga vyuma vimelegea hela zimejaa mfukoni mwao
 
Mkuu cheki picha hapo juu...Wala Mimi sijatumwa na mtu...Mimi ni mtu wa KAWAIDA Sana..Ila nashindwa kuamini ametumia uchawi gani? Kumbuka waliokuwa wanaondolewa Kisha wanarudi Ila now ni tofauti....wewe huko uliko Hali ikoje?
Kwani kipindi cha kampeni kimeshapita? Wewe utakuwa mtoto uliyezaliwa mwaka 2005. Ulizia kuhusu machinga wa Congo na Ubungo Tanesco, ukielewa, edit mawazo yako.
 
Baada ya muda watarudi tena maana tatizo halijapata ufumbuzi wa kudumu.
Utapelekaje huduma za kijamii mbali na makazi ya watu.
Yaani mtu alipe elfu 1 kwenda kununua Ndizi za elfu 2. Kweli?!!
 
Baada ya muda watarudi tena maana tatizo halijapata ufumbuzi wa kudumu.
Utapelekaje huduma za kijamii mbali na makazi ya watu.
Yaani mtu alipe elfu 1 kwenda kununua Ndizi za elfu 2. Kweli?!!
Una mifano hai? Maana huku niliko wamehamia karibu na makazi ya watu...mfano soko la kiloleli,nyasaka nk
 
Una mifano hai? Maana huku niliko wamehamia karibu na makazi ya watu...mfano soko la kiloleli,nyasaka nk
1.Mi nipo Buswelu kona. Wameondoa vibanda vya mboga mboga wamepeleka Wilayani.
Nauli ya kutoka hapa mpaka wilayani ni elfu 1 kwenda na kurudi.

2.Machinga wa Makoroboi wamepelekwa Igogo. Toka mjini mpaka Igogo ni mia nane kwenda na kurudi.
Huoni hiyo?
 
wameacha uchafu hao jamaa HONGERA TELE KWA RAIS SAMIA MAMA NI MAMA ULIMI WAKE WA UPOLE NI DAWA
 
Unatuonyesha Uchafu ili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…