Rais Samia amezindua makao makuu ya benki ya Ushirika Tanzania

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua makao makuu ya benki ya ushirika Tanzania

View: https://www.youtube.com/watch?v=9c3a8yFwdSA

Rais Samia Suluhu Hassan

Ameeleza kuwa amefurahi benki hiyo haijaanza kinyonge kwani imeanza na mtaji wa Tsh. Bilioni 58 huku akisema ana imani benki hiyo itaenda kuyagusa maisha ya Watanzania hususan wakulima.

Amezitaka benki nyingine kushirikiana na benki hiyo ili kuwasaidia wananchi na siyo kushindana nayo kwani haipo kwa ajili ya kuwapindua. Amesisitiza kuwa ni wakati wa ushirika kuchukua nafasi yake ili kuchangia ukuaji wa pato la Taifa.

Rais amewataka ushirika wabadilike ili wawe imara zaidi. Anasema yeye ni miongoni mwa watu waliokuwa wanauona Ushirika kama chaka la wizi, hata hivyo amewapongeza kwa kusimama vizuri.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Ameeleza kuwa vyama vikuu vya ushirika vimeshanunua 51% ya share. Ambapo benki hiyo inaanza na mtaji wa Bilioni 58 huku ikiwa na matawi manne ikiwemo makao makuu Dodoma, tawi lingine lipo Tandahimba, Kilimanjaro na Tawi la nne lipo Tabora. Aidha matawi hayo yatatumia majengo ya serikali ili kupunguza gharama.

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya ushirika Tanzania Godfrey Mura

Wakati akieleza historia ya bank hiyo ameeleza kuwa matawi yanayofuata kufunguliwa ni Dar es salaam, Kagera na Mwanza. Ameeleza kuwa hii si tu benki ila ni movement (vuguvugu) ya kunufaisha Watanzania wengi, huku dhamira ikiwa ni kuhakikisha angalau 50% ya Watanzania wawe katika mfumo rasmi wa kibenki kufikia 2030 na wanachama wasiopungua milioni 10.
 
Hakuna anayefuatilia, Wote wanafuatilia kesi ya uongo ya Lissu
Uwepo wa h comment yako inaonyesha tayari una taarifa ya h shughuli ya rais 😂

Afu sema n ww ndo unafatilia kesi na sio wote, kuna wengn wapo kwenye biashara zao, hawajui kuna kesi ya Lissu wala hawajui rais anazindua nn.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua makao makuu ya benki ya ushirika Tanzania

View: https://www.youtube.com/watch?v=9c3a8yFwdSA

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza kuwa vyama vikuu vya ushirika vimeshanunua 51% ya share. Ameeleza kuwa benki hiyo inaanza na mtaji wa Bilioni 58 huku ikiwa na matawi manne ikiwemo makao makuu Dodoma, tawi lingine lipo Tandahimba, Kilimanjaro na Tawi la nne lipo Tabora. Aidha matawi hayo yatatumia majengo ya serikali ili kupunguza gharama.

Huyu mpuuzi anapotezea watu time tu.
 
Kwani Lissu ameshafikishwa mahakamani kusikiliza ile kesi yake ya mchongo ya uhaini, au mambo ya kitoto bado yanaendelea?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua makao makuu ya benki ya ushirika Tanzania

View: https://www.youtube.com/watch?v=9c3a8yFwdSA

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza kuwa vyama vikuu vya ushirika vimeshanunua 51% ya share. Ameeleza kuwa benki hiyo inaanza na mtaji wa Bilioni 58 huku ikiwa na matawi manne ikiwemo makao makuu Dodoma, tawi lingine lipo Tandahimba, Kilimanjaro na Tawi la nne lipo Tabora. Aidha matawi hayo yatatumia majengo ya serikali ili kupunguza gharama.

Kuzindua tu. Viongozi afrika hawana kazi
 
Hakuna anayefuatilia, Wote wanafuatilia kesi ya uongo ya Lissu
hahahaaaa yaani ukiwa muongo uwe na akili kuliko wewe unakuwa muongo na akili huna kama hufuatilii umejuwaje kama hafuatiliwi? inamaana umefuatilia ukajuw ahafuatiiwi kwahiyo wewe ndiyo unamfuatilia kwa karibu sana
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua makao makuu ya benki ya ushirika Tanzania

View: https://www.youtube.com/watch?v=9c3a8yFwdSA

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameeleza kuwa vyama vikuu vya ushirika vimeshanunua 51% ya share. Ameeleza kuwa benki hiyo inaanza na mtaji wa Bilioni 58 huku ikiwa na matawi manne ikiwemo makao makuu Dodoma, tawi lingine lipo Tandahimba, Kilimanjaro na Tawi la nne lipo Tabora. Aidha matawi hayo yatatumia majengo ya serikali ili kupunguza gharama.

Hiyo Benki itakufa kibudu Kama ilivyokufa Benki ya Nyumba (THB).
 
Yaani hili taifa linavituko mliuza benki ya kilimo ndio ikaanzishwa crdb ya sasa .
 
Waliuza CRDB wenyewe leo wameona umuhimu wa bank ya ushirika tena? Kweli kuwa mtanzania ni full time job, wanapaswa watulipe aisee
 
Back
Top Bottom