"This is not Europe this is Tanzania", aache basi kuitaja Ulaya yenye railway network kila mahala + subways, na mipangilio kila mahala na maisha mazuri wa raia wake + miundombinu Bora.
Tuache kujisifiasifia, Bali tujikite kuongeza bidii na kutekeleza maana tuko nyuma ya muda saana na huko Ulaya tunakotaka kufananisha wako mbali sana na kasi sana.
Tupambane kuboresha miundombinu kila mahala na hizi railway network ziwe kila mahala.
Kumbe kulikuwa hakuna haja ya royal tour, hata hawa wangeweza tu kutusaidia Kwa gharama nafuu na uzalendo wao kwa Africa.
Ashukuliwe JPM kwa akili kubwa alizokuwa nazo na kuamua maamuzi magumu kujenga SGR na fikra za electrified train, na pia kuamua Stieggler ijengwe chapuchapu watu wapate uhakika wa umeme.
Hawa wengine wanataka kutembelea mbeleko ya JPM, naamini tusingepata zawadi ya JPM tungeendelea kuona hizi ni hadithi tu na kuishia kushangaa kwenye video huku wenye mamlaka wakiendelea kamchezo kao ka paka na panya.
Tuamke tufanye kazi kwa bidii, tuache na tukomeshe wizi, rushwa, matumizi ya hovyo ya Serikali, tupunguze ukubwa wa serikali nk.
Tuache kupenda kurelax na kujisifia kila hatua ilihali tuna hatua nyingi mara zaidi ya laki moja zimebaki.