Rais Samia amjibu Mtanzania aliyefanya Makala ya kuonesha ubora wa SGR na Vituo vyake

Mwendokasi ni morogoro road tu na kipande kidogo Cha kawawa,dar Ina barabara nyingi zaidi ya hizo,kipi kilikuaminisha shida ya usafiri itaisha kwa barabara moja?
 
"This is not Europe this is Tanzania", aache basi kuitaja Ulaya yenye railway network kila mahala + subways, na mipangilio kila mahala na maisha mazuri wa raia wake + miundombinu Bora.

Tuache kujisifiasifia, Bali tujikite kuongeza bidii na kutekeleza maana tuko nyuma ya muda saana na huko Ulaya tunakotaka kufananisha wako mbali sana na kasi sana.
Tupambane kuboresha miundombinu kila mahala na hizi railway network ziwe kila mahala.

Kumbe kulikuwa hakuna haja ya royal tour, hata hawa wangeweza tu kutusaidia Kwa gharama nafuu na uzalendo wao kwa Africa.

Ashukuliwe JPM kwa akili kubwa alizokuwa nazo na kuamua maamuzi magumu kujenga SGR na fikra za electrified train, na pia kuamua Stieggler ijengwe chapuchapu watu wapate uhakika wa umeme.
Hawa wengine wanataka kutembelea mbeleko ya JPM, naamini tusingepata zawadi ya JPM tungeendelea kuona hizi ni hadithi tu na kuishia kushangaa kwenye video huku wenye mamlaka wakiendelea kamchezo kao ka paka na panya.

Tuamke tufanye kazi kwa bidii, tuache na tukomeshe wizi, rushwa, matumizi ya hovyo ya Serikali, tupunguze ukubwa wa serikali nk.
Tuache kupenda kurelax na kujisifia kila hatua ilihali tuna hatua nyingi mara zaidi ya laki moja zimebaki.
 
" God Willing they will all come to completion"

Mwisho wa kunukuu
 
Huyo mtoa clip kasahau kabisa kwamba tuna madeni makunwa sana yamejenga SGR...😆😆😆
 
Umeongea vizuri Mkuu.

Hongera kwa kuwa mzalendo, natamani kila mmoja wetu aishi na falsafa hii.
 
Mwendokasi ni morogoro road tu na kipande kidogo Cha kawawa,dar Ina barabara nyingi zaidi ya hizo,kipi kilikuaminisha shida ya usafiri itaisha kwa barabara moja?
Kuanzia kimara mwisho kuelekea kibamba siyo mwendokasi tena

Ova
 
I Usiku katumwa ni mtu wa ikulu huko
 
Badru naye ana makelele mengi mno, ajifunze kutengeneza organised content, yaani ametumia kama dakika kadhaa kupiga makelele, nimemuona YouTube
 
Kilichonisikitisha sana tena sana ni level ya ujinga wa kumzuia kuchukua picha ndani. Mbona tukienda ulaya tunaruhusiwa kupiga picha??? Yaani ni ajabu eti hata kivuka cha Chato kile kipya kuna jamaa aliketa uzi humu alizuiwa kupiga picha yaani ni ajabu sana tena sana, hii documentary imenifanya nitoe machozi tena kwa jinsi Dkt Samia alivyojitoa na Dkt Magufuli. Nadhani kijana apewe nafasi ya kutengeneza documentary nyingine
 
Hebu ngoja tuone kwenye eneo ambalo huwa tunafeli sana tutafanyaje this time, USIMAMIZI
 
Chadema ndio wanakimbilia kukata tiketi wakati walikua wanauponda mradi,

Kama wanavyojazana kwenye ndege kule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…