Pre GE2025 Rais Samia ampa Sheikh wa Arusha Land Rover Discovery limsaidie kwenye shughuli za kidini. Hii si Rushwa kabisa?

Pre GE2025 Rais Samia ampa Sheikh wa Arusha Land Rover Discovery limsaidie kwenye shughuli za kidini. Hii si Rushwa kabisa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Nawaacha mtoe mapovu, mambo ndio kama haya, Sheikh amepewa land rover bana likamsadie kwenye kutoa huduma zake.... Hii si rushwa kabisa? Tusubiri 'zawadi' hizi ziendelee kutolewa kwa viongozi wengine wa dini.

Tunataka uchaguzi ufanyike kila mtu akiwa na fursa sawa ya kushindana, kwa namna hii mwenzangu na mimi atakuwa na nafasi ya kushindana na mtu kama huyu? TUNAFANYAJE KUMALIZA HAYA? Kwa kuendelea kuwa chawa na kulalamika?

Narusha swali kwenu Wakuu.


Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda amekabidhi gari mpya chapa ya Land Rover Discovery yenye Thamani ya Milioni 100 kwa Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma ili kuweza kumsaidia kwenye shughuli zake za kidini Mkoani hapa.

Kupata vimbwanga vingine wakati wa Uchaguzi ingia hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Paul Makonda amekabidhi gari hilo muda mchache baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa kwenye msikiti Mkuu wa Bondeni Jjjini Arusha leo Oktoba 25, 2024, akiwataja Viongozi wa dini kama msingi mkuu wa amani na utulivu unaoshuhudiwa kote nchini Tanzania.


Kwa Upande wake Sheikh Shaaban Bin Juma baada ya kukabidhiwa gari hilo, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Upendo wake kwa Watanzania, akimuombea Kheri Rais Samia pamoja na wasaidizi wake katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.:BearLaugh::BearLaugh:
Hongera zake huyo Shehe endapo kama msaada huu kweli umetolewa kwa Nia njema.

Lakini kwa jinsi uhalisia ilivyo na kwa jinsi ninavyofahamu tangu miaka mingi iliyopita, mathalani kuanzia miaka ya 1995, magari ya namna hiyo hapa nchini yalikuwa yakitolewa na hao watoaji wa magari kwa wale watu 'wavaa kaunda suti' ili waweze kuzitumia katika 'shughuli zao.' Na shughuli zao siku hizi zimepamba Moto hasa hapa nyumbani.
 
Yes,
hela ya umma inatumika hadharani kwa shekhe ambae pia ni mwananchi mlipa kodi. Tatizo liko wapi? au chuki binafsi tu gentleman. wakichangiwa unaowapenda haina Tatizo right?[emoji205]

Kutoka ulipo hadi milembe ni kama km ngapi mkuu
 
Wakuu,
gari mpya chapa ya Land Rover Discovery yenye Thamani ya Milioni 100
my observation
  1. Kwa sisi tunaojua thamani ya landrover mpya,hiyo sio bei ya gari mpya, ni bei ya used yenye hali nzuri。
  2. serikali yetu hainunui magari ya UK, tunanunua Japan, hivyo hiyo ni PR tuu Konda Boy kwa mamie!
  3. Gari itakuwa imetolewa na tajiri fulani kwa lengo la PR only。
  4. Konda Boy ndie RC wa kwanza kuvuta Range Sport,hapo anakula point 3 kuwajali Waislamu wa RChuga。
  5. Soon mtashihidia mkuu wa ma laingwanan akipatiwa landrover yake
P
 
Kanisa lipi??

..Kanisa la Kilutheri ambalo Freeman Mbowe alilichangia.

..pia amechangia Kanisa la Nabii Mwamposa.

..huu sio uchangiaji mzuri hata kama anachangia Wakristo na Waislamu.

..Serikali, na sio Raisi, ndio wachangie madhehebu ya kidini ktk miradi ya huduma za kijamii.

..pia kuwepo na fungu na utaratibu maalum wa serikali kuchangia madhehebu ya kidini na sio kuchangia bila utaratibu kama inavyofanyika sasa hivi.
 
Yes,
hela ya umma inatumika hadharani kwa shekhe ambae pia ni mwananchi mlipa kodi. Tatizo liko wapi? au chuki binafsi tu gentleman. wakichangiwa unaowapenda haina Tatizo right?🐒
I hope mtakuwa mnamfanyia service na kumuwekea wese

Ova
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemzawadia Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma gari aina ya Land Rover Discovery 4 lenye thamani ya shilingi milioni 100 ili limsaidie kwenye shughuli zake za kidini.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amemkabidhi Sheikh Shaaban gari hilo leo Ijumaa baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa kwenye msikiti Mkuu wa Bondeni Jijini Arusha leo Oktoba 25, 2024.

Wakati wa kukabidhi gari hilo RC Makonda amenukuliwa akisema yafuatayo “Huyu Baba yetu na Sheikh wetu wa Mkoa alikuja siku moja pale ofisini nikamwambia Baba nikusindikize, tukaenda mpaka tukatoka kwenye geiti nje naitafuta gari sikuiona, mwisho nikamuona anahangaika kupiga simu ‘leta huku gari leta’......alivoleta ile gari nilivyoiona moyo wangu uliingia huzuni nikasema hii gari ndio itakua ya mwanzo na mwisho kuitumia”

“Nikasema kwakuwa mimi sina pesa lakini ninae Mungu anaeweza kuniwezesha, nikampigia simu Daktari Samia Suluhu Hassan akasema hivi Viongozi wa dini we Mtoto unawapenda eeh? sijakaa sawa siku ya pili akapatikana Kijana akaniletea pesa kwahiyo leo nimekuja kumkabidhi Sheikh wangu wa Mkoa gari lake atakalokuwa analitumia kama mali yake, namshukuru sana Daktari Samia” - RC Makonda.

FaizaFoxy usimsumbue shehe kuomba lift.
Yaani hii story kama siielewi vizuri vile, anasema:
1:"... Kwakuwa sina Hela ninaye Mungu.."
2: "...Nilimpigia Simu Mam Samia,akasema ,we Mtoto unawapenda sana viongozi wa Dini?
3:Kesho alipatikana Kijana akaleta Hela...
Hapo Hela ilitoka Kwa Kijana au Mama alimtuma Kijana alete hizo pesa?
Gari alininua nani?
 
I hope mtakuwa mnamfanyia service na kumuwekea wese

Ova
itakua kama lile tuliomchangia kibaraka ombaomba la Kimataifa tu gentleman ambalo halijulikani limenunuliwa ama laa, na ya mafuta sijui ataanza kuomba omba lini 🐒
 
itakua kama lile tuliomchangia kibaraka ombaomba la Kimataifa tu gentleman ambalo halijulikani limenunuliwa ama laa, na ya mafuta sijui ataanza kuomba omba lini 🐒
Ahh ok maana aside akalipaki tu

Ova
 
Yaani hii story kama siielewi vizuri vile, anasema:
1:"... Kwakuwa sina Hela ninaye Mungu.."
2: "...Nilimpigia Simu Mam Samia,akasema ,we Mtoto unawapenda sana viongozi wa Dini?
3:Kesho alipatikana Kijana akaleta Hela...
Hapo Hela ilitoka Kwa Kijana au Mama alimtuma Kijana alete hizo pesa?
Gari alininua nani?
Kachomekewa mtu kamchukulia
Tu itakuwa kwa niaba ya maza

Ova
 
yaani shekhe wa jiji la Arusha apaki ndinga, kweli gentleman?🐒
Mufti mwenye alichukulia range kwa Lukosi alikuwa analalamika wese
We huyo sheh wa arusha labda wese awekewe lkn syo pesa ya mfukoni mwake

Ova
 
Mufti mwenye alichukulia range kwa Lukosi alikuwa analalamika wese
We huyo sheh wa arusha labda wese awekewe lkn syo pesa ya mfukoni mwake

Ova
Alhad Musa aliewahi kua shekhe wa mkoa wa Dar es salaam hadi leo ana v8 kwani anapata wap wese?

Infact,
nyakati hizi hadi mashekhe wa kata na vijiji wana mandinga ya maana gentleman huko vijijini..

ni kujipanga tu gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom