Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

16 December 2021
Abu Dhabi, UAE

FEDHA ZAIDI ZA KUKAMILISHA MRADI MZIMA WA UJENZI WA RELI MPYA SGR ZASAKWA

Waziri wa fedha Mh. Mwigulu Nchemba na ujumbe wake wapo Abu Dhabi UAE kusaka fedha za kugharamia miundo mbinu ikiwemo michepuko ya mtandao wa reli mpya SGR kama kipande cha Tabora Kigoma n.k ( Source ITV Tanzania news)
Source : Kwa kirefu : (Habari na Picha ,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Fedha na Mipango-Abu Dhabi)

……………………………………………….

Na Benny Mwaipaja, Abu Dhabi

SERIKALI ya nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu ya Abu Dhabi imeahidi kuendeleza ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na kijamii na Serikali ya Tanzania ili kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Abu Dhabi, Falme za Nchi za Kiarabu na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Rais, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nanyan, baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliowasilishwa kwake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Ikulu ya nchi hiyo.

Akizungumza baada ya mazungumzo yao ya faragha, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kuwa Sheikh Mansour ameahidi kutuma ujumbe maalum nchini Tanzania kwa ajili ya kuangalia miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa hivi sasa na mingine mipya kwa ajili ya kutoa fedha.

Dkt. Nchemba aliitaja miradi iliyowasilishwa kwa Serikali ya Abu Dhabi kuwa ni ile ya uendelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Kuzalisha Nishati ya Umeme wa Mwalimu Julius Nyerere JNHPP Rufiji, ujenzi wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, kilimo na uvuvi pamoja na elimu.

“Kwenye sekta ya elimu tumejenga madarasa mengi, tumejenga vituo vya afya vingi sana na vingine viko vijijini lakini hatujajenga nyumba za watoa huduma wanaotakiwa kufanyakazi kwenye maeneo hayo” alisema Dkt. Nchemba.
Pia waziri huyo wa fedha wa Tanzania alifika katika Kasri ya Al Watan (Qasr Al Watan) na kuwasilisha Salaam kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwenda kwa mwana wa mfalme wa Abu Dhabi His Highness Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan aliye pia naibu amiri jeshi mkuu wa majeshi (Crown Prince of Abu Dhabi and Deputy Supreme Commander of the Armed Forces).



medium_2021-12-16-b52b50b51d.jpg

His Highness Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Crown Prince of Abu Dhabi and Deputy Supreme Commander of the Armed Forces, received a written message from Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of Tanzania, regarding the development of relations between the two countries.
The message was received by His Highness Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan, Deputy Prime Minister and Minister of Presidential Affairs, when His Highness received today at Qasr Al Watan His Excellency Mwigulu Nchemba, Minister of Finance and Planning of Tanzania.
During the meeting between His Highness and the Tanzanian delegation, they discussed the friendly relations between the UAE and Tanzania, development opportunities, economic partnership and enhancing trade exchange between the two countries .

Source : Mohamed bin Zayed receives Tanzanian President's note
 
..DENI LA TAIFA ni mjadala endelevu ktk mataifa mengi.

..Na sio ajabu wanachama wa chama kimoja kutofautiana kimsimamo kuhusu ukubwa au udongo wa deni la taifa.

..hata kwa Wamarekani fedha za mpango wa uchumi wa Raisi Joe Biden zimekwama kupitishwa kwasababu ya msimamo wa Senator mmoja wa chama chake.

..Yaani bila kura ya huyo Senator pesa haitoki kwasababu Democrats hawana masenator wa kutosha kupitisha huo mpango.

..Wanasiasa wa Tz wajifunze kutofautiana bila kujengeana UADUI.
 
Ndungai angelalamika hivi enzi za JPM sijui ingekuwaje. Ila nimeshangaa kwenye uwekaji huo wa jiwe la msingi hakuwepo na shghuli imefanyika mkoani kwake.
 
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
Ndu"gay Ni mnafiki mmoja wakupuuzwa
 
Magufuli alikopa zaidi ya trillion 30 peke yake ndani ya miaka 5 tu, lakin Huyo Ndugai hakuongea kitu. Lakin huyu mama amekopa trillion 1.3 Ndugai anapiga kelele kila mahali!
Ndugai Ni team sukuma gang, dawa mama apige chini masalia yote ya magufuli
 
Ndugai ni Spika Ndugu...

Bungeni ndio mahali Sukuma Gang wananguvu... umeona mama yenu alivopanic leo...

Na Subirini bunge lazima hii serikali ikwame
Nadhani wewe Ni mtoto wa Juzi!

Hii sio hile ccm ya mazuzu na washamba, ngojeni tutawatia adabu kenge nyinyi!
 
Ndugai apumzike sasa kutawala miaka 20 pale kijijini kongwa na bado wagogo wanakula ubuyu inatosha.
 
Back
Top Bottom