Rais Samia ampokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Ikulu Dar es Salaam leo Machi 30, 2023

Maelezo mengi hakuna lolote ,ule mkwala wa Obama wa power Africa ulikuwa hivihivi tu

USSR
 

BBC
Makamu wa Rais wa Marekani Kamla Harris ametangaza ushirikiano na Tanzania katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi kisiasa na kijamii.
Bi Harris vilevile ameipongeza serikali ya Tanzania katika suala zima la usimamizi wa demokrasia huku akisisitiza ushirikishwaji zaidi wa wanawake katika demokrasia ambapo ametangaza Marekani kutoa kiasi cha dola bilioni moja kusaidia wanawake katika eneo hilo.
Marekani inatarajia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024.
Katika hatua nyingine hapo kesho march 31 wizara ya Biashara na Viwanda ya Tanzania na Wizara ya Biashara ya Marekani zinatarajia kusaini Hati ya Makubaliano (MOU) kuanzisha majadiliano rasmi ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Katika mwaka wa fedha 2024, utawala wa rais Biden umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusiana na demokrasia, haki na utawala nchini huku maeneo mengine ya uwekezaji pia yakigusiwa katika ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Makamu wa Rais wa Marekani aanza ziara yake ya siku tatu Tanzania​



Ikulu ya rais TanzaniaCopyright: Ikulu ya rais Tanzania
Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia SuluhuImage caption: Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia Suluhu
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris yuko nchini Tanzania katika ziara yake ya siku tatu. Huu ni mwendelezo wa ziara ya nchi tatu za Afrika, ikiwemo Ghana na Zambia.
Hii leo amepokelewa na mwenyeji wake rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyu wa ngazi ya juu katika uongozi wa rais wa Marekani Joe Biden kutembelea taifa hili la Afrika Mashariki ambalo amelisifu kwa kudumisha amani.
Ndege yake, imegusa ardhi ya Tanzania saa tano usiku wa jana huku akipokelewa kwa vifijo na nderemo.
Mbali na mambo mengine, Kamala Harris pia ametumia ziara yake hiyo kuhimiza kujengewa uwezo na kuwezeshwa kwa wanawake, hasa ikizingatiwa kwamba, yeye ni miongoni mwa wanawake walioweka historia ya kuwa makamu wa rais wa kwanza kutoka nchini mwake kutembelea nchi ambayo inaongozwa na raiskiongozi mwanamke.
Rais Samia amesema jambo hilo, limeleta faraja kubwa na kutia hamasa miongoni mwa wanawake.
“Marekani itaendeleza jitihada zake za kudumisha uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, kukuza demokrasia lakini vile vile kumuimua mwanamke. Kwa sababu kuinua mwanamke mmoja ni sawa na kuinua familia nzima,” amesema Harris.
Ujio wa kiongozi huyo, ni mwitikio wa mwaliko wa rais Samia Suluhu Hassan lakini pia ni matokeo ya jitihada za diplomasia ya nchi hasa baada ya kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita. Hii inaonekana kufungua milango ya diplomasia kwa jumuia ya kimataifa.
Marekani na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa kibiashara wa muda mrefu ambao thamani yake ni dola za kimarekani takriban , $424m huku uwekezaji wa Marekani nchini Tanzania ukifika dola bilioni moja. Mbali na hivyo, serikali ya Marekani imekusudia kutoa msaada wa dola za kimarekani 560 kama msaada rasmi kwa mwaka 2024.
“Matumaini ni makubwa miongoni mwa watanzania, hasa wafanyabiashara, ambao matarajio yao makubwa ni kwamba ziara hii itadumisha ushirikiano na hivyo kuongeza uwekazaji.”
Ikumbukwe kwamba, Kamala analitembelea bara la Afrika katika kipindi ambacho China inaonekana kuwa na ushawishi mkubwa barani humo hasa ikizingatiwa kwamba, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uwekezaji mkubwa kutoka taifa hilo. Hii ni dhahiri kwamba, mataifa yenye nguvu duniani yanaliangalia bara la Afrika kama sehemu muhimu ya kupimana nguvu na kuongeza ushawishi.
Kamala, ambae ziara yake inaisha rasmi hapo kesho nchini Tanzania, anaekelea nchini Zambia ambapo atahitimisha safari yake ya nchi tatu barani Afrika.
 
Haha kuna mafisadai wanazisubiri kwa hamu walu wapige 100m usd
 
Marekani watupe na msaada wa kukabiliana na wezi wa hizo pesa, tuna matatizo mengi sana nchi hii.

Na kuhusu ushoga vipi wakati tumeshachukua pesa zao, hicho kiburi cha kupinga hadharani kitoke wapi?!

Huu ushoga sasa naona kila mmoja aisemee nafsi yake, serikali yetu ina mambo mengi sana nayo inachoka akili!
 
Rais Samia na Tanzania Kwa Ajili ya hatua za kidemokrasia na Kulinda Haki za binadamu ambazo zimechukukiwa na Rais Samia kinyume na Mtangulizi wake JP Magufuli.

Kwa hiyo ilo jarada limeandika kama wewe ulivyo andika hapo juu au ni chuki zako
Huyu ni mmoja wa genge kubwa tu humu ambao kazi yao ni kubandika maneno yaliyojaa chuki. Hakuna posti anayotoa isiyo na tusi la kidizaini. Huwezi kuwa Mtanzania halafu unajitukana. Haiwezekani. Na kama ukiona hivyo, ujue huyo mtu amepungukiwa kitu au anapata kitu kutokana na mapungufu yake hayo(anatumika) kwa kurusha matusi kwa Jamii nzima.....

...ina nifikisha kudai kuwa aidha anatumika kulisha madubwasha yaani Ai bots au yeye ni Ai bot, manake sio kawaida.....Uwasilishaji wake wa Taarifa una utata.
 
Kwa sasa hivi msaada tunaoweza kuupata kutoka nchi yoyote ile duniani na ukawa ni wa maana kubwa kwa nchi yetu ni kutupa uwezo sisi wananchi kukabiliana na mafisadi na wakwapuzi walioenea kila mahala nchini mwetu.

Haya mengine yote ni mchezo uleule wa kutuweka chini ya himaya zao.
 
Hivi Makao Makuu ya nchi si yalishaenda Dodoma na Kwa gharama kubwa sana.
Ya Dar si imebakia mjengo.
 
Serikali ya Marekani imeahidi Kuipatia Tanzania Msaada rasmi wa Fedha Dola milioni 560 sawa na Tilioni 1.3 ikiwa na kuimarisha ushirikiano wake.

Hayo yameelezwa na VP Kamala jijini Dar wakati wa Mazungumzo yake ni Rais Samia..

Hii Sio mara ya kwanza Kwa Marekani Kuipatia Tanzania pesa nyingi kwani kabla ya Magufuli tayari Tanzania ilikuwa inapata zaidi ya dola mil.700 Kwa mwaka za MCCL ambazo zilisidia ujenzi wa Barabara za Songea Hadi Masasi, Sumbawanga Hadi Tunduma na Umeme Kigoma nk..

My Take.

Akufaaye Kwa Dhiki Ndio rafiki na Demokrasia inalipa.

Naipenda sana Marekani na sera zake nayo inaipenda Tanzania Kwa Ajili ya geopolitics ila Watanzania hatujuikutumia fursa..

Tukicheza vizuri tutakuwa kama Egypt via mapesa ya Marekani..

 
Nakubaliana na wewe ila ndiyo mambo ya utawala bora na demokrasia hayo ambayo hatujawa na nia ya dhati kuyafuata. Tumekuwa na taasisi zinazotakiwa kudhibiti mwenendo wa serikali kama Bunge, Ofisi ya CAG na TAKUKURU lakini ona tunavyozichezea matokeo yake pesa za kuendesha hizo taasisi zinapotea bure.

Kwa hiyo inaanza na sisi wenyewe kuamua kupata kweli hilo unalolisema.
 
Hivi watanzania wanaelewa maana ya demokrasia na haki za binadamu kama zinavyofahamika na marekani? Kwa marekani demokrasia na haki za binadamu zinaambatana na na haki za mashoga almaarufu kama LGBT!! Ukikubali demokrasia na haki za binadamu zinazoigiwa debe na marekani duniani kote maana yake ni kukubali haki za mashoga! Misaada hii iliyoahidiwa ya mamilioni ya dola za marekani itatekelezeka kwa masharti ya uhuru wa haki za binadamu ikiwemo ya LGBT! Hii ni hatua ya kwanza ambayo lugha ya awali inayotumika hadharani ni DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU!! Wakati wa kutaka kuokea hiyo misaada ndio ufafanuzi wa demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani hufuata na hao ndio suala la haki za mashoga/LGBT hujitokeza!! Je tutakua na ubavu wa kukataa misaada hii lukuki?? Yetu macho!! Ila Malawi walishindwa wakajikuta wanahalalisha ushoga rasmi!!

Taarifa ya Marekani iliyotolewa rasmi kuhusu makubaliano ya demokrasia na haki za binadamu hii hapa:

• Kuimarisha Haki za Kidemokrasia na Utawala Bora:
Katika maombi yake ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024, utawala wa Biden-Harris umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusu demokrasia, haki na utawala nchini Tanzania. Hili ni ongezeko kubwa la msaada kwa jitihada za Tanzania katika eneo hili. Zaidi ya hayo, USAID imeichagua Tanzania kama nchi itakayopokea usaidizi kusaidia jitihada zake za kukuza ushiriki wa wanawake na wasichana katika uongozi wa kiraia na kisiasa, hivyo kutoa takriban Dola za Kimarekani Milioni 1 za ziada kugharimia programu hizi kuanzia mwaka huu.

Huko GHANA Makamu wa rais wa Marekani ambako ndiko alikoanzia ziara yake barani afrika hakumung'unya maneno kuhusu mfungamano wa demokrasia na haki za mashoga-LGBT. Huu hapa msimamo wake wakati anaongea na Rais wa GHANA:


In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”

Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”

Tusijidanganye kuwa msimamo huo wa Marekani kuhusu haki za binadamu na ushoga utabadilika hapa Tanzania tofauti na kwingineko!! Wamesema kabisa kuwa hilo halitabadilika na ni sehemu muhimu sera ya nchi za nje ya marekani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…