Rais Samia ampokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Ikulu Dar es Salaam leo Machi 30, 2023

Katika maeneo mengine sina shida, hasa ya kiuchumi na kisiasa. Lakini eneo la msaada wa kijamii na la wanawake, halafu yakichagizwa na maneno matamu ya suala zima la usimamizi mzuri wa demokrasia kidogo hapo nina "zoom" ili kuzidi kujionea.
View attachment 2571129
BBC
Makamu wa Rais wa Marekani Kamla Harris ametangaza ushirikiano na Tanzania katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi kisiasa na kijamii.
Bi Harris vilevile ameipongeza serikali ya Tanzania katika suala zima la usimamizi wa demokrasia huku akisisitiza ushirikishwaji zaidi wa wanawake katika demokrasia ambapo ametangaza Marekani kutoa kiasi cha dola bilioni moja kusaidia wanawake katika eneo hilo.
Marekani inatarajia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024.
Katika hatua nyingine hapo kesho march 31 wizara ya Biashara na Viwanda ya Tanzania na Wizara ya Biashara ya Marekani zinatarajia kusaini Hati ya Makubaliano (MOU) kuanzisha majadiliano rasmi ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Katika mwaka wa fedha 2024, utawala wa rais Biden umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusiana na demokrasia, haki na utawala nchini huku maeneo mengine ya uwekezaji pia yakigusiwa katika ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Makamu wa Rais wa Marekani aanza ziara yake ya siku tatu Tanzania​

Ikulu ya rais TanzaniaCopyright: Ikulu ya rais Tanzania
Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia SuluhuImage caption: Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia Suluhu
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris yuko nchini Tanzania katika ziara yake ya siku tatu. Huu ni mwendelezo wa ziara ya nchi tatu za Afrika, ikiwemo Ghana na Zambia.
Hii leo amepokelewa na mwenyeji wake rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyu wa ngazi ya juu katika uongozi wa rais wa Marekani Joe Biden kutembelea taifa hili la Afrika Mashariki ambalo amelisifu kwa kudumisha amani.
Ndege yake, imegusa ardhi ya Tanzania saa tano usiku wa jana huku akipokelewa kwa vifijo na nderemo.
Mbali na mambo mengine, Kamala Harris pia ametumia ziara yake hiyo kuhimiza kujengewa uwezo na kuwezeshwa kwa wanawake, hasa ikizingatiwa kwamba, yeye ni miongoni mwa wanawake walioweka historia ya kuwa makamu wa rais wa kwanza kutoka nchini mwake kutembelea nchi ambayo inaongozwa na raiskiongozi mwanamke.
Rais Samia amesema jambo hilo, limeleta faraja kubwa na kutia hamasa miongoni mwa wanawake.
“Marekani itaendeleza jitihada zake za kudumisha uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, kukuza demokrasia lakini vile vile kumuimua mwanamke. Kwa sababu kuinua mwanamke mmoja ni sawa na kuinua familia nzima,” amesema Harris.
Ujio wa kiongozi huyo, ni mwitikio wa mwaliko wa rais Samia Suluhu Hassan lakini pia ni matokeo ya jitihada za diplomasia ya nchi hasa baada ya kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita. Hii inaonekana kufungua milango ya diplomasia kwa jumuia ya kimataifa.
Marekani na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa kibiashara wa muda mrefu ambao thamani yake ni dola za kimarekani takriban , $424m huku uwekezaji wa Marekani nchini Tanzania ukifika dola bilioni moja. Mbali na hivyo, serikali ya Marekani imekusudia kutoa msaada wa dola za kimarekani 560 kama msaada rasmi kwa mwaka 2024.
“Matumaini ni makubwa miongoni mwa watanzania, hasa wafanyabiashara, ambao matarajio yao makubwa ni kwamba ziara hii itadumisha ushirikiano na hivyo kuongeza uwekazaji.”
Ikumbukwe kwamba, Kamala analitembelea bara la Afrika katika kipindi ambacho China inaonekana kuwa na ushawishi mkubwa barani humo hasa ikizingatiwa kwamba, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uwekezaji mkubwa kutoka taifa hilo. Hii ni dhahiri kwamba, mataifa yenye nguvu duniani yanaliangalia bara la Afrika kama sehemu muhimu ya kupimana nguvu na kuongeza ushawishi.
Kamala, ambae ziara yake inaisha rasmi hapo kesho nchini Tanzania, anaekelea nchini Zambia ambapo atahitimisha safari yake ya nchi tatu barani Afrika.
"Bi Harris vilevile ameipongeza serikali ya Tanzania katika suala zima la usimamizi wa demokrasia huku akisisitiza ushirikishwaji zaidi wa wanawake katika demokrasia ambapo ametangaza Marekani kutoa kiasi cha dola bilioni moja kusaidia wanawake katika eneo hilo"
 
tuomba kufahamu kama huo msaada una masharti yoyote?
umasikini ni mbaya sana
Masharti ya Marekani Yako wazi ni Demokrasia na Haki za binadamu ndio principal zao,Nchi zinzofuata hivyo inakuwa ni kufaulu Kwa ushawishi wa Marekani wa sera zake za Nje.

Ni kweli umaskini ni mbaya ila maskini mwenzio hawezi kukutoa kwenye umaskini ni wewe mwenyewe kucheza vyema na tajiri.
 
View attachment 2571129
BBC
Makamu wa Rais wa Marekani Kamla Harris ametangaza ushirikiano na Tanzania katika maeneo mbali mbali ya kiuchumi kisiasa na kijamii.
Bi Harris vilevile ameipongeza serikali ya Tanzania katika suala zima la usimamizi wa demokrasia huku akisisitiza ushirikishwaji zaidi wa wanawake katika demokrasia ambapo ametangaza Marekani kutoa kiasi cha dola bilioni moja kusaidia wanawake katika eneo hilo.
Marekani inatarajia kutoa Dola za Kimarekani milioni 560 kama msaada rasmi kwa Tanzania katika mwaka wa fedha wa 2024.
Katika hatua nyingine hapo kesho march 31 wizara ya Biashara na Viwanda ya Tanzania na Wizara ya Biashara ya Marekani zinatarajia kusaini Hati ya Makubaliano (MOU) kuanzisha majadiliano rasmi ya kibiashara baina ya nchi hizo mbili.
Katika mwaka wa fedha 2024, utawala wa rais Biden umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusiana na demokrasia, haki na utawala nchini huku maeneo mengine ya uwekezaji pia yakigusiwa katika ushirikiano kati ya Marekani na Tanzania.

Makamu wa Rais wa Marekani aanza ziara yake ya siku tatu Tanzania​

Ikulu ya rais TanzaniaCopyright: Ikulu ya rais Tanzania
Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia SuluhuImage caption: Makamu wa rais wa Marekani bi kamala Harris kushoto na mwenyeji wake Mama Samia Suluhu
Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris yuko nchini Tanzania katika ziara yake ya siku tatu. Huu ni mwendelezo wa ziara ya nchi tatu za Afrika, ikiwemo Ghana na Zambia.
Hii leo amepokelewa na mwenyeji wake rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyu wa ngazi ya juu katika uongozi wa rais wa Marekani Joe Biden kutembelea taifa hili la Afrika Mashariki ambalo amelisifu kwa kudumisha amani.
Ndege yake, imegusa ardhi ya Tanzania saa tano usiku wa jana huku akipokelewa kwa vifijo na nderemo.
Mbali na mambo mengine, Kamala Harris pia ametumia ziara yake hiyo kuhimiza kujengewa uwezo na kuwezeshwa kwa wanawake, hasa ikizingatiwa kwamba, yeye ni miongoni mwa wanawake walioweka historia ya kuwa makamu wa rais wa kwanza kutoka nchini mwake kutembelea nchi ambayo inaongozwa na raiskiongozi mwanamke.
Rais Samia amesema jambo hilo, limeleta faraja kubwa na kutia hamasa miongoni mwa wanawake.
“Marekani itaendeleza jitihada zake za kudumisha uhusiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara, kukuza demokrasia lakini vile vile kumuimua mwanamke. Kwa sababu kuinua mwanamke mmoja ni sawa na kuinua familia nzima,” amesema Harris.
Ujio wa kiongozi huyo, ni mwitikio wa mwaliko wa rais Samia Suluhu Hassan lakini pia ni matokeo ya jitihada za diplomasia ya nchi hasa baada ya kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita. Hii inaonekana kufungua milango ya diplomasia kwa jumuia ya kimataifa.
Marekani na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa kibiashara wa muda mrefu ambao thamani yake ni dola za kimarekani takriban , $424m huku uwekezaji wa Marekani nchini Tanzania ukifika dola bilioni moja. Mbali na hivyo, serikali ya Marekani imekusudia kutoa msaada wa dola za kimarekani 560 kama msaada rasmi kwa mwaka 2024.
“Matumaini ni makubwa miongoni mwa watanzania, hasa wafanyabiashara, ambao matarajio yao makubwa ni kwamba ziara hii itadumisha ushirikiano na hivyo kuongeza uwekazaji.”
Ikumbukwe kwamba, Kamala analitembelea bara la Afrika katika kipindi ambacho China inaonekana kuwa na ushawishi mkubwa barani humo hasa ikizingatiwa kwamba, katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na uwekezaji mkubwa kutoka taifa hilo. Hii ni dhahiri kwamba, mataifa yenye nguvu duniani yanaliangalia bara la Afrika kama sehemu muhimu ya kupimana nguvu na kuongeza ushawishi.
Kamala, ambae ziara yake inaisha rasmi hapo kesho nchini Tanzania, anaekelea nchini Zambia ambapo atahitimisha safari yake ya nchi tatu barani Afrika.

Majizi yameshika calculator tayari kiweka figure kwenye invoice
 
 Capitalism and corruption are brother and sister if we real want to eradicate corruption we must welcome socialism, take example of China, Russia, North Korea etc.
 
Jarida la The African News linaripoti kwamba,Ziara ya VP Kamala Tanzania ni kuonesha Uungwaji Mkono wa Serikali ya Biden Kwa Rais Samia na Tanzania Kwa Ajili ya hatua za kidemokrasia na Kulinda Haki za binadamu ambazo zimechukukiwa na Rais Samia kinyume na Mtangulizi wake JP Magufuli.

Wahuni tu hao ..kama wana mpunga waende wakamlize vita huko Somalia, Congo na Ethiopia.

Tangu lini mzungu akaipenda ngozi nyeusi..mnakatazwa kutumia dawa za kienyeji mkidaganywa kuwa ni ushirikina muda huo huo wanatumia mimea kutengeneza dawa.

Poor Africa.
 
Wao ndio waliwaambia wapigane? Muuane nyie alaumiwe Marekani?Acha ujinga
 
Serikali ya Marekani imeahidi Kuipatia Tanzania Msaada rasmi wa Fedha Dola milioni 560 sawa na Tilioni 1.3 ikiwa na kuimarisha ushirikiano wake.

Hayo yameelezwa na VP Kamala jijini Dar wakati wa Mazungumzo yake ni Rais Samia..

Hii Sio mara ya kwanza Kwa Marekani Kuipatia Tanzania pesa nyingi kwani kabla ya Magufuli tayari Tanzania ilikuwa inapata zaidi ya dola mil.700 Kwa mwaka za MCCL ambazo zilisidia ujenzi wa Barabara za Songea Hadi Masasi, Sumbawanga Hadi Tunduma na Umeme Kigoma nk..

My Take.

Akufaaye Kwa Dhiki Ndio rafiki na Demokrasia inalipa.

Naipenda sana Marekani na sera zake nayo inaipenda Tanzania Kwa Ajili ya geopolitics ila Watanzania hatujuikutumia fursa..

Tukicheza vizuri tutakuwa kama Egypt via mapesa ya Marekani..

Obama alikuja bongo 2013 ni kipi kimebadilika ...acheni mawazo mgando.
 
Hujui kitu ila unapayuka tuu..

Wewe ndio ulitoa pes za kujenga Barabara ya Tunduma Sumbawanga?

Au wajomba zako ndio wlitoa pesa za kujenga Barabara ya Songea Masasi?

Au wewe ndio Huwa unatoa pesa za malaria,kifua Kikuu,ukimwi na chanjo?
 
Back
Top Bottom