Kwahiyo penye upinzani mkali Mwendazake aliweka kibaraka - kidikteta kidogo kufanyizia upinzani kama ilivyokuwa akisema. Ok-. Tuseme mama ameamua kupiga deki nchi, kurejesha amani, heshima, umoja na maelewano. Sasa tuseme Bw. Polepole tayari, Bashiru tayari, Biswalo tayari na sasa Sabaya tayari wako pembeni.
Hebu tuendelee kumsaidia mama ili yale macho yake yaliyolegea yawaone waliobaki, walioharibu taswira ya nchi kwa kisingizio cha uzalendo!
Mimi ninaowajua ni hawa wafuatao:
1) Spika Ndugai - huyu hakuna haja ya kutumia bunge kumng'oa. Huyu atengenezewe zengwe kwenye chama halafu apokonywe kadi ya chama tu! Ndiyo njia rahisi! Kumbuka hata Jumbe alipokonywa kadi ya CCM akapoteza Urais!
Kwa ufupi Spika haijatambua kuwa Magufuli hayupo tena! Bado anadhani kuna ushirika wa mihimili kutenda maovu.
2) Very James UVCCM! Huyu naye kichwa kibovu, aondoke zake akawe UVCCM Chato!
3) Charamila RC Mbeya! Maneno mengi ya kashfa na dharau kwa watanzania! Aende Chato akaabudu kaburi la Mwendazake!
4). Huyu Biswalo naye angefanyiwa uchunguzi ili tuweke nchi sawa. Kuna watu wana maumivu makali sana yaliyosababishwa na huyo jamaa.
5). Bashite. Pamoja na kuwa yuko pembeni lakini alifanya maovu mengi ya kuhatarisha amani ya nchi. Wananchi wana machungu sana kuona anazurura tu mtaani wakati kadhulumu haki za watu. UTAWALA BORA uheshimiwe.
6) Cypriam Msiba! Huyo ni wa kukamata na kuficha. Hafai kuishi kwenye jamii iliyo staarabika!
Hebu na wewe fichua wengine. Hakika Mama anaona sana japo macho yamelegea!
NAWASALIMU KWA JINA LA JAMUHURI YA TANZANIA---- KAZI IENDELEE!