Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

niliwahi kumuona huyu jamaa akimshusha mfiwa katika gari, akamlaza chini na kumkanyaga shingoni mbele ya familia yake waliokuwa katika gari, zama zake zimefika kikomo atavuna alichopanda kwa aliowatenda
 
niliwahi kumuona huyu jamaa akimshusha mfiwa katika gari, akamlaza chini na kumkanyaga shingoni mbele ya familia yake waliokuwa katika gari, zama zake zimefika kikomo atavuna alichopanda kwa aliowatenda
Weeee wapi huko[emoji22]
 
Stupid text!
 
Yale machozi aliyotoa kumlilia JPM yalikuwa ya kweli kabisa.

Wenzake wa juu wqlijiwekea kinga ya kutoshtakiwa. Hawa wa chini ndio watapata tabu sana kulipia uovu wao.
 
Ebu acheni vituko! Hizo zote ni allegations za mtumishi wa umma chini ya uangalizi mahiri wa JPM, inawezekana je 😜!
Sio kweli ni majungu tu hayo!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] I see..huu Ni utoto..alikuwa na utoto
 
Kama haya yaliyoandikwa yatakuwa ni kweli kwa asilimia kubwa basi nchi hii ilikosa Utawala Bora kwa asilimia 100 kwa baadhi ya Taasisi. Watu waliogopa Mamlaka kama ukoma. Tunaiomba Tume ya Uchunguzi ifanye kazi yake kwa weledi mkubwa bila kumuonea. Iwaite wahenga wote waeleze ukweli kwa yale yote waliotendewa. Kwa maelezo hayo hapo juu huyu mtu anatakiwa kufikishwa Mahakamani kama itathibitika hayo yaliyosemwa yana ukweli.
 
Anayefahamu anijzulishe ni kwa nini alipambana sana na Bw Swai?.

Maana Swai si Mwanasiasa.
Swai ni suporter wa Upinzani Na ni mbishi mchagga yule hawezi toa hela kirahisi rahisi ni fighter Sabaya akaona isiwe tabu nitamtengenezea mizengwe ya kila aina.
 
Akitumbuliwa wewe unapata faida ipi
Haiyumkini wewe ni mnufaika muhimu wa madhila ya huyo sabaya wako! Ama utakuwa nyumbandogo au baunsa wake!
Yaani kwa akili zako timamu unashangilia na kuuhusudu ubazazi wa jambarka Hilo? Pytuuuuh! Nimekudharau na kukutema Kama tope la ugoro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…