Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Duh! Alisalimika kweli?!?

Alishindwa walinzi walishindwa kumuonyesha lakini walinzi walipewa kichapo! Sijui jamaa akili zake zikoje,mademu kibao wakali mashombe shombe warito warito na yeye mpunga wa dhulumati anao kibao sijui kwanini asingewatafuta akawalamba au kama anashindwa si angekuwa anaongea na stivie nyerere ampe connection.
 
Huyu sabaya Ni mshenzi sana tulikuaga nae Kwenye Pub moja Blue house fire daraja mbili alikuwa akija usku sana na mabausa kwa ubabe mwingi mziki unazimwa kisha anatajwa na Dj kama Pedeshee mkuu wa Wilaya Ya Hai Ole Sabaya, kisha anachukuwa Mike anatuimbia nyimbo za Ken Rodgers
Anaendaga gym pia na genge lake la wahuni huko arusha. Nikamwuliza vipi? Amekuharass pia? Bro akanijibu huwa mafia anakua harassed?[emoji23][emoji23] basi nikatulia
 
Eti ubinadamu, kweli unajielewa wewe..............umedokeza kulikuwa na three attempts (this is a serious clue to be pursued now and revealed for the cause of action.

Ndio maana tunasema karma hits on both sides at calculable timing which will reciprocate accordingly.
Hahahahaha. Lete mvinyo tusherehekee. Hakuna kipindi Mungu ameitetea Tanzania kama mwaka 2021
 
Sabaya atalipa gharama ya uovu wake.
Kwa hapa Arusha, ngoja watu waanze kupata pesa. Atapigwa pumbu tu. Hiyo ni guarantee malamamaee!! Kama alipigwa chuma Erasto Msuya na mabilioni yake na uchawi wake wote. Sabaya ni panya mdogo sana.. it's a matter of time..
 
Sabaya akimaliza kesi ya duniani atakutana na nyingine ya mbinguni hafai, ndio maana mwendazake alivyoondoka jamaa alilia akijua na yeye kinga yake imeondoka, kweli amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu.
 
Na akionekana hana hatia atarejeshwa kazini na kulipwa stahiki zake zote zilizosimamishwa.

Lakini ninavyoelewa tuhuma yoyote dhidi ya viongozi wa kariba yake huwa ndiyo mwisho wa uteuzi.

Sasa kwa barua hiyo ya ikulu, inamaanisha kibarua bado anacho uchunguzi ukimsafisha, vinginevyo angelikuwa kateuliwa mwingine kushika nafasi yake.
Huyu harudi,hata utendaji kata hapewi
Ana makandokando mengi...ile kujifanya
Anapigania wanyonge nk,ile ilikuwa boshen
Tu

Ova
 
Siku utakapoguswa wewe mama D huo upepo wa bendera utaupunga vinginevyo. Hapo hujatambua tu ndani serikali iliyopita ndani kwa ndani walikuwa hawapatani na chokochoko zilikuwa nyingi. Walishughulikiana kimya wenyewe kwa wenyewe nyie huku nje mkikenue kumwaga sifa.

Sikiliza mama, ni hivi mama anaadabisha vifaranga vyake kwa hasira kwa kuwa vilikuwa vinamdharau enzi hizo, kwa yakini atawasambaratisha kweli, vifaranga pamoja na udogo wao wataondoka kwenye himaya kwenda kujitafutia bila kuogopa hatari mwewe nje. Vifaranga watapambana kimya kimya kulinda uhai wao hatimaye watakuwa wazima hata hivyo hatarejea kumsalimia mama. Baada ya kumaliza zoezi la kushughulikia vifaranga vyake na vikatoweka kwenye mbele yake na usumbufu kupungua, Mama atabaki mpweke, watu wazima walikuwa wakishangilia mama kuwashughulikia vifaranga vyake hawatamfariji kwa kuwa na wao wanahitaji kukaa kwenye kiota hicho.

Msimu wa mvua utawadia, mama atakimibilia kwenye kiota akidhani atwakuta vifaranga wamerejea nyumbani ili awapashe joto, lakini wapi

Kiangazi hicho kinafika kwa msimu wa mavuno, kwenda shambani anakuta mazao yote wametafuna wale walioukuwa wakimshangilia, yeye hana akiba ya chakula, kisha anaanza safari za kuingia msituni kujitafutia chakula na ahitaji mengine

Wawindaji wanaingia msituni na kuchioma moto ili kuwaibua wanyama waliwao wawawinde, kiota cha mama kiko katikati ya mstu huo na yeye yuko mbali anahea kwa ajili ya familia. Kwa mbali anaona moto unaotoa moshi, anabeba furushi dogo ili awahi kwenye kiota kuzuia kisiungue moto, lakini inashindikana................ndipo anajitokeza mama mmoja jamii ya mbuni ambaye na yeye ana mayai yake kwenye ardhi ndani ya huo msitu anakimbia kwa ksai ya kilomita 70 kuelekea mtoni anafika anjiloweka kwenye maji kisha kwa kasi ile ile anarejea kwenye tawa la mayai yake na kuzima moto ambao tayari ulikuwa umefika eneo hilo. Mama anayehea msituni naye anafika kwenye kiota chake huku akimtizama mbuni anavyoyalinda mayai yake kwa upendo, wakati kiota chake kisicho na vifaranga wala mayai kikiteketea kwa moto bila msaada wa jeshi kubwa lililoonekana kumpa moyo mama. Kisha mama anajawa na mawazo na kufanya maamuzi ya kuhama huku akiwa amepata hasara isiyoelezeka.
Mtaimba mapambiyo yote. Mtaandika fasihi simulizi zote. Mtaimba kwa code na note ila mjue CCM halisi ndiyo iko madarakani. Mungu ni fundi. Mlinyanyasa Watanzania mpaka Chama Cha Mapinduzi???? Leta mvinyo. Mtasafishwa nyote na. hakuna kifaranga kitapona. Ulia mbali vyote.
 
Mpenda haki yoyote lazima
Ashangilie,hivi yule diwani aliyepigwa
Alikuwa wa chama gani????

Ova
 
Mmmh mbona tuhuma nyingi sana as if waliokua wanafanyiwa hayo kama nikweli wao walikua wasafi ?Nyuma hakuna watu walio umizwa na hao wafanya biashara wanaotetewa? ama kweli uchunguzi ufanyike haraka hapo kuna kiladalili za kupakana matope siasa ni mchezo mchafu sana. Lakini nano kuendesha uchunguzi huru na wahaki I'll upande wowote usionewe?
 
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hawa pichani ni waliokuwa walinzi wa Freeman Mbowe. Kuna Khalifa Hassan, Adam Kasekwa (ADAMO) na Mohamed Lingwenya.. Freeman Mbowe aliongeza ulinzi wa kutembea nao baada ya kuvamiwa Dodoma na kuvunjwa mguu wake wa kulia.

Wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu (aliyekuwa DC wa HAI) Lengai Ole Sabaya na genge lake walivamia hotel ya Freeman Mbowe inaitwa 'Protea Hotel Aishi Machame', huko Hai, wakawakamata hawa watu, wakapewa kesi ya UGAIDI. Pia wakabebeshwa mzigo wa nguo na sare za JWTZ na wakaambiwa wamekutwa nazo, wakapewa na vilipuzi.

Mashtaka mengine ni kukutwa na silaha pamoja na dawa za kulevya aina ya Heroin.. Waliteswa sana. Walipigwa sana. Waliumizwa sana. Tazama makovu yao. Waone walivyokondeana. Hawa wanaishi Tundu la choo hapa, pua zao hapa. Wapo gereza la Segerea.

Wanafungiwa private cell. Kila mmoja room yake. Hawatoki nje isipokuwa saa 11 alfajiri wakati wa kufunguliwa, kuhesabiwa na kupewa uji, saa 3 asubuhi kupewa ugali maharage, na saa 9 mchana wanafungiwa. Muda wote wamefungwa pingu kwenye miguu na mikono yao. Upelelezi haujawahi kukamilika.

Mahakamani hawapelekwi na hata usikilizwaji wa kesi kwa njia za video hawafanyiwi. Mahakama ni kama imewasahau. Sio sawa kabisa hii. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuna watu wanateseka sana kwa sababu ya amri za SABAYA. Wapo wengi, hawa ni baadhi.

Tunamtaka DPP aharakishe upelelezi wa kesi ya hawa ndugu zetu wenye familia zao au vinginevyo, awaachie huru watu hawa wanateseka bila hatia.. Hizi ni roho chafu na hila za shetani. Nchi yetu sio ya kidikteta.. SABAYA amewaumiza sana watu HAI. Ushahidi upo. @ MMM

View attachment 1784238
Nimeumia sana Mbowe apambane hawa vijana watoke na wafidiwe angalau wapewe mitaji kuja kuanza maisha upya....uraiani duuu inaumiza sana
 
choko baba yako.
mungu fundi kweli kweli,ndio sababu pamoja na kuporwa kwao ubunge hakua mjinga kuruhusu machafuko,watu waliwapuuza maana mnapigania ugali tu hamna lolote.
wewe na aina yako kama nyarandu,mlikimbia chama baada ya kuona hakuna nafasi kwa mafisadi ya chama na taifa.

jpm amefariki,lakini hakuna kima yeyote atajaribu kuirudisha tz ilikokua,na wajinga wajinga wataendelea kufinywa tu,haijalishi ni ndugu zako au shemeji zako.
kabisa akina sabaya wanafinywa kiseng
 
Back
Top Bottom